Kigoma: Mganga wa Kienyeji afungwa jela maisha kwa kulawiti mtoto wa miaka 8

Kigoma: Mganga wa Kienyeji afungwa jela maisha kwa kulawiti mtoto wa miaka 8

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Mahakama ya Wilaya Kigoma Mkoa wa Kigoma imemhukumu mganga wa kienyeji, Venas Edward (48), mkazi wa Ujiji Manispaa ya Kigoma/Ujiji kutumikia kifungo cha maisha jela kwa kosa la kumnajisi mtoto wa kike mwenye umri wa miaka minane

254CDBF3-548D-43DE-973B-855863A83D99.jpeg

Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Katoki Mwakitalu, baada ya upande wa mashtaka kuthibitisha kosa hilo pasipokuacha shaka yoyote.

Hakimu Mwakitalu alisema katika kesi hiyo upande wa mashtaka ulikuwa ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Raymond Kimbe, na ulipeleka mashahidi wanne na kielelezo kimoja ambacho ni PF3.

Alisema mama wa mtoto huyo alimpeleka mtoto wake nyumbani kwa mshtakiwa kwa ajili ya kutibiwa, na baada ya kumfikisha, mganga alimtuma mama huyo aende dukani kununua wembe.

Alisema baada ya mama kwenda dukani, mshtakiwa alimfanyia mtoto huyo kitendo hucho cha kikatili.

Alieleza kuwa baadaye mama wa mtoto huyo alifika kutoka dukani na kumchukua mtoto wake na kurudi nyumbani kwake.

Alieleza zaidi kuwa baada ya muda mama alisikia mtoto wake analalamika kusikia maumivu sehemu zake za siri, ndipo mama alipomkagua na kugundua kuwa mtoto wake alikuwa amenajisiwa.

Aliendelea kueleza kuwa mama wa mtoto huyo alimbana mtoto wake kwa kumuuliza ni nani aliyekufanyia kitendo hicho ndipo alimjibu kuwa ni mshtakiwa.

Mshtakiwa huyo baada ya kuhukumiwa kwenda jela maisha, aliangua kilio hadharani na kusababisha ndugu zake nao kuanza kuangua vilio mahakamani mbele ya umati uliofika mahakamani kwa ajili ya kusikiliza hukumu hiyo.

Awali akisoma hati ya mashtaka Wakili Kimbe alidai kuwa Aprili 23, mwaka 2019 majira ya asubuhi eneo la Kasoko Ujiji, mshtakiwa alinajisi mtoto huyo na kumsababishia maumivu makali sehemu zake za siri.
 
Hivi ni kwanini watu wanategemea sana tiba mbadala?
Tba mbadala kuna baadhi ya magonjwa zinasaidia sana Sky. Kitendo alichokifanya huyo anayejiita mtaalamu wa jadi ni tabia mbaya ya mtu binafsi wala haitokani na kiagizwa na shughuli zake kama ambavyo kuna baadhi ya madaktari hubaka hadi wajawazito tena baada ya kuwachoma sindano za usingizi kama ilivyotokea hivi karibuni kule Rukwa
 
Wale madaktari ingekuwa huku kwetu Kwamtogole wangepelekwa mahakamani kwanza, majina yao kuingia kwenye sex offenders register, baada ya kumaliza kifungo watafute kazi ya kuchanganya zege.
 
Wale madaktari ingekuwa huku kwetu Kwamtogole wangepelekwa mahakamani kwanza, majina yao kuingia kwenye sex offenders register, baada ya kumaliza kifungo watafute kazi ya kuchanganya zege.
Kwa maana hiyo leseni zao za udaktari zinakua revoked for life? Sheria hiyo ije na huku Songea kwa Mfaranyaki aisee
 
Halafu Zitto hataki World Bank watuletee fedha za kuondoa Ujinga huu Kigoma
 
Kwa maana hiyo leseni zao za udaktari zinakua revoked for life? Sheria hiyo ije na huku Songea kwa Mfaranyaki aisee
Hapo bodi yao haijatoa maamuzi lakini jina likiingia kwenye sex offenders register huruhusiwi kufanya kazi na vulnerable people. Wagonjwa,wazee, watoto wote ni vulnerable.
 
asa huyu mganga nae vipi kwann hajatumia taaluma yake kuua kesi au mganga hajigangi
 
Back
Top Bottom