Kigoma: Polisi Wadaiwa kuua raia kwa risasi na kujeruhi wawili kwenye kiwanja cha mpira Lake Tanganyika

Kigoma: Polisi Wadaiwa kuua raia kwa risasi na kujeruhi wawili kwenye kiwanja cha mpira Lake Tanganyika

Muwaambie raia wawe na utulivu na wasipende kupambana na polis Eti nguvu ya umma wataumia sana,tii SHERIA bila shuruti

USSR

Nguvu ya umma ndio upige watu risasi?. Polisi anaruhusiwa kutumia risasi pale tu retaliation ya raia ni sawasawa au madhara yake Ni sawa na risasi.
 
Waha wana akili za kijinga sana.
Nadhani nimeeleweka. Polisi walikuwa wakituliza ghasia ila hao ndugu zetu wakajifanya miamba yakawakuta ya kuwakuta.

Mtaendelea kutetea polisi dhidi ya Raia mpaka lini?. Kuanzia Mauaji ya Akwelina mlitetea na hata mfanya biashara wa mtwara mlitetea mpaka leo.
 
IGP Sirro ni mtu wa hovyo hovyo kwa kuruhusu watu wa hovyo kutenda unyama kwa binadamu wenzeo na bado wakalindwa.
Wameshabadilisha IGP wa kila ain, Ila bado polisi wanaua raia wasio na hatia.
Hapa shida sio IGP tena,
 
Una wa
Waha wana akili za kijinga sana.
Nadhani nimeeleweka. Polisi walikuwa wakituliza ghasia ila hao ndugu zetu wakajifanya miamba yakawakuta ya kuwakuta.

Unawaita watu wajinga kisa tu wamepigwa risasi na polisi. Usijifanye Raia namba moja wakati hata Leo waweza pigwa shaba na polisi kiss umrdhaniwa Ni jambazi.

Refer kifo Cha imran Kombe mkurugenzi wa usalama wa Taifa aliyepigwa risasi na polisi akidhaniwa ni jambazi. So nobody is safe against police brutality.
 
Amesema licha ya kupiga risasi hizo lakini mashabiki hao waliendelea kumshambulia kwa mawe akiwa ameanguka chini ndipo alipofyatua risasi tatu na moja ilimpata marehemu Juma ambaye alijeruhiwa katika paja la mguu wa kushoto na risasi ya pili ilimjeruhi Omary Amdan (35), katika unyayo wa mguu wake wa kushoto na risasi ya tatu ilimjeruhi Nasibu Moshi (35), katika mguu wake wa kushoto.
🔦
 
Huu Ni ujinga hakuna polisi anae ruhusiwa kutumia silaha ya Moto Tena kwa mwananchi ambae Hana silaha, hata Kama hakutii sheria bado alikua na namna nyingine ya kufanya sio kuua.
Amesema mashabiki hao waliendelea kushambuliana na kuwapiga mawe askari waliokuwepo uwanjani hapo na kusababisha askari namba F.5123 D/ CPL Subira aliyekuwa na silaha aina ya AK 47 kushambuliwa sehemu ya kichwani na kuanguka chini” amesema kamanda Manyama

Tuambie namna ambayo angefanya hapa mkuu.

Tuchukulie niwewe umeangushwa chini na mawe yanamiminika na unasiraha ambayo inabidi uilinde kwa sababu kwenye huo umati sio wote ni wema mtu anaweza kupita nayo, pia ulinde uhai wako
 
Mamwera sijawahi wakubali hata kidogo lakini sometimes tuwaonee huruma,

Askari yupo chini mawe yanarushwa afu wajinga wanataka wampore AK47 ungekuwe wewe unafanyaje?
 
Back
Top Bottom