Kigoma: Polisi Wadaiwa kuua raia kwa risasi na kujeruhi wawili kwenye kiwanja cha mpira Lake Tanganyika

Kigoma: Polisi Wadaiwa kuua raia kwa risasi na kujeruhi wawili kwenye kiwanja cha mpira Lake Tanganyika

Amesema mashabiki hao waliendelea kushambuliana na kuwapiga mawe askari waliokuwepo uwanjani hapo na kusababisha askari namba F.5123 D/ CPL Subira aliyekuwa na silaha aina ya AK 47 kushambuliwa sehemu ya kichwani na kuanguka chini” amesema kamanda Manyama

Tuambie namna ambayo angefanya hapa mkuu.

Tuchukulie niwewe umeangushwa chini na mawe yanamiminika na unasiraha ambayo inabidi uilinde kwa sababu kwenye huo umati sio wote ni wema mtu anaweza kupita nayo, pia ulinde uhai wako
Yeye alienda kufanya nini hapo?
 
Vurugu hizo zilitokea jana Jumatatu Machi 14, 2022 saa 10 jioni wakati wa fainali ya mchezo wa mpira wa miguu wa kumuenzi Dk Living Stone baina ya timu ya Mwandiga Fc dhidi ya Kipampa Fc ya Ujiji ulioandaliwa na Shirika la Joy in The Harvest kwa kushirikiana na Chama cha Mpira wa Miguu Kigoma (KFA) na mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Ester Mahawe.
Kumuenzi mtu ambaye hata hakuwa na mchango wowote kwenye maendeleo yao
 
Huu Ni ujinga hakuna polisi anae ruhusiwa kutumia silaha ya Moto Tena kwa mwananchi ambae Hana silaha, hata Kama hakutii sheria bado alikua na namna nyingine ya kufanya sio kuua.
Namna ipi tueleze
 
Kupitia Twitter pia, Abdul Nondo Kaandika;

View attachment 2151568

--
Askari polisi mwenye namba F.5123 D/ CPL Subira ambaye aliyekuwa na bunduki aina ya AK 47 adaiwa kumuua Juma Ramadhani kwa kumpiga risasi na kuwajeruhi watatu wakati akiwa kwenye harakati za kujihami kwenye vurugu zilizotokea katika kiwanja cha mpira cha Lake Tanganyika mkoani Kigoma.

Vurugu hizo zilitokea jana Jumatatu Machi 14, 2022 saa 10 jioni wakati wa fainali ya mchezo wa mpira wa miguu wa kumuenzi Dk Living Stone baina ya timu ya Mwandiga Fc dhidi ya Kipampa Fc ya Ujiji ulioandaliwa na Shirika la Joy in The Harvest kwa kushirikiana na Chama cha Mpira wa Miguu Kigoma (KFA) na mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Ester Mahawe.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 15, 2022 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, James Manyama amesema marehemu Juma amefariki dunia akiwa hospitalini akiendelea na matibabu.

Kamanda Manyama amesema vurugu hizo zilitokea kipindi cha kwanza wakati Mwandiga Fc iliyokuwa ikiongoza kwa goli moja liliposawazishwa na Kipampa Fc ambapo mashabiki wa Kipampa Fc kuvamia jukwaa la mashabiki wa timu ya Mwandiga na kuanza kuwazomea huku wakiwarushia chupa za maji na mawe hali iliyosababisha kuibuka kwa vurugu.

Amesema baada ya vurugu hizo kutokea askari waliokuwa wamepangwa kwa ajili ya kuimarisha ulinzi walijitahidi kudhibiti vurugu hizo lakini walizidiwa nguvu na kuomba msaada.

"Askari waliongezeka uwanjani pale kwa ajili ya kutuliza fujo na kutumia mabomu ya machozi na kishindo kuthibiti vurugu hizo lakini mashabiki hao waliendelea kufanya fujo.

“Amesema mashabiki hao waliendelea kushambuliana na kuwapiga mawe askari waliokuwepo uwanjani hapo na kusababisha askari namba F.5123 D/ CPL Subira aliyekuwa na silaha aina ya AK 47 kushambuliwa sehemu ya kichwani na kuanguka chini” amesema kamanda Manyama

Amesema askari huyo aliamua kujihami dhidi ya tishio la kunyang’anywa silaha pamoja na kutetea uhai wake kwa kufyatua risasi tisa hewani sambamba na kutoa onyo la kuwatawanya mashabiki waliokuwa wakimshambulia kwa mawe.

Amesema licha ya kupiga risasi hizo lakini mashabiki hao waliendelea kumshambulia kwa mawe akiwa ameanguka chini ndipo alipofyatua risasi tatu na moja ilimpata marehemu Juma ambaye alijeruhiwa katika paja la mguu wa kushoto na risasi ya pili ilimjeruhi Omary Amdan (35), katika unyayo wa mguu wake wa kushoto na risasi ya tatu ilimjeruhi Nasibu Moshi (35), katika mguu wake wa kushoto.

Amesema majeruhi wote walikimbizwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa Maweni kwa matibabu na vurugu zilipotulia mchezo huo wa fainali uliendelea hadi mwisho.

Amesema saa 12 jioni Juma Ramadhani akiwa anapatiwa matibabu alifariki dunia huku majeruhi wawili walipatiwa matibabu na kuruhusiwa kwenda nyumbani huku askari Subiri alibakia kwa ajili ya matibabu zaidi.

Amesema kutokana na tukio hilo jeshi la polisi linawashikilia watu wanne wanatuhumiwa kuwa chanzo cha vurugu hizo na upelelezi wa tukio hilo bado unaendelea na watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria zaidi.

" Niwasihi wananchi wa mkoa wa Kigoma wakati wa ushabiki wa michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu washabikie kwa ustaarabu, kuvumiliana na kufuata sheria za nchi na kuacha kushabikia kwa mihemko inayosababisha vurugu,"amesema Kamanda Manyama.

Chanzo: Mwananchi
Kama askari alipiga risasi juu kuashiria watu watawanyike na wasiendelee na fujo, lakn wakakaidi na wakazidi kumshambulia askari akiwa na silaha hapo lazma silaha itumike kwa ajili ya kujihami
 
Kama askari alipiga risasi juu kuashiria watu watawanyike na wasiendelee na fujo, lakn wakakaidi na wakazidi kumshambulia askari akiwa na silaha hapo lazma silaha itumike kwa ajili ya kujihami
Wewe lazima utakuwa ni polisi au mtoto wa polisi hakuna raia katili namna hii
 
Wewe lazima utakuwa ni polisi au mtoto wa polisi hakuna raia katili namna hii
Mimi sio Polisi, ila nilipita JKT nilifundishwa hivyo. Askari unapokuwa na silaha kwa ajili ya kuimarisha ulinzi kitu cha kwanza ni usalama wako kwanza. Kwa hiyo hapo ulitaka askari apokonywe silaha na apigwe?
 
Aliwafuata kufanya nini hao wananchi?
 
Aliwafuata kufanya nini hao wananchi?
Kumbe habari ujaisoma vizuri. Askari walienda pale kwa ajili ya kuhakikisha amani inakuwepo. Fujo imetokea lazima askari waende kutuliza ghasia kwa sabb wapo pale kwa sabb hiyo.
Ajabu askari wapo pale, fujo bado inaendelea wangefanyeje sasa
 
Kwa hiyo solution ilikuwa ni kuua na wakati kuna washawasha hapo?
 
Angemiminia hata raia kumi risasi za kifuani ingekuwa poa sana, kuna muda ibadidi tujue kwamba hata polisi nao mi binadamu na wanaweza kuwa emotional pia.

Hata kama ni mimi siwezi kutuliwa nipigwe mawe na umati wa watu waliojitoa akili, tena nikiwa na Mrussia (AK-47).

Watu wavute bangi zao huko kisha waje kuleta stress zao kwenye kazi za watu? UA.
 
Kwa hiyo solution ilikuwa ni kuua na wakati kuna washawasha hapo?
Hata mimi ningeua, siwezi kushambuliwa na mawe kama mwizi ilhali nina AK-47 mkononi.

Kwahiyo ulitaka huyo askari avumilie hayo mawe? Kwamba aamke hapo akivumilia kupigwa mawe mpaka aifike hiyo washawasha???

Ni sawa tu hata hivyo alijitahidi sana, angeamua kuiweka kwenye automatic mode kisha aruhusu risasi mngewaokota wengi hapo.
 
Unauliza hivi na kupata sauti ya kuongea kwasababu tu hayajakukuta wewe, na Wala aliefariki hauhusiani nae.

Subiri siku polisi wafanye tukio litakalogusa familia au damu yako hapo ndipo utaelewa namna inayopaswa kutumika
Natumai ungesikia polisi aliuwawa kwa kupigwa mawe, ungefurahi sana.
 
Back
Top Bottom