Kigoma: Polisi Wadaiwa kuua raia kwa risasi na kujeruhi wawili kwenye kiwanja cha mpira Lake Tanganyika

Mpuuzi wewe angekuwa amepiga maza ako usingeongea huu utumbo wako
Mama gani huyo wa kwenda kuanzisha vurugu na kupiga askari mawe?

Kwenye hiyo mechi Askari waliwakosea nini mashabiki??

Kuna scenario yes siwezi kusupport unyama wa polisi, lakini kwa hili wakikuwa sawa tu. Huyo askari nae alitaka kuishi.
 
Ile bunduki anayopewa askari mnadhani ni urembo? Kuna majitu majinga eti polisi haruhusiwi kutumia risasi za Moto mnajazana ujinga mkawapige mawe muone.

Kuna mazingira ambayo tunapaswa kufahamu kwamba polisi nao ni binadamu aisee unampiga mawe ili uibe bunduki?

Polisi anailinda bunduki kushinda baba na mamake wazee Kama hamjapita mafunzo mkae kimya aisee.

Amefanya Safi kabisa na angetandika za kichwa iwe fundisho umeenda uwanjani kuangalia mpira au unapeleka bangi zako?
 
Pole sana kwa wafiwa. Lakini tuwekeni hoja zisizo na msingi pembeni, leo hii Afande subira angeuawa kwa kupigwa mawe na wananchi wanaojiita wenye hasira kali tena zitokanazo na mpira kisha waondoke na silaha ya kivita AK 47 unadhani kungekua na maoni gani juu ya uimara wa askari wetu?

Ni jambo jema amefanya katika kutekeleza majukumu yake na kulinda uhai wake, unauawa kwa kuleta vurugu tena za mpira ?? Na unaamrishwa kwa kupiga risasi za warnings! Lakini bado hawasikii tulitaka askari afanyeje? Iwe fundisho kwa wengine kuwaheshimu watu wanaotekeleza majukumu ya kuwalinda wao wenyewe, walidhani ni silaha yenye mpira ndani.

TUTII SHERIA PASIPO SHURUTI
 
Amesema mashabiki hao waliendelea kushambuliana na kuwapiga mawe askari waliokuwepo uwanjani hapo na kusababisha askari namba F.5123 D/ CPL Subira aliyekuwa na silaha aina ya AK 47 kushambuliwa sehemu ya kichwani na kuanguka chini” amesema kamanda Manyama

Tuambie namna ambayo angefanya hapa mkuu.

Tuchukulie niwewe umeangushwa chini na mawe yanamiminika na unasiraha ambayo inabidi uilinde kwa sababu kwenye huo umati sio wote ni wema mtu anaweza kupita nayo, pia ulinde uhai wako
Hii taarifa ni ngumu sana kuiamini police wamekua mabingwa wa kupika taarifa ambazo ni tofauti na kilichotokea.
 
Pole sana kwa wafiwa. Lakini tuwekeni hoja zisizo na msingi pembeni, leo hii Afande subira angeuawa kwa kupigwa mawe na wananchi wanaojiita wenye hasira kali tena zitokanazo na mpira kisha waondoke na silaha ya kivita AK 47 unadhani kungekua na maoni gani juu ya uimara wa askari wetu?

Ni jambo jema amefanya katika kutekeleza majukumu yake na kulinda uhai wake, unauwa kwa kuleta vurugu?? Tena unaamrishwa kwa kupiga risasi za warnings! Lakini bado hawasikii tulitaka askari afanyeje? Iwe fundisho kwa wengine kuwaheshimu watu wanaotekeleza majukumu ya kuwalinda wao wenyewe, walidhani ni silaha yenye mpira ndani.

TUTII SHERIA PASIPO SHURUTI
Umeongea vema kabisa, imagine walipewa onyo la matamshi, wakapewa onyo kwa kupigwa risasi Tisa hewani, lakini hao wavuta bangi walidhani Ile bunduki ni gitaa wamawekewa band au diamond anatumbuiza muha mwenzao.

That gun anayopewa askari hapewi Kama urembo na hii dharau kwa askari wanapofuata Sheria na taratibu za crowd control tunapaswa kuwa watiifu otherwise haya madhara hutokea maana risasi haichagui pa kupenya.

Tunapohimiza askari kufuata taratibu za kazi yao nasi tunapaswa kufuata maelekezo yao pale wanapotekeleza majukumu yao .

Watu zaidi ya 1000 mnapompiga mawe mtu mmoja mwenye bunduki mnakuwa mnatarajia afanye nini??? Huu no ujinga wa hali ya juu hatuwezi kutetea upuuzi wa namna hii.

Tukemee tabia ya kutofuata maelekezo au onyo kutoka kwa askari especially kwenye mazingira Kama haya inapotokea vurugu.
 
Huwezi toa maamuzi bora kwa kusikiliza upande mmoja Mkuu, but usijali ipo siku utaguswa na wewe ndio utajua hujui
 
Huu Ni ujinga hakuna polisi anae ruhusiwa kutumia silaha ya Moto Tena kwa mwananchi ambae Hana silaha, hata Kama hakutii sheria bado alikua na namna nyingine ya kufanya sio kuua.
Jiwe ni silaha hao raia walikuwa na mawe
 
Unauliza hivi na kupata sauti ya kuongea kwasababu tu hayajakukuta wewe, na Wala aliefariki hauhusiani nae.

Subiri siku polisi wafanye tukio litakalogusa familia au damu yako hapo ndipo utaelewa namna inayopaswa kutumika
Polisi ni watu hatari sn
 
Nguvu ya umma ndio upige watu risasi?. Polisi anaruhusiwa kutumia risasi pale tu retaliation ya raia ni sawasawa au madhara yake Ni sawa na risasi.
Hujaona hapo alijeruhiwa??police kakosea lakini raia wa kigoma mjifunze kuilinda amani...michezo ni furaha...kama mtu kasikia story hii tofauti na ilivyoletwa hapa,atupe version yake inasemaje ila kama ipo hivi,kama raia tuna ya kujifunza..
 
Kupitia Twitter pia, Abdul Nondo Kaandika;

View attachment 2151568

--
Askari polisi mwenye namba F.5123 D/ CPL Subira ambaye aliyekuwa na bunduki aina ya AK 47 adaiwa kumuua Juma Ramadhani kwa kumpiga risasi na kuwajeruhi watatu wakati akiwa kwenye harakati za kujihami kwenye vurugu zilizotokea katika kiwanja cha mpira cha Lake Tanganyika mkoani Kigoma.

Vurugu hizo zilitokea jana Jumatatu Machi 14, 2022 saa 10 jioni wakati wa fainali ya mchezo wa mpira wa miguu wa kumuenzi Dk Living Stone baina ya timu ya Mwandiga Fc dhidi ya Kipampa Fc ya Ujiji ulioandaliwa na Shirika la Joy in The Harvest kwa kushirikiana na Chama cha Mpira wa Miguu Kigoma (KFA) na mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Ester Mahawe.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 15, 2022 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, James Manyama amesema marehemu Juma amefariki dunia akiwa hospitalini akiendelea na matibabu.

Kamanda Manyama amesema vurugu hizo zilitokea kipindi cha kwanza wakati Mwandiga Fc iliyokuwa ikiongoza kwa goli moja liliposawazishwa na Kipampa Fc ambapo mashabiki wa Kipampa Fc kuvamia jukwaa la mashabiki wa timu ya Mwandiga na kuanza kuwazomea huku wakiwarushia chupa za maji na mawe hali iliyosababisha kuibuka kwa vurugu.

Amesema baada ya vurugu hizo kutokea askari waliokuwa wamepangwa kwa ajili ya kuimarisha ulinzi walijitahidi kudhibiti vurugu hizo lakini walizidiwa nguvu na kuomba msaada.

"Askari waliongezeka uwanjani pale kwa ajili ya kutuliza fujo na kutumia mabomu ya machozi na kishindo kuthibiti vurugu hizo lakini mashabiki hao waliendelea kufanya fujo.

“Amesema mashabiki hao waliendelea kushambuliana na kuwapiga mawe askari waliokuwepo uwanjani hapo na kusababisha askari namba F.5123 D/ CPL Subira aliyekuwa na silaha aina ya AK 47 kushambuliwa sehemu ya kichwani na kuanguka chini” amesema kamanda Manyama

Amesema askari huyo aliamua kujihami dhidi ya tishio la kunyang’anywa silaha pamoja na kutetea uhai wake kwa kufyatua risasi tisa hewani sambamba na kutoa onyo la kuwatawanya mashabiki waliokuwa wakimshambulia kwa mawe.

Amesema licha ya kupiga risasi hizo lakini mashabiki hao waliendelea kumshambulia kwa mawe akiwa ameanguka chini ndipo alipofyatua risasi tatu na moja ilimpata marehemu Juma ambaye alijeruhiwa katika paja la mguu wa kushoto na risasi ya pili ilimjeruhi Omary Amdan (35), katika unyayo wa mguu wake wa kushoto na risasi ya tatu ilimjeruhi Nasibu Moshi (35), katika mguu wake wa kushoto.

Amesema majeruhi wote walikimbizwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa Maweni kwa matibabu na vurugu zilipotulia mchezo huo wa fainali uliendelea hadi mwisho.

Amesema saa 12 jioni Juma Ramadhani akiwa anapatiwa matibabu alifariki dunia huku majeruhi wawili walipatiwa matibabu na kuruhusiwa kwenda nyumbani huku askari Subiri alibakia kwa ajili ya matibabu zaidi.

Amesema kutokana na tukio hilo jeshi la polisi linawashikilia watu wanne wanatuhumiwa kuwa chanzo cha vurugu hizo na upelelezi wa tukio hilo bado unaendelea na watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria zaidi.

" Niwasihi wananchi wa mkoa wa Kigoma wakati wa ushabiki wa michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu washabikie kwa ustaarabu, kuvumiliana na kufuata sheria za nchi na kuacha kushabikia kwa mihemko inayosababisha vurugu,"amesema Kamanda Manyama.

Chanzo: Mwananchi

Polisi alikuwa na AK 47 kwenye uwanja wa mpira? Kulikuwa na vita?​

28567FF6-A55B-4F58-8B75-55AC9221D5C0.jpeg
 
Huu Ni ujinga hakuna polisi anae ruhusiwa kutumia silaha ya Moto Tena kwa mwananchi ambae Hana silaha, hata Kama hakutii sheria bado alikua na namna nyingine ya kufanya sio kuua.
Sasa ulitaka wamwue huyo Polisi na kuchukua AK47? Raia na sisi tuache upimbi! Polisianaruhusiwa kujihami kwa risasi za moto akiona kuna hatari ya kunyang'anywa silaha au kuuawa! Vijana waache mihemuko watamalizwa kwa risasi za moto! Kama kweli walimshambulia kwa mawe niko upande wake!
 
Kupitia Twitter pia, Abdul Nondo Kaandika;

View attachment 2151568

--
Askari polisi mwenye namba F.5123 D/ CPL Subira ambaye aliyekuwa na bunduki aina ya AK 47 adaiwa kumuua Juma Ramadhani kwa kumpiga risasi na kuwajeruhi watatu wakati akiwa kwenye harakati za kujihami kwenye vurugu zilizotokea katika kiwanja cha mpira cha Lake Tanganyika mkoani Kigoma.

Vurugu hizo zilitokea jana Jumatatu Machi 14, 2022 saa 10 jioni wakati wa fainali ya mchezo wa mpira wa miguu wa kumuenzi Dk Living Stone baina ya timu ya Mwandiga Fc dhidi ya Kipampa Fc ya Ujiji ulioandaliwa na Shirika la Joy in The Harvest kwa kushirikiana na Chama cha Mpira wa Miguu Kigoma (KFA) na mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Ester Mahawe.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 15, 2022 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, James Manyama amesema marehemu Juma amefariki dunia akiwa hospitalini akiendelea na matibabu.

Kamanda Manyama amesema vurugu hizo zilitokea kipindi cha kwanza wakati Mwandiga Fc iliyokuwa ikiongoza kwa goli moja liliposawazishwa na Kipampa Fc ambapo mashabiki wa Kipampa Fc kuvamia jukwaa la mashabiki wa timu ya Mwandiga na kuanza kuwazomea huku wakiwarushia chupa za maji na mawe hali iliyosababisha kuibuka kwa vurugu.

Amesema baada ya vurugu hizo kutokea askari waliokuwa wamepangwa kwa ajili ya kuimarisha ulinzi walijitahidi kudhibiti vurugu hizo lakini walizidiwa nguvu na kuomba msaada.

"Askari waliongezeka uwanjani pale kwa ajili ya kutuliza fujo na kutumia mabomu ya machozi na kishindo kuthibiti vurugu hizo lakini mashabiki hao waliendelea kufanya fujo.

“Amesema mashabiki hao waliendelea kushambuliana na kuwapiga mawe askari waliokuwepo uwanjani hapo na kusababisha askari namba F.5123 D/ CPL Subira aliyekuwa na silaha aina ya AK 47 kushambuliwa sehemu ya kichwani na kuanguka chini” amesema kamanda Manyama

Amesema askari huyo aliamua kujihami dhidi ya tishio la kunyang’anywa silaha pamoja na kutetea uhai wake kwa kufyatua risasi tisa hewani sambamba na kutoa onyo la kuwatawanya mashabiki waliokuwa wakimshambulia kwa mawe.

Amesema licha ya kupiga risasi hizo lakini mashabiki hao waliendelea kumshambulia kwa mawe akiwa ameanguka chini ndipo alipofyatua risasi tatu na moja ilimpata marehemu Juma ambaye alijeruhiwa katika paja la mguu wa kushoto na risasi ya pili ilimjeruhi Omary Amdan (35), katika unyayo wa mguu wake wa kushoto na risasi ya tatu ilimjeruhi Nasibu Moshi (35), katika mguu wake wa kushoto.

Amesema majeruhi wote walikimbizwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa Maweni kwa matibabu na vurugu zilipotulia mchezo huo wa fainali uliendelea hadi mwisho.

Amesema saa 12 jioni Juma Ramadhani akiwa anapatiwa matibabu alifariki dunia huku majeruhi wawili walipatiwa matibabu na kuruhusiwa kwenda nyumbani huku askari Subiri alibakia kwa ajili ya matibabu zaidi.

Amesema kutokana na tukio hilo jeshi la polisi linawashikilia watu wanne wanatuhumiwa kuwa chanzo cha vurugu hizo na upelelezi wa tukio hilo bado unaendelea na watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria zaidi.

" Niwasihi wananchi wa mkoa wa Kigoma wakati wa ushabiki wa michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu washabikie kwa ustaarabu, kuvumiliana na kufuata sheria za nchi na kuacha kushabikia kwa mihemko inayosababisha vurugu,"amesema Kamanda Manyama.

Chanzo: Mwananchi
Ilivyoandikwa ni tofauti na ilivyokuwa, anyway acha maisha yaendelee.
 
Back
Top Bottom