Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma linafanya uchunguzi wa tukio la fujo zilizopelekea majeruhi ya watu watatu, ni kwamba Mei 5, 2026 muda wa saa 12.00 mchana huko katika Kijiji cha Kililani, Kata ya Buhingu, Wilaya ya Uvinza, Mkoa wa Kigoma, Jeshi la Polisi, Idara ya ardhi na hifadhi ya Taifa ya Mahale wakiwa kwenye zoezi la utoaji elimu kwa Wananchi wa Kijiji cha Kililani kuhamasisha Wananchi hao kuhama ili kupisha eneo la Hifadhi ya Taifa ya Mahale, lilijitokeza kundi la watu likizuia zoezi hilo la uelimishaji na kujichukulia sheria mkononi kwa kufunga Barabara na kuwashambulia kwa silaha za jadi na Mawe.
Katika vurugu hizo watu watatu wamejeruhiwa, wawili kati yao wanaendelea kupatiwa matibabu katika kituo cha afya Buhingu. Uchunguzi utakapokamilika hatua stahiki zitachukuliwa dhidi ya wahusika.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma linatoa wito kwa baadhi ya Wananchi wa Mkoa wa Kigoma kuendelea kutii sheria bila shuruti na kutojihusisha na vitendo vya kujichukulia sheria mkononi.
Pia soma:
~ Askari wamewajeruhi vijana watatu kwa risasi – Uvinza wakati wa msafara wa DC, Mei 5, 2026, hatua zichukuliwe
~ UVINZA: Vijana watatu kujeruhiwa kwa risasi, DC asema waliwavamia Askari wakitaka kuwanyang’anya bunduki