Kigoma: Wamuua binti kwa kipigo wakimlazimisha kuolewa ili wapate ng'ombe

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
JESHI la Polisi Mkoani Kigoma linawashikilia watu watatu akiwemo baba mzazi Kulwa Juakali (40) Mkazi wa kijijicha Lufubu wilayani Uvinza kwa tuhuma za kumpiga fimbo mtoto wake Mbaru Juakali (17) hadi kusababisha kifo huku chanzo cha tukio hilo kikidaiwa kuwa ni kumlazimisha mtoto huyo kuolewa chini ya umri kwa mahari ya ng'ombe 13 bila ridhaa yake.

"Binti alipigwa sehemu mbalimbali za mwili wake akilazimishwa kuolewa ambapo kulikua na ahadi ya kulipwa mahari ya ng'ombe 13 na waliokua wakishinikiza aolewe ni wazazi na hao ndio walikua na uroho wa kupokea mahari ya hao ng'ombe 13, taarifa zilizopo binti huyu alikua anachumbiwa na Wanaume watatu kwahiyo yule ambae ofa yake ilikuwa kubwa kwa ng'ombe 13 huyo ndio alikua analazimishwa aolewe nae wakati binti hakuridhia na kupelekea kipigo" amesema Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma James Manyama.

Polisi Kigoma wanasema upelelezi wa tukio hilo bado unaendelea na watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria akiwemo baba mzazi Kulwa Juakali (40), Baba mkubwa wa marehemu Shija Juakali (44) na Baba mdogo wa marehemu aitwaye Majiba Juakali (29) wote wakazi wa Kijiji cha Lufubu wilayani Uvinza mkoani Kigoma.

Nipashe
 
Kwa majina haya ni wasukuma 100%. Maisha yamebadilika sana. Sasa hivi huwezi kumchagulia mtoto mchumba.
Km ulishindwa kupata mali kwa kufanya kazi basi usitegemee kuwafanya watoto wako kitega uchumi.
Hao ni kifungo cha maisha au kunyongwa.
 
Tanzania bado iko gizani sana.

Ukiwa mjini unaona kama nchi imepiga hatua kwenye mambo fulani lakini ukweli ni kwamba bado Sana

Hebu fikiria Kama tusingetawaliwa tukaambukizwa effects Fulani mataifa ya Africa yangekuwaje,
 
JESHI la Polisi Mkoani Kigoma linawashikilia watu watatu akiwemo baba mzazi Kulwa Juakali (40) Mkazi wa kijijicha Lufubu wilayani Uvinza kwa tuhuma za kumpiga fimbo mtoto wake Mbaru Juakali (17) hadi kusababisha kifo huku chanzo cha tukio hilo kikidaiwa kuwa ni kumlazimisha mtoto huyo kuolewa chini ya umri kwa mahari ya ng'ombe 13 bila ridhaa yake.

"Binti alipigwa sehemu mbalimbali za mwili wake akilazimishwa kuolewa ambapo kulikua na ahadi ya kulipwa mahari ya ng'ombe 13 na waliokua wakishinikiza aolewe ni wazazi na hao ndio walikua na uroho wa kupokea mahari ya hao ng'ombe 13, taarifa zilizopo binti huyu alikua anachumbiwa na Wanaume watatu kwahiyo yule ambae ofa yake ilikuwa kubwa kwa ng'ombe 13 huyo ndio alikua analazimishwa aolewe nae wakati binti hakuridhia na kupelekea kipigo" amesema Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma James Manyama.

Polisi Kigoma wanasema upelelezi wa tukio hilo bado unaendelea na watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria akiwemo baba mzazi Kulwa Juakali (40), Baba mkubwa wa marehemu Shija Juakali (44) na Baba mdogo wa marehemu aitwaye Majiba Juakali (29) wote wakazi wa Kijiji cha Lufubu wilayani Uvinza mkoani Kigoma.

Nipashe
😡 😡
 
Kuna uajabu kwani?
Ajabu ndo haya yaliyowakuta.. Miaka 23 ilitakiwa awe darasani bado hivyo hatutegemei angekua na mtoto.. na hata kama angekua na mtoto bado asingeweza kumpiga mtoto kisa apate ng'ombe maana angekua kaelimika..

So alipata mtoto at wrong time ndio maana kafikia alipofikia.
 
Back
Top Bottom