Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Zaidi ya watu 200 wakazi wa kijiji cha Kagunga, Halmashauri ya wilaya ya Kigoma, mkoani Kigoma wako mafichoni/ porini huku usalama wao ukiwa shakani kutokana na kile kinachodaiwa uwepo wa oparesheni 'isiyo salama' inayoendeshwa na Jeshi la Polisi dhidi yao kijijini hapo
Akizungumza na Jambo TV mapema leo, Ijumaa Novemba 29.2024 aliyekuwa mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa kijiji hicho kupitia ACT Wazalendo Hassan Mikidadi Yasin ambaye ni mmoja wa watu walioko mafichoni amesema chanzo cha kutokea kwa hayo yote ni matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa ambapo kwa madai yake ni kwamba yeye alimshinda kwa tofauti ya kura nane aliyekuwa mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM) lakini baadaye walibaini uwepo wa njama za kubadilisha matokeo hayo
Inaelezwa kuwa zoezi la upigaji wa kura kwenye kijiji hicho lilienda mpaka majira ya saa 4 usiku na hiyo ikitokana na ukweli kwamba kijiji hicho kina idadi kubwa ya watu lakini vituo vya kupigia kura vilivyowekwa ni vichache, hata hivyo zoezi la upigaji kura lilipomalizika uhesabuji wa kura ulianza na kukamilika majira ya saa 9 usiku
Wananchi walisubiri matokeo kwa muda mrefu lakini baadaye wengi wao walitawanyika usiku huo, lakini siku iliyofuata yaani Novemba 28.2024 asubuhi walifika eneo la majumuisho kwa ajili ya kupata matokeo lakini subira yao ilienda hadi majira ya saa 8 pasipo matokeo hayo kutangazwa
"Wasimamizi wa uchaguzi waliniambia mimi na mawakala wangu tuingie ndani lakini mawakala wa CCM wao hawakuitwa, tulipoingia taarifa ikaonyesha kwamba wanataka kwenda kutangaza matokeo huku wakisema majumuisho wameshamaliza, nikahoji unasemaje majumuisho umemaliza wakati mimi mgombea sina fomu yoyote inayoonesha nimepata kura ngapi, hapo wakati nina kura kura kutoka kwa mawakala wangu ambao pia wamenyimwa fomu ya matokeo ya kila kituo, tulipoangalia ikaonekana tumetofautiana kidogo, mimi nimepata 1007 na mgombea wa CCM amepata kura 999" -Yasin
Anasema baada ya kugundua njama za kubadilishwa kwa matokeo hayo aligomea na kusabisha mabishano ambayo baadaye maafisa wa Polisi wakilazimika kuingia ndani, huku nje wananchi wakishinikiza kudai matokeo yao.