Kigugumizi cha nini kwenye Uraia Pacha? Shuhudia unavyowakwamisha Watanzania kuwekeza nyumbani. Miradi, mijengo ya maana ingeota kama uyoga


Tangu uame kuacha kumsapoti Mkuu wa nchi baada ya kumwagika kama chawa hasiye na mifupa

Ndio Nilijua wewe mtu wa namba gani, una wivu sanaaa

Haswa baada ya chawa ulojaribu, I guess na nje ya humu kupigwa chini

Pole, acha wivu mambo yasonge.

Niffer oyeee
 
Hahaha nchi hii ya ajabu sana, msukuma akitoka Mwanza akaja Dar es Salaam kutafuta maisha ni sawa, lakini Mkurya akienda kutafuta maisha Kenya, ni kibaraka tayari.

Kwanini kila mtu asibaki alikozaliwa, au walipizaliwa wazazi wake, kama kuhama kuhemea ni ukibaraka?

Na vibaraka ni walioko ulaya na marekani tu, vipi walioko South Afrika au UAE?

Mbona tuna Wapemba na Waunguja kibao hapa Tanganyika, na wao wanaishi kwetu wananunua ardhi na kuwekeza kwa uhuru, lakini Watanganyika haturuhusiwi kule Zanzibar?

Zanzibar wana vitambulisho vyao vya ukaazi, Mtanganyika huruhusiwi, hiyo siyo URAIA pacha?

Nchi moja lakini kila upande unakitambulisho chake cha uraia, Wazanzibari wana haki kuishi Tanganyika, lakini Mtanganyika hana haki kuishi Zanzibar.

Sasa hawa wa Zanzibari wanapopata haki huku Tanganyika na kwao wana uraia wa Zanzibar huo siyo Uraia PACHA ni nini?
 
Umeandika nini wewe? Au ndo ile wanaita kunena kwa lugha?
 
Mimi ni miongozni mwa watu wanaounga mkono uraia pacha lakini huwa nasikitika sana mnapounganisha suala la uwekezaji na uraia pacha. Hamuoni kuwa mnafanya makosa ku-support msemo usemao kuwa ''utu kwa mali''? Yaani ni kama wazazi kumthamini mtoto kwa sababu tu ana uwezo. Mimi nadhani tungejenga hoja kuwa wao wana uraia wa damu ambao hauwezi kufutika. Kama uraia unaangaliwa kwa kigezo cha ''uwekezaji'' basi vijana wote waliopo Bongo ambao hawana kazi wala hawawezi kuwekeza uraia wao ufutwe.
 
Uraia pacha sio suluhisho kwa matatizo yetu makubwa hasa umasikini. Kenya ndiyo inchi ya kwanza Afrika kwa kuwa na Hohehahe kibao pale Kibera na Mathare. Tunahitaji viongoz wenye maona na uthubutu kusimamia Kodi na rasilimali.
Wewe hujaelewa mada hata kidogo. Wamesema hivi: watu wote waliozaliwa Tanzania na wazazi wa kitanzania; kuwanyang'anya uraia wao ni kuvunja haki za binadamu. Hayo mambo ya uwekezaji au umaskini hayana connection yoyote na uraia pacha. Yaani ukalishe ''migololi'' yako kuanzia asubuhi mpaka jioni na usifanye kazi halafu raia pacha aje awe suluhisho la uvivu wako?
 
Kuna baadhi ya Kodi hupungua ikiwa anayewekeza ni Raia Kwa Kuzaliwa na ambaye sio raia.

Kwahiyo Kwa kuruhusu Uraia pacha, nilidhani ingekuwa catalyst ya Kuwavutia zaidi wawekezaji wazawa ambao ndiyo wangenufaika na huo Uraia pacha
 
Wasiwasi wao Mkubwa ni hofu ya ugaidi pamoja na kukosekana Kwa uzalendo.

Hivyo vitu nimewahi kumsikia Mkubwa fulani akiviongea, wakati Kwa mara ya kwanza hoja ya Uraia pacha ikipigiwa chapuo miaka ile
Hizi ndiyo hoja ''mfu'' kuliko hoja zote nilizowahi kusikia kuhusu uraia pacha. Hawa viongozi wa Tanzania wasio na uzalendo, wanaoiba na kufanya ufisadi wa kukufuru ni raia wa nje? Au hajui maana ya neno uzalendo? Inapotoka ripoti ya mkaguzi mkuu hayo mafedha yote yanaibwa na diaspora? Kuhusu ugaidi, kina Makonda na Mafwele ni raia wa nje? Nchi zenye uraia pacha mbona hatuoni zikisumbuliwa na ugaidi kuliko nchi nyingine?
 
Ukisikia hoja zao wapinga Uraia pacha ni pamoja na hiyo

Yaani mtu anajificha kwenye hicho kigezo cha uzalendo wakati Wezi wa Mali za Umma ni hao hao Viongozi
 
Serikali ikiruhusu uraia pacha, wewe wewe tena utakuja kuisifia.

Chawa hamna maana kabisa nyie.
 
Serikali ikiruhusu uraia pacha, wewe wewe tena utakuja kuisifia.

Chawa hamna maana kabisa nyie.
hatuwezi kuruhusu vibara waje waharibu nchi yetu hata suku moja gentleman...

wakawekeze na kujenga hiyo mijengo ya maana kama uyoga hata hapo nchi jirani tu, tutawasapoti lakini si vinginevyo
 
Kama ni wazalendo wa kweli wakane uraia wa Nchi zingine wabaki na uraia wa Tanzania
 
hatuwezi kuruhusu vibara waje waharibu nchi yetu hata suku moja gentleman...

wakawekeze na kujenga hiyo mijengo ya maana kama uyoga hata hapo nchi jirani tu, tutawasapoti lakini si vinginevyo
Hoja zenu sio za kutiwa maanani.
Kesho raisi akisema wapo kwenye mchakato unabadili gia angani kua anaupiga mwingi na kuanza kuokoteza faida za uraia pacha.
 
Tatizo lako ni moja hueleweki .

Tangu nimesikia umekuja hata wale watu ninaowafahamu nimewatahadharisha wasikupe engagement ya aina yoyote maana leo uko moto kesho baridi.

Sote tunajua sababu kubwa ya CCM kuukata uraia pacha miaka imepita watu walikuwa wanasita ila kwa kizazi hiki mtu akishashika karatasi zikakaa vizuri offer ya kazi ya kueleweka imekuja anapiga chini uraia huo.

Endeleeni kuamini kuwa mzalendo ni kuwa mtanzania tu ila mkae mkijua uzalendo uko moyoni na sio utaifa.

Njia pekee ya kuanza upya ni mpaka kama yale yaliyotokea Kenya 2007/08 ndio unaona hadi leo wamefika hapo asije kukudanganya mtu bila PEV Kenya wangepata katiba mpya 2010 never.

Katiba yao ni ilikuwa worse kuliko hata hii yetu maana rais alikuwa ni mbunge pia katika kipindi chake chote cha utawala yani rais ana kofia mbili bado mamlaka yasiyo na mipaka

Kupitia katiba ile ndio maana marais Jomo Kenyatta, Daniel Moi na Emilio Mwai Kibaki walikuwa ni marais na Wabunge katika vipindi vyao vyote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…