Kigugumizi cha nini kwenye Uraia Pacha? Shuhudia unavyowakwamisha Watanzania kuwekeza nyumbani. Miradi, mijengo ya maana ingeota kama uyoga

Kigugumizi cha nini kwenye Uraia Pacha? Shuhudia unavyowakwamisha Watanzania kuwekeza nyumbani. Miradi, mijengo ya maana ingeota kama uyoga

Hoja zenu sio za kutiwa maanani.
Kesho raisi akisema wapo kwenye mchakato unabadili gia angani kua anaupiga mwingi na kuanza kuokoteza faida za uraia pacha.
hoja hapo iko wazi tu, na ni very clear,
maslahi ya waTanzania wote lazima ndiyo kiwe kipaumbele cha Taifa...

hayo mengine ya mtu moja moja sijui kwasababu tu anaishi wapi, yatawekewa, utararatibu ili huyo mtu binafsi akiona unafaa aufwate kujenga hayo majumba yake kama uyoga, na akiona haufai basi akaushe tu na utaratibu wake, ilimradi tu waTanzania wote wako salama wanaenyo amani na utulivu :pulpTRAVOLTA:
 
Bahati mbaya sana sikaririshwi na binadamu yeyote nipo huru sana! Haya mambo ya vibaraka wa Ulaya na Marekani nimenza kuysikia nikiwa chipukizi wa ccm miaka ya mwisho ya 70 na 80, bado yapo kumbe! Vibaraka wa Uarabuni kama Oman, UAE, Saudia, nk hawapo? Mbn wabongo ni vibaraka tu wa levels zote na wapo tu hapo ndani? Hiyo amani unayoongelea itaharibiwa na Duality ni ipi? Una justification yoyote au ni yaleyale ya kuombea matajiri waishi kama shetani?
Mkuu una muda wa kujibishana na takataka hiyo ya CCM.

Huyo nilipekeka ignore list muda with that kind of thinking ndio maana Tanzania iko nyuma from the word go!

Niliambiwa eti huyo ni mbunge na waziri , very mediocre.
 
Wasiwasi wao Mkubwa ni hofu ya ugaidi pamoja na kukosekana Kwa uzalendo.
Tanzania balozi ya US ilishambuliwa 1998 je kulikuwa na uraia pacha mkuu?

Ugaidi it is too subjective, ugaidi unafanyika popote hivyo kila nchi inapaswa ijilinde na ugaidi kwa kuwa mipaka ya nchi watu wanaingia na kutoka.
Hivyo vitu nimewahi kumsikia Mkubwa fulani akiviongea, wakati Kwa mara ya kwanza hoja ya Uraia pacha ikipigiwa chapuo miaka ile
Huyo alikuwa anaongea kufifisha hoja hiyo.

Ndio maana mtu ulikuwa ukiingia kusoma majuu miaka hiyo wanakupangia vyuo vya maeneo fulani tu huko unakuta kuna watu wao walishawaattach hivyo wanakufuatilia nyendo zako zote uwapo masomoni na baada ya masomo unafanya nini maana waliamini ukiingia nje ya mipaka ya Tanzania utafunzwa usaliti sasa kama ni hivyo si wangewaacha watu wasome huko huko Tanzania?
 
Ushauri wako ni Mzuri lakini ninacho shangaa Serikali Ya Tanzania kwa nini inaogopa Huo Uraia Pacha? Ungekuwa Uraia Pacha una madhara jirani zetu Wa-Kenya wasingekubali kuruhusu huo Uraia Pacha Bado sisi Wa-Tanzania tuko nyuma kila kitu ingelifaa tuige wenzetu majirani zetu Wa-Kenya walioruhusu Uraia Pacha.
Una madhara ambayo hayaonekani
 
diaspora gani wanaojitambua? nadhani kama tunasolve issue ya uraia tuongee ukweli na tuwathamini tu kwa sababu ni watoto wetu na hakuna madhara wakiwa na uraia pacha, ila ni diaspora gani anajitambua, tutajie hata mmoja tu. mange? is that the real picture?

Tanzania ina over protectionism isiyo na umuhimiu wowote na hii inatokana na sera za nyerere za ujamaa, nenda hata urusi au china uone kama kuna uraia pacha, wanaogopa kuliko chochote, sababu yao kuu ati mtu hatakuwa royal kwa serikali yake, wengine wanafikiri mtu akiwa na allegiance kwa nchi mbili atatoa siri za nchi. siri zipi sasa kama Tanzania au Africa hii ambayo Marekani akitaka kukujua hahitaji mtu wa ndani, atatumia mitandao tu anakufahamu hadi chooni kwako? ni kitu gani tunacholinda hasa hadi tuwakatae watoto wetu kaka zetu na dada zetu walioenda kutafuta maisha nje? tujifunze basi, nchi zenye uraia pacha zimepata madhara gani? mfano Kenya, Rwanda, Nigeria, Ghana, South Africa, Congo DR etc wamepata madhara gani? ati watu watakuja kuchukua ardhi, kwani wakichukua wakaiendeleza pakawa pazuri utaathirika nini? wanaondoka na ardhi? Dubai mbona kuna kila mtu na maendeleo yanaonekana ni ya wadubai? kwani mtu akija na pesa yake akaspend hapa si ameongeza mzunguko, uchumi na ajira? akili za wanaopinga uraia pacha ni finyu sana.
Hatutaki bakini huko huko tu au njooni mtuchukue
 
Ushauri wako ni Mzuri lakini ninacho shangaa Serikali Ya Tanzania kwa nini inaogopa Huo Uraia Pacha? Ungekuwa Uraia Pacha una madhara jirani zetu Wa-Kenya wasingekubali kuruhusu huo Uraia Pacha Bado sisi Wa-Tanzania tuko nyuma kila kitu ingelifaa tuige wenzetu majirani zetu Wa-Kenya walioruhusu
Ushauri wako ni Mzuri lakini ninacho shangaa Serikali Ya Tanzania kwa nini inaogopa Huo Uraia Pacha? Ungekuwa Uraia Pacha una madhara jirani zetu Wa-Kenya wasingekubali kuruhusu huo Uraia Pacha Bado sisi Wa-Tanzania tuko nyuma kila kitu ingelifaa tuige wenzetu majirani zetu Wa-Kenya walioruhusu Uraia Pacha.
Nchi nyingi duniani ziko kwenye mfumo wa uraia pacha, nina jamaa ambao wana citizenship ya nchi zaidi ya mbili. Tatizo lililopo utawala wa Bongo una uoga kwa kuwa wamezoea kuburuza raia, imagine unafanya mambo yako freely then watume vibwengo wao(wasiojulikana) ili wakuteke whilst una uraia pia wa USA au wa UK huo moto watakaowashiwa na embassy husika watajuta na huo ni mfano kiduchu tu kwani yako mengi. Halikadhalika watu ambao hawajatembea hata kama ni wasomi huwa in a way ni bongolala kwa kule tu kukosa exposure hivyo wanatawalika kirahisi yaani ni kama kuku mwenye mdondo sasa hawa ambao ni full exposure hawatakiwi wajazane kwani wengi wao wanajitambua vilivyo hivyo kuwapeleka mzobemzobe si kitu rahisi.
 
Ushauri wako ni Mzuri lakini ninacho shangaa Serikali Ya Tanzania kwa nini inaogopa Huo Uraia Pacha? Ungekuwa Uraia Pacha una madhara jirani zetu Wa-Kenya wasingekubali kuruhusu huo Uraia Pacha Bado sisi Wa-Tanzania tuko nyuma kila kitu ingelifaa tuige wenzetu majirani zetu Wa-Kenya walioruhusu Uraia Pacha.
Hatuko nyuma Mkuu.
Walionyuma ni viongozi wanaokataa uraia pacha.
Viongozi wetu wanaangalia upande mmoja wa shilingi.
Wao wanaangalia upande wa mwenge tu, kuigeza upande wa pili hawataki.
 
Kwa akili hizi tungetegemea nini mkuu? Tubaki kusugua goti maana tushafanya ndio solution ya kila kitu
Mkuu mimi vijana waliokuwa wakisubiria miujiza ya uraia pacha wakati karatasi zimekaa sawa na kuna kazi zinakuja zinahitaji kubadili uraia mimi nilikuwa mstari wa mbele kuwaambia waache kusubiri akili chakavu za CCM ziwaamulie uzalendo na utaifa upo moyoni sio hizo propaganda mfu za miaka nenda rudi.

Wanaotajwa na CAG wamekwapua pesa si ni raia na wanavaa mabendera shingoni na wanapewa ulinzi na bado wanaiba mabilioni kila siku na hawafanywi kitu.

Imagine mtu anasema ukiwa na uraia pacha wewe ni kibaraka sababu za kuitwa kibaraka hana hata moja yenye mashiko.
 
Back
Top Bottom