diaspora gani wanaojitambua? nadhani kama tunasolve issue ya uraia tuongee ukweli na tuwathamini tu kwa sababu ni watoto wetu na hakuna madhara wakiwa na uraia pacha, ila ni diaspora gani anajitambua, tutajie hata mmoja tu. mange? is that the real picture?
Tanzania ina over protectionism isiyo na umuhimiu wowote na hii inatokana na sera za nyerere za ujamaa, nenda hata urusi au china uone kama kuna uraia pacha, wanaogopa kuliko chochote, sababu yao kuu ati mtu hatakuwa royal kwa serikali yake, wengine wanafikiri mtu akiwa na allegiance kwa nchi mbili atatoa siri za nchi. siri zipi sasa kama Tanzania au Africa hii ambayo Marekani akitaka kukujua hahitaji mtu wa ndani, atatumia mitandao tu anakufahamu hadi chooni kwako? ni kitu gani tunacholinda hasa hadi tuwakatae watoto wetu kaka zetu na dada zetu walioenda kutafuta maisha nje? tujifunze basi, nchi zenye uraia pacha zimepata madhara gani? mfano Kenya, Rwanda, Nigeria, Ghana, South Africa, Congo DR etc wamepata madhara gani? ati watu watakuja kuchukua ardhi, kwani wakichukua wakaiendeleza pakawa pazuri utaathirika nini? wanaondoka na ardhi? Dubai mbona kuna kila mtu na maendeleo yanaonekana ni ya wadubai? kwani mtu akija na pesa yake akaspend hapa si ameongeza mzunguko, uchumi na ajira? akili za wanaopinga uraia pacha ni finyu sana.