Kigugumizi cha nini kwenye Uraia Pacha? Shuhudia unavyowakwamisha Watanzania kuwekeza nyumbani. Miradi, mijengo ya maana ingeota kama uyoga

Hakuna mtu anang'ang'ania kuwekeza TZ ila serikali yenu ndo inaomba diaspora wawekeze TZ. Jielimishe.
 
Halafu inapunguza uzalendo, watawala watafisadi umma na kukimbilia kwingine. Kuna wageni watakuja TZ kwa mwanya huo huo na kuifanya nchi iwe shamba la bibi.

Hao wanaofisadi kila mwaka kulingana na report ya CAG wamekimbilia wapi? Akili chakavu hizi, fisadi anakufisadi na anaweza kuwa chumbani kwako, hahitaji uraia pacha! Lini Tz iliacha kuwa shamba la bibi yako? Ufisadi upo left and right na hakuna mwenye uraia pacha anayekukamua hadi umekua na chuki ya namna hii. Kua
 
Kama inasaidia watawala kwanini wanaipinga?
 
Halafu inapunguza uzalendo, watawala watafisadi umma na kukimbilia kwingine. Kuna wageni watakuja TZ kwa mwanya huo huo na kuifanya nchi iwe shamba la bibi.

Kwani sahizi hamna upigaji? Hao mafisadi wana dual citizenship rn?

Kama wageni watakuja kuwanyonya nyie mnashindwa nini kwenda kuwanyonya wao si wote mtakua na dual citizenship?

Tatizo la wabongo ni ujinga na inferiority complex. Kwa jinsi mnavyoziogopa Kenya na Rwanda hamuwezi shindana on the global stage mna inferiority complex kupita maelezo na elimu zenu za kata hazijawasaidia kitu.
 
Umesema sahihi Mkuu, hizo ni miongoni mwa sababu mfu kabisa za kuzuia Uraia pacha

Ndiyo maana huwa nasema, Viongozi wetu hawapo kutunguongoza ili tupige hatua za kimaendeleo, isipokuwa Kwa ajili ya maslahi yao binafsi
 
Itakuwa hawaja ngamua vizuri mambo.

Kama hilo tu linawashinda wataweza vp kung'amua swala la uraia pacha kwa mapana yake?

Tatizo kubwa TZ ni ujinga kuanzia viongozi wa juu hadi watu wa mitaani. Ujinga na inferiority complex inawasumbua sana wabongo hawajiamini kabisa wanajiona wao ni wanyonge, ni watu wa kuibiwa tu na kunyanyswa kama wakiambiwa washindane na wenzao wa kimataifa.
 
Ndio ukweli mchungu
 
Umesema sahihi Mkuu, hizo ni miongoni mwa sababu mfu kabisa za kuzuia Uraia pacha

Ndiyo maana huwa nasema, Viongozi wetu hawapo kutunguongoza ili tupige hatua za kimaendeleo, isipokuwa Kwa ajili ya maslahi yao binafsi
Taratibu tu mkuu kuna kizazi kitawaamsha hiki chetu naona kama ni wachache tuliamka usingizini kutoka zidumu fikra za mwenyekiti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…