Kigugumizi cha nini kwenye Uraia Pacha? Shuhudia unavyowakwamisha Watanzania kuwekeza nyumbani. Miradi, mijengo ya maana ingeota kama uyoga

Kigugumizi cha nini kwenye Uraia Pacha? Shuhudia unavyowakwamisha Watanzania kuwekeza nyumbani. Miradi, mijengo ya maana ingeota kama uyoga

Faida ni nyingi kuruhusu Uraia Pacha

Kuna raia wengi Marekani na Ulaya ambao Wana asili ya Tanzania, ambao wangetamani kurudi na kuwekeza nyumbani Tanzania

Hata baadhi ya wana michezo, wengi wangeweza kurudi nyumbani na kuchezea timu yetu ya Taifa

Hilo lingefanyika, huenda nasi baada ya miaka 60 ya Uhuru Tanzania ingeshiriki michuano ya Kombe la Dunia.

Najua hatujachelewa, Viongozi wanaweza kuruhusu hili likafanyika
Tatzo mboga mboga wanaogopa eti wata ingiza mamluki wa kuwatoa ikulu. Mboga mboga wanawaza madaraka tu
 
Bahati mbaya sana sikaririshwi na binadamu yeyote nipo huru sana! Haya mambo ya vibaraka wa Ulaya na Marekani nimenza kuysikia nikiwa chipukizi wa ccm miaka ya mwisho ya 70 na 80, bado yapo kumbe! Vibaraka wa Uarabuni kama Oman, UAE, Saudia, nk hawapo? Mbn wabongo ni vibaraka tu wa levels zote na wapo tu hapo ndani? Hiyo amani unayoongelea itaharibiwa na Duality ni ipi? Una justification yoyote au ni yaleyale ya kuombea matajiri waishi kama shetani?
unakasirika na nini sasa gentleman kwa kuambiwa ukweli?🤣

sasa gentleman,
ungejikita kwenye mada mahususi zaidi, sio kung'ang'ana na kufafanua maoni na mtazamo wangu juu ya hoja muhimu sana ya mtoa hoja, ambae ni muandishi nguli wa habari nchini, mwalimu mwandamizi wa sheria anaheshimika sana kwenye taasisi za elimu ya juu mbalimbali humu nchini na kada huru wa CCM.

nini maoni yako kadiri ya mtoa hoja urais pacha ni fursa ama sio fursa?

Mungu Ibariki Tanzania 🐒
 
Ukizaliwa tu Tz hata ukibadilisha uraia bado unaweza kuwekeza kirahisi tu tofauti na wageni
 
Tatzo mboga mboga wanaogopa eti wata ingiza mamluki wa kuwatoa ikulu. Mboga mboga wanawaza madaraka tu
Ikiwa wakubwa wanashindwa kuridhia Uraia pacha Kwa hofu ya kung'olewa madarakani basi hawana nia ya dhati katika mapambano ya kumaliza Umasikini wetu.

Uraia pacha ni nyenzo muhimu Kwa Nchi kupiga hatua za maendeleo
 
Ikiwa wakubwa wanashindwa kuridhia Uraia pacha Kwa hofu ya kung'olewa madarakani basi hawana nia ya dhati katika mapambano ya kumaliza Umasikini wetu.

Uraia pacha ni nyenzo muhimu Kwa Nchi kupiga hatua za maendeleo
Umaskn wetu ndugu mtanzania hawaujui wao wanaangalia matumbo yao tu. Leo toka uwapinge uone kama hawata kupoteza
 
Na hasara ni zipi?

-Kaveli-
Wasiwasi wao Mkubwa ni hofu ya ugaidi pamoja na kukosekana Kwa uzalendo.

Hivyo vitu nimewahi kumsikia Mkubwa fulani akiviongea, wakati Kwa mara ya kwanza hoja ya Uraia pacha ikipigiwa chapuo miaka ile
 
Ushauri wako ni Mzuri lakini ninacho shangaa Serikali Ya Tanzania kwa nini inaogopa Huo Uraia Pacha? Ungekuwa Uraia Pacha una madhara jirani zetu Wa-Kenya wasingekubali kuruhusu huo Uraia Pacha Bado sisi Wa-Tanzania tuko nyuma kila kitu ingelifaa tuige wenzetu majirani zetu Wa-Kenya walioruhusu Uraia Pacha.
Uraia pacha sio suluhisho kwa matatizo yetu makubwa hasa umasikini. Kenya ndiyo inchi ya kwanza Afrika kwa kuwa na Hohehahe kibao pale Kibera na Mathare. Tunahitaji viongoz wenye maona na uthubutu kusimamia Kodi na rasilimali.
 
Back
Top Bottom