Tetesi: Kigwangalla kuwa Waziri mpya wa Afya, Dr. Gwajima kwenda Jinsia, Wanawake, Wazee na Watoto!

Tetesi: Kigwangalla kuwa Waziri mpya wa Afya, Dr. Gwajima kwenda Jinsia, Wanawake, Wazee na Watoto!

Naona apewe Dokta Msukuma na yeye si dokta ? atawasaidia madokta wenzake kwenye masuala ya afya🐒
 
Anayo haki ya kuteuliwa arekebishe mihemko, staha ya ulimi na kuishi uongozi kwa unyenyekevu, he misses maturity kwenye ulimi, he seems too much of his own like am the one with brain who knows better na kubehave kama Mwanamke kwenye social media platforms, he should learn to endure provocations. Kila la kheri kwake uonevu na ubabe si kheri.
 
Wampe Ndugulile kama atabadilisha, japo Gwajima anafanya vizuri sana kwenye hiyo wizara
 
Watanzania ni aina ya watu ambao unakuta wanataka kuvuka pori lenye Simba. Kwenye kuchagua nani awavushe kati ya Masai aliekuwa akiswaga n’gombe kwenye hilo pori tangia ujana wake mpaka umri wa utu uzima au mzaramo alietoka Dar. Katika kupiga kura asilimia kubwa watachagua mzaramo. Matokeo yake kwenye safari yao wengi wanaishia kuliwa na Simba.

Ni ujinga wa hali ya juu kumfanyia majungu Dr Gwajima wizara ya afya yaani ametulia na kuanza kuangaika na barakoa kwa sababu amko tayari kuona huduma za afya zinakuwa bora. Kila alipokuwa akifanya troubleshooting za kitaalamu kwa kukosoa watu kutofata system za afya mnaanza kumnanga. Afya ni system bro sio mtu bila ya wafanyakazi kuheshimu mifumo ya kazi utapewa huduma mbovu tu.

NHS England ni mfumo bora wa afya duniani (kwa kura za kimataifa) ni kwa sababu ya system. Pamoja na hayo ata huko ulaya wana madokta na nurses especially juniors wanaokosea medical procedures sana tu na kupelekea watu madhara au vifo vinavyoepukika (google mid-Staffordshire hospital) uone upuuzi wa management uliopelekea vifo chungu mzima vya wagonjwa.

To minimise risk kuna systems ambazo wanatakiwa wazifuate, kila kitu ni system kuanzia usafi, medical procedures (usijifanye sijui we umesoma miaka 7 hakuna upuuzi huo ni system first) documentation system, inter professional working system, maabara system, inventory control system and so forth with hospital management.

Dr Gwajima anazijua system za afya mnooooo kutokana na work experience as a medical practitioner, as a health manager, as a policy advisor and qualifications in medical health management ndio sababu ya kupewa hiyo wizara.

Imebidi apunguze kasi kwa sababu hampo tayari kuona ufanisi kwenye hiyo sector, kila akijaribu mna mtukana. Hila trust me ni ujinga wa hali ya juu kumfanyia majungu huyo mama anaijua afya.
 
Huyu mwenye kashfa akiwa Waziri apewe tena Uwaziri!!!!!!!!
 
Hizi tetesi zimesikika hapa Sanya juu kwenye tukio kubwa la kumsimika Chifu wa Siha Mangi Kileo.

Viongozi mbalimbali wa serikali wapo hapa hivyo tetesi kama hizi siyo za kupuuza.

Mangi Kileo ni miongoni mwa wasomi WANNE wa kwanza wa Tanzania kugraduate Makerere akiwemo pia mzee Cleopa David Msuya.

Mangi Kileo amehudumu serikalini katika nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo Katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii ambayo Kigwangalla alipata kuhudumu pia.

Lisemwalo lipo kama halipo laja.

Mungu wa mbinguni awabariki sana!
Kigwangwala kuwa Waziri wa Afya itakuwa kituko kikubwa sana , alipokuwa Naibu wa wizara hii alikuwa anaingia ofisini saa 10 alfajiri na kuwafungia mageti Wakurugenzi wa idara ili waonekane wamechelewa kazini , au umesahau vituko hivi ?

Badala ya kuboresha huduma za Hospitali yeye akaanza kupambana na Akina Mwaka waliokuwa wanauza lishe za Uzazi , haya kwenye utopolo huo alipata faida gani ?
 
Hii mambo ya kulamba lamba vyeo na positions za ku-rule over other human beings bila kuzitolea jasho unasubiri uteuliwe ni really ukoswaji wa akili

No human being who needs anybody to rule over him for him to live and endesha maisha yake

Hizi positions na vyeo ni absolutely useless...

As we estimate mpaka mwaka 2800 duniani hakutakua na mfumo unaoitwa serikali,utakua ni useless,human beings hawatataka tena kusimamiwa na mwanadamu mwingine ili society iweze ku-function....

Wanadamu watakua na IQ kubwa kiasi kwamba any idea ya "kiongozi" au cheo fulani itakua ni alien na foreign
Absolutely correct
 
Back
Top Bottom