Kigwangwala: Kama kudaiana, Simba tunamdai MO hela nyingi sana

Kigwangwala: Kama kudaiana, Simba tunamdai MO hela nyingi sana

Mashabiki wa simba wengi hawajasoma! Hawawezi kuelewa kingwala anazungumzia nini
Hapo kwenye coupon rate kawaacha wengi sana akiwemo sumbai
Timu ikiwa inafanya vizuri mashabiki huwa wanaweka masikio pamba kwa uongozi hata kama ni batili. Kigwangala hajaanza kuzungumzia hili leo. Alilizungumzia kipindi kile wakati simba iko kwenye peak akaishia kushambuliwa na Mo akaja kumsema kuwa aliomba mkopo kwake wa pikipiki akamkatalia. Najua leo wataungana naye as if ndipo kaanza kusema hivi.
 
Wakati Hamis Kigwangala anawaambia Wana Simba SC Tanzania ukweli kuhusu MO na mikataba yake, wengi walimtukana hasa wale mashabiki maandazi.

Sasa mmeanza kujua ukweli mmekaa kimya kama mmefumaniwa.

LuoBoy Media [emoji3578]
 
Mambo ya simba bora ungekaa kmy kama unakumbuka mambo ya simba na mzee kilomi yalivyo potea na hili swala litapotea kama upepo unapoteza mda wako bure
 
Mashabiki wa simba wengi hawajasoma! Hawawezi kuelewa kingwala anazungumzia nini
Hapo kwenye coupon rate kawaacha wengi sana akiwemo sumbai
Kwako kusoma ni mpaka mwanafunzi ajue maana ya coupon rate hata kama hiyo term haihusiani na course yake?!

Jitafakari.
 
Mashabiki wa simba wengi hawajasoma! Hawawezi kuelewa kingwala anazungumzia nini
Hapo kwenye coupon rate kawaacha wengi sana akiwemo sumbai
Sisi tunaupeo kuliko huyo Kigwangala wako. Note sentence yake ya mwisho yote ni njaa tu ili naye akapige pesa pale simba
 
Mbunge wa Nzega Vijijini Dr Kigwangala amesema aliwaambia Wananchi kuwa pale Msimbazi Hakuna Mwekezaji kuna Uhuni mtupu lakini hawakumuelewa

Wakasema Dr Kigwangalla ana chuki binafsi kwa sababu amenyimwa mkopo wa Tukutuku

Leo hii wote wanalia Wahuni hawajaingiza hata shilling 1 kwenye account ya Simba lakini wanasema wanaidai club mabilioni

Dr Kigwangalla amesema kimsingi Simba inamdai MO tsh billion 43.333

Naye Meya Mstaafu wa Chadema Kule Ubungo mh Boniface Jacob amesema kwa miaka 3 Simba imekuwa ikiendeshwa kitapeli na haijapata faida yoyote kama Club zaidi ya kumnufaisha Mwekezaji Guvu Moya

Wanachama wanaitaka Klabu yao
 
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Anaandika Mhe. Hamisi Kigwangwala

“Kama ni kudaiana tu, tena bila mikataba, basi na sisi wana @SimbaSCTanzania tunamdai mwekezaji pesa nyingi sana!”

“Tulimtaka aweke bilioni 20 kwenye account yetu ili tununue bonds, kumbe hakuweka! Kama angeweka tungenunua bonds za miaka 25, at a coupon rate of 15.95% tungepata faida ya bilioni 3.19 kila mwaka. Kwa miaka 7 aliyotuzubaisha bila mafanikio yoyote yale, tungevuna bilioni 22.33!

“Deni la pili: ni pesa alizotukosesha kutokana na ufadhili wa Azam - bilioni ngapi? Kwa mwaka ni bilioni 3. Kwa miaka 7 ni bilioni 21!

“Na yeye matangazo yake alikuwa analipia ufadhili kiasi gani?

“Tayari kwa haya mawili tu, tunamdai mwekezaji Glezabhai zaidi ya bilioni 43.33! Taja na wewe madeni mengine tunayomdai Glezabhai ili twende sawa!

“Halafu, Wajumbe wa Bodi waliokurupuka leo kutoka usingizini tuna jambo nao: watuambie walimpa Glezabhai mamlaka ya kumiliki timu yetu kwa msingi upi? Maana hakufuata prospectus ya mchakato wa transformation wa kampuni inavyotaka.

“Nimemuona Ndugu Issa akitumia Memorandum ya kampuni…how? Kama mchakato wa kulipia hisa haujakamilika hiyo document haina nguvu yoyote ile, ile bodi yao waliyokuwa wanakaa haina maana yoyote ile. Na wala Simba Sports Club haijauzwa na wala haidaiwi na mtu - kimsingi tumerudi GROUND ZERO!

“Ile bodi ilikuwa genge la watu walioiteka tu timu yetu kinyemela. Kwa taarifa za Ndg. Issa, maana yake Glezabhai hana haki wala mamlaka yoyote yale kisheria kwenye Simba. Simba SC ni club ya wanachama kwa asilimia 100.

“Wanachama tunamtaka Ndg. Mangungu aitishe mkutano mkuu haraka tuamue hatma ya club yetu. Kwenye mkutano huo aandae hesabu za mapato na matumizi ya Simba….kuanzia viingilio vya getini siku za mechi, mikataba ya mauzo ya bidhaa, mikataba ya mauzo ya haki za matangazo (ikiwemo ya bidhaa za Glezabhai, mbet nk), mapato ya CAF (robo fainali zote), n.k.

“Ndg. Mangungu na Kamati Tendaji wakishindwa kufanya hivi, tutaingilia kati kwa kuunda ‘kikosi kazi’ maalum (task force) cha kuiokoa club yetu.”
Kalpana wewe ni Wakili Msomi! Una maoni gani juu ya haya maelezo ya Mwana simba mwenzenu mh. Dr. Hamis Kigwangala, kuhusu Mwekezaji na pia mmiliki halali kabisa (kupitia maelezo yake mwenyewe) wa timu yenu?
 
Nimeanza kuuona ubabaishaji wa Mo kwenye kuisimamia na kuindesha klabu, simply ameuteka mfumo na channel zote za mapato ndani ya Simba Sc na kuzielekeza anapotaka yeye.

Tuanze sasa na ile bilioni 20 iko wapi?
Bilioni 20 gani tena Sheikh!! Kama ni zile zilizotolewa na Mwekezaji, zimetumika kusajilia wachezaji wakali kabisa!

Zimetumika kulipia mishahara na posho za hao wachezaji! Zimetumika kununulia mboga ya mchicha, zimetumika kumleta Manzoki mwenye ule uchaguzi wetu! Zimetumika kuisafirisha timu kwenye michezo ya ndani na ile ya Kimataifa, nk.
 
Ni kweli MO ni msanii lakini vipi kuhusu hawa viongozi upande wa wanachama ...

Walifanya nini kipindi Mo anadanganya?

Hapa wote wajiuzulu tuanze upya ...hao kina masoud si wasafi.
Hata hao kina Mangungu nao hawana maana, wamefeli, badala kuachia ngazi kistaarabu kwasababu ya kutofikia malengo bado wanakomaa mpaka wafukuzwe kwa aibu.

Uitishwe mkutano mkuu wa wanachama wa dharura waondoshwe wale.
 
Bilioni 20 gani tena Sheikh!! Kama ni zile zilizotolewa na Mwekezaji, zimetumika kusajilia wachezaji wakali kabisa!

Zimetumika kulipia mishahara na posho za hao wachezaji! Zimetumika kununulia mboga ya mchicha, zimetumika kumleta Manzoki mwenye ule uchaguzi wetu! Zimetumika kuisafirisha timu kwenye michezo ya ndani na ile ya Kimataifa, nk.
Huo mchicha wa bilioni 20 nataka kufahamu unauzwa masoko yapi hapa Dsm..
 
Jambo la muhimi ni kuwa Yanga na Azamu ndio watakaoiwakilisha nchi kwenye michuano ya kimataifa.
Hivyo Simba mnamuda wa kutosha wa kulumbana na hata mkitaka kuzichapa nyie zichapeni tu na hakuna kitakachoharibika
 
Back
Top Bottom