Kigwangwala: Kama kudaiana, Simba tunamdai MO hela nyingi sana

Kigwangwala: Kama kudaiana, Simba tunamdai MO hela nyingi sana

uzuri
Anaandika Mhe. Hamisi Kigwangwala

“Kama ni kudaiana tu, tena bila mikataba, basi na sisi wana @SimbaSCTanzania tunamdai mwekezaji pesa nyingi sana!”

“Tulimtaka aweke bilioni 20 kwenye account yetu ili tununue bonds, kumbe hakuweka! Kama angeweka tungenunua bonds za miaka 25, at a coupon rate of 15.95% tungepata faida ya bilioni 3.19 kila mwaka. Kwa miaka 7 aliyotuzubaisha bila mafanikio yoyote yale, tungevuna bilioni 22.33!

“Deni la pili: ni pesa alizotukosesha kutokana na ufadhili wa Azam - bilioni ngapi? Kwa mwaka ni bilioni 3. Kwa miaka 7 ni bilioni 21!

“Na yeye matangazo yake alikuwa analipia ufadhili kiasi gani?

“Tayari kwa haya mawili tu, tunamdai mwekezaji Glezabhai zaidi ya bilioni 43.33! Taja na wewe madeni mengine tunayomdai Glezabhai ili twende sawa!

“Halafu, Wajumbe wa Bodi waliokurupuka leo kutoka usingizini tuna jambo nao: watuambie walimpa Glezabhai mamlaka ya kumiliki timu yetu kwa msingi upi? Maana hakufuata prospectus ya mchakato wa transformation wa kampuni inavyotaka.

“Nimemuona Ndugu Issa akitumia Memorandum ya kampuni…how? Kama mchakato wa kulipia hisa haujakamilika hiyo document haina nguvu yoyote ile, ile bodi yao waliyokuwa wanakaa haina maana yoyote ile. Na wala Simba Sports Club haijauzwa na wala haidaiwi na mtu - kimsingi tumerudi GROUND ZERO!

“Ile bodi ilikuwa genge la watu walioiteka tu timu yetu kinyemela. Kwa taarifa za Ndg. Issa, maana yake Glezabhai hana haki wala mamlaka yoyote yale kisheria kwenye Simba. Simba SC ni club ya wanachama kwa asilimia 100.

“Wanachama tunamtaka Ndg. Mangungu aitishe mkutano mkuu haraka tuamue hatma ya club yetu. Kwenye mkutano huo aandae hesabu za mapato na matumizi ya Simba….kuanzia viingilio vya getini siku za mechi, mikataba ya mauzo ya bidhaa, mikataba ya mauzo ya haki za matangazo (ikiwemo ya bidhaa za Glezabhai, mbet nk), mapato ya CAF (robo fainali zote), n.k.

“Ndg. Mangungu na Kamati Tendaji wakishindwa kufanya hivi, tutaingilia kati kwa kuunda ‘kikosi kazi’ maalum (task force) cha kuiokoa club yetu.”
ubaya ni kwamba hizi ni zama za wasomi,mbumbumbu waliopambana na umande kipindi cha kusoma hamna budi kuwasaidia waliokimbia umande...imagine we ni mbumbumbu furthermore hujasoma...big up kigwa
 
Nimeanza kuuona ubabaishaji wa Mo kwenye kuisimamia na kuindesha klabu, simply ameuteka mfumo na channel zote za mapato ndani ya Simba Sc na kuzielekeza anapotaka yeye.

Tuanze sasa na ile bilioni 20 iko wapi?
Alikuwa anailipa kwa dose kila mwaka bilioni 5
 
Iyo pesa unayodai

Iyo pesa unayodai Mo alikuwa anatoa na imefika bilioni 20 ilikuwa kwenye makubaliano yapi ya kimkataba? Walikubaliana kwamba itabadilishwa iwe mtaji wa b.20? Kwanini yeye na wenzake walidanganya kwamba ameshaiweka benki? Alete ayo makubaliano kimaandishi kwamba pesa alizokuwa anatoa ndizo zigeuzwe kuwa mtaji wa b.20 vinginevyo uyu unamtetea lakini ni chanzo kikubwa Cha matatizo ya Simba, Mchakato wa mabadiliko kaukwamisha yeye kwa maana alishiriki kuendesha Mchakato huo kwa speed ya zimamoto wakati huo akijua Kuna vifungu vingi vya kisheria alivifunika kitu kilichopelekea serikali kumrudisha nyuma arekebishe vifungo ivyo vilivyokiukwa Kisha aendelee mbele, alikuwa anaitaka Simba kwa haraka sana kuliko kuzingatia masharti na kanuni za uwekezaji kwenye vilabu vya Tanzania Sasa awezi kumlaumu mtu kwamba anamkwamisha ni yeye mwenyewe ndie aliyejikwamisha asitafute huruma hapa!
Mumtetee lakini mjue keshayatimba na yashabumbuluka ivyo achutame!
Kwahiyo hizo mlizokuwa mnachukua mnasema nje ya mkataba...mlijua ni sadaka? Kwanza unajua maana ya mkataba? Mlikubaliana bilioni 19..Je mlikubaliana atoe zote kwa pamoja?

Watu walikua wanakula hela tu wanajua zimeanguka kwenye ndege!
Hazikuanguka kwenye ndege mzee... Zilitoka kwa Mo
 
Nimeanza kuuona ubabaishaji wa Mo kwenye kuisimamia na kuindesha klabu, simply ameuteka mfumo na channel zote za mapato ndani ya Simba Sc na kuzielekeza anapotaka yeye.

Tuanze sasa na ile bilioni 20 iko wapi?
Hiyo bil 20 si alinunua mchicha, soksi na boxer za wachezaji. Hujasikia CPA Issa akiliongelea hilo.
 
Bila kuondoa wasanii kwenye mpira wetu mpira hauwezi kupiga hatua!
Mtu ana CPA anakwambia alikuwa anasolve mambo kidemokrasia...
Mimi sijawahi kusikia neno demokrasia kwenye mahesabu kwa miaka yangu 21 niliyosoma.

Najua Kuna swali, njia na jibu!
Sijawahi kuona demokrasia hapo, ndio leo nasikia kwa CPA nabii Issa!
 
Mo anapaswa kuendelea kuwa Mfadhili kama Gharib. Hilo tunaliunga mkono.

Lakini ulaghai wake wa kutaka kujimilikisha SImba KINYUME NA UTARATIBU unapaswa kupigwa vita kwa nguvu zote.

Kuna wale wanaotaka matokeo uwanjani hata kama Timu iuzwe kwa ulaghai wao hawajali. Hawa ni wa kupigwa vita kwa nguvu zote pia.
 

HUJAELEWA AU MNAFANYA SPINNING KWA MAKUSUDI.

SHida iliyopo ni umiliki wa 49% za hisa za Simba.
Amwzipataje ?
Je utaratibu wa MOU umefuatwa?
Je makubaliano yalifuatwa?
Je mchakato ulishakamilika?
Jw alideposit hela kweli?
Wapi?
Inapaswa kuwa siri wakati Simba ni ya wanachama?
Kwa nini anafanya siri?
kama aliweka pesa je imenunua BONDS kweli ?

Kama haya yana UKAKASI basi Mo anafanya ulaghai kujimilikisha klabu kwa sababu ya NJAA ya wanachama.
 
Sisi tunaupeo kuliko huyo Kigwangala wako. Note sentence yake ya mwisho yote ni njaa tu ili naye akapige pesa pale simba
Viongozi wenu wameshathibitisha Mo hana umiliki wa 49% , we nani unabisha?

Wao ndo walipaswa kupokea 20B wamwkiri hawajapokea. We nani unabisha?

Unabariki huu ulaghai kwa hoja za kitoto, yaani Mnamuuzia mtu timu kitapeli. Kesho akiwa hayupo iwe mali ya familia yake😃😃
 
HUJAELEWA AU MNAFANYA SPINNING KWA MAKUSUDI.

SHida iliyopo ni umiliki wa 49% za hisa za Simba.
Amwzipataje ?
Je utaratibu wa MOU umefuatwa?
Je makubaliano yalifuatwa?
Je mchakato ulishakamilika?
Jw alideposit hela kweli?
Wapi?
Inapaswa kuwa siri wakati Simba ni ya wanachama?
Kwa nini anafanya siri?
kama aliweka pesa je imenunua BONDS kweli ?

Kama haya yana UKAKASI basi Mo anafanya ulaghai kujimilikisha klabu kwa sababu ya NJAA ya wanachama.
Sifanyi Spinning uzuri tuna reference kutoka huko kwenu.
Screenshot_20240609_162501_Instagram.jpg

Sasa hapa mlifikafika vipi,maana mpaka kufikia hatua hii maana yake mchakato wa kumkabidhi MO hizo asilimia 49 ulikamilika au ilikuwa ni SHOW OFF kuwakomesha Yanga?
 
Mo anapaswa kuendelea kuwa Mfadhili kama Gharib. Hilo tunaliunga mkono.

Lakini ulaghai wake wa kutaka kujimilikisha SImba KINYUME NA UTARATIBU unapaswa kupigwa vita kwa nguvu zote.

Kuna wale wanaotaka matokeo uwanjani hata kama Timu iuzwe kwa ulaghai wao hawajali. Hawa ni wa kupigwa vita kwa nguvu zote pia.
Mo aanzishe timu yake, je bilioni 5 Kwa mwaka zinatosha kuiendesha timu kama ya Simba?
 
Back
Top Bottom