Kigwangwala: Kama kudaiana, Simba tunamdai MO hela nyingi sana

Kigwangwala: Kama kudaiana, Simba tunamdai MO hela nyingi sana

Anaandika Mhe. Hamisi Kigwangwala

“Kama ni kudaiana tu, tena bila mikataba, basi na sisi wana @SimbaSCTanzania tunamdai mwekezaji pesa nyingi sana!”

“Tulimtaka aweke bilioni 20 kwenye account yetu ili tununue bonds, kumbe hakuweka! Kama angeweka tungenunua bonds za miaka 25, at a coupon rate of 15.95% tungepata faida ya bilioni 3.19 kila mwaka. Kwa miaka 7 aliyotuzubaisha bila mafanikio yoyote yale, tungevuna bilioni 22.33!

“Deni la pili: ni pesa alizotukosesha kutokana na ufadhili wa Azam - bilioni ngapi? Kwa mwaka ni bilioni 3. Kwa miaka 7 ni bilioni 21!

“Na yeye matangazo yake alikuwa analipia ufadhili kiasi gani?

“Tayari kwa haya mawili tu, tunamdai mwekezaji Glezabhai zaidi ya bilioni 43.33! Taja na wewe madeni mengine tunayomdai Glezabhai ili twende sawa!

“Halafu, Wajumbe wa Bodi waliokurupuka leo kutoka usingizini tuna jambo nao: watuambie walimpa Glezabhai mamlaka ya kumiliki timu yetu kwa msingi upi? Maana hakufuata prospectus ya mchakato wa transformation wa kampuni inavyotaka.

“Nimemuona Ndugu Issa akitumia Memorandum ya kampuni…how? Kama mchakato wa kulipia hisa haujakamilika hiyo document haina nguvu yoyote ile, ile bodi yao waliyokuwa wanakaa haina maana yoyote ile. Na wala Simba Sports Club haijauzwa na wala haidaiwi na mtu - kimsingi tumerudi GROUND ZERO!

“Ile bodi ilikuwa genge la watu walioiteka tu timu yetu kinyemela. Kwa taarifa za Ndg. Issa, maana yake Glezabhai hana haki wala mamlaka yoyote yale kisheria kwenye Simba. Simba SC ni club ya wanachama kwa asilimia 100.

“Wanachama tunamtaka Ndg. Mangungu aitishe mkutano mkuu haraka tuamue hatma ya club yetu. Kwenye mkutano huo aandae hesabu za mapato na matumizi ya Simba….kuanzia viingilio vya getini siku za mechi, mikataba ya mauzo ya bidhaa, mikataba ya mauzo ya haki za matangazo (ikiwemo ya bidhaa za Glezabhai, mbet nk), mapato ya CAF (robo fainali zote), n.k.

“Ndg. Mangungu na Kamati Tendaji wakishindwa kufanya hivi, tutaingilia kati kwa kuunda ‘kikosi kazi’ maalum (task force) cha kuiokoa club yetu.”
Wafuwazikewafuwao
 
Kama Mo ameweka pesa inamaana akiandamwa hivi atasusa mpaka maelewano yawepo na Club hataachia na hakuna pa kumpeleka kama kweli alitoa hizo pesa, tukija kushtuka msimu ushaisha tukiwa kapa.

Kama hakutoa pesa hastahili kuwepo, ni wa kumtoa kupitia sheria za Club na Nchi sababu msimu utaisha na janja janja zake.

ANGALIZO ni kuvurugana kumbe kuna chura mmoja mkubwa keshafanya yake, msimu unanza kukiwa na mgogoro. Vyura wamekuwa wajanja sana kwenye fitina, si wa uwapuuza.

MWANASIMBA NI VIZURI KUJUA UKWELI KABLA YA KUCHEMKA HOVYO NA KULIPUKIA UPANDE WOWOTE. Maoni ya mashabiki mitandaoni yana nguvu sasa usikurupuke ukatoa maoni ya kuumiza Club yako. Fahamu tatizo halisi, toa maoni. Usitoe maoni bila kujiridhisha na uhalisia wa tatizo.

SASA, Uhalisia utapatikana kwenye hesabu za miaka mitatu nyuma.
Iwapo kuna mtu mwenye Financial statements za miaka mitatu nyuma aziweke hapa. Ni rahisi sana kuzihoji B20 kwa kutazama tu namna timu ilivyojiendesha kupitia mahesabu.
 
Glezabhai muda mrefu tu alishaonyesha ni msanii lakini makolo waliweka pamba masikioni.
Kwahiyo unadhani GSM nl msafi? Hapa kajificha kwenye kivuli cha makombe miaka 3 mfululizo. Subir siku Yanga itakapofanya vibaya ndipo utakaposikia uchafu na upigaji wa GSM ukiibuliwa ndani ya Yanga
 
Jambo la muhimi ni kuwa Yanga na Azamu ndio watakaoiwakilisha nchi kwenye michuano ya kimataifa.
Hivyo Simba mnamuda wa kutosha wa kulumbana na hata mkitaka kuzichapa nyie zichapeni tu na hakuna kitakachoharibika
Kwahiyo hata muda wa kwenda kuwaamulia huna?
 
Alichoandika ni uongo?
Mbona pale kwenye Document alipofanya rejea inaonesha mwekezaji atamiliki hisa 50% na Wanachama hisa 50%. Wakati tuliambiwa mwekezaji atamiliki hisa 49% na wanachama hisa 51%. Huenda Kigwangala anatumia Document ambayo si sahihi.
 
Back
Top Bottom