Kigwangwala: Kama kudaiana, Simba tunamdai MO hela nyingi sana

Wafuwazikewafuwao
 
Kama Mo ameweka pesa inamaana akiandamwa hivi atasusa mpaka maelewano yawepo na Club hataachia na hakuna pa kumpeleka kama kweli alitoa hizo pesa, tukija kushtuka msimu ushaisha tukiwa kapa.

Kama hakutoa pesa hastahili kuwepo, ni wa kumtoa kupitia sheria za Club na Nchi sababu msimu utaisha na janja janja zake.

ANGALIZO ni kuvurugana kumbe kuna chura mmoja mkubwa keshafanya yake, msimu unanza kukiwa na mgogoro. Vyura wamekuwa wajanja sana kwenye fitina, si wa uwapuuza.

MWANASIMBA NI VIZURI KUJUA UKWELI KABLA YA KUCHEMKA HOVYO NA KULIPUKIA UPANDE WOWOTE. Maoni ya mashabiki mitandaoni yana nguvu sasa usikurupuke ukatoa maoni ya kuumiza Club yako. Fahamu tatizo halisi, toa maoni. Usitoe maoni bila kujiridhisha na uhalisia wa tatizo.

SASA, Uhalisia utapatikana kwenye hesabu za miaka mitatu nyuma.
Iwapo kuna mtu mwenye Financial statements za miaka mitatu nyuma aziweke hapa. Ni rahisi sana kuzihoji B20 kwa kutazama tu namna timu ilivyojiendesha kupitia mahesabu.
 
Glezabhai muda mrefu tu alishaonyesha ni msanii lakini makolo waliweka pamba masikioni.
Kwahiyo unadhani GSM nl msafi? Hapa kajificha kwenye kivuli cha makombe miaka 3 mfululizo. Subir siku Yanga itakapofanya vibaya ndipo utakaposikia uchafu na upigaji wa GSM ukiibuliwa ndani ya Yanga
 
Jambo la muhimi ni kuwa Yanga na Azamu ndio watakaoiwakilisha nchi kwenye michuano ya kimataifa.
Hivyo Simba mnamuda wa kutosha wa kulumbana na hata mkitaka kuzichapa nyie zichapeni tu na hakuna kitakachoharibika
Kwahiyo hata muda wa kwenda kuwaamulia huna?
 
Alichoandika ni uongo?
Mbona pale kwenye Document alipofanya rejea inaonesha mwekezaji atamiliki hisa 50% na Wanachama hisa 50%. Wakati tuliambiwa mwekezaji atamiliki hisa 49% na wanachama hisa 51%. Huenda Kigwangala anatumia Document ambayo si sahihi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…