Kihenzile afuturisha na kufanya Dua ya kumuombea Rais Samia

Kihenzile afuturisha na kufanya Dua ya kumuombea Rais Samia

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Mbunge wa Jimbo la Mufindi na Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile leo April 06,2024 ameungana na Viongozi wa Dini , Serikali pamoja na Wananchi kupata Iftar ya pamoja iliyoambatana na dua ya kumuombea Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuleta maendeleo katika Sekta mbalimbali katika kipindi cha miaka mitatu.

Iftari hiyo imefanyika nyumbani kwake Kijiji cha Ibatu Kata ya Igowole Wilayani Mufindi Mkoani Iringa.

Naibu Waziri Kihenzile amesema uamuzi huo wa kufanya dua ya kumuombea Rais Samia ni kwasababu ya mambo mengi aliyoyafanya ikiwemo sekta ya elimu ambapo amesema tayari madarasa zaidi ya 30 katika Jimho hilo yameshaongezwa huku katika Sekta ya barabara kukiwa na KM zaidi ya 30 ya barabara kutoka Luhunga hadi Ikani’ngombe na maeneo mengine korofi yameshakarabatiwa na amesema fedha nyingi zimetolewa kwaajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambayo ni ukombozi kwa Wananchi.

WhatsApp Image 2024-04-08 at 03.38.42.jpeg
WhatsApp Image 2024-04-08 at 03.38.42(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-04-08 at 03.38.43(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-04-08 at 03.38.45.jpeg
WhatsApp Image 2024-04-08 at 03.38.47.jpeg
WhatsApp Image 2024-04-08 at 03.38.48.jpeg
WhatsApp Image 2024-04-08 at 03.38.49.jpeg
 
Back
Top Bottom