Kihongosi: Ni Ngumu kujua anayeteka Watu Nchini, Vyombo vya Ulinzi vikibaini vitaleta Taarifa, Wananchi waripoti taarifa

Kihongosi: Ni Ngumu kujua anayeteka Watu Nchini, Vyombo vya Ulinzi vikibaini vitaleta Taarifa, Wananchi waripoti taarifa

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251



Odemba: Taarifa hizo zipo, ndio na sisi tunaziona. Kwamba watu wanatekwa hapa nchini? Ndio, watu wanapata changamoto. Nani anayeteka watu hapa Tanzania?

Kihongosi: Ni vigumu kujua jambo hilo ndugu Odemba, kwa sababu sisi kama Chama Cha Mapinduzi..."

Odemba: Kama chama tawala mmeshindwa kufahamu anaye..."

Kihongosi: ...sisi kama Chama Cha Mapinduzi..."

Odemba: ...ambacho ni chama tawala."

Kihongosi: Ndio, sisi kama Chama Cha Mapinduzi..."

Odemba: Ndio, chama tawala."

Kihongosi: Ndio, chama tawala. Tangu kuasisiwa kwetu tumekuwa tukithamini utu wa watu. Tukithamini undugu wa taifa letu na katika miongozo yetu ukisoma, tunathamini utu wa kila mmoja. Kwa hiyo sisi kama chama, matukio haya yanapotokea kwanza yanatuumiza sana."

Odemba: Mnaumizwa..."

Kihongosi: "...na matukio yote yanayotokea. Haya ambayo umeyataja, kama chama yanatuumiza sana. Na ndio maana yanapotokea matukio haya, tunasisitiza mamlaka zinazohusika ziweze kufanyia kazi. Lakini kama chama hatujawahi kufurahi kuona kwamba kuna mwananchi anapata changamoto. Kwa hiyo hilo jambo naweza nikakuthibitishia kwamba Chama Cha Mapinduzi tunaomba sana ata kwa wananchi, endapo kuna taarifa ambazo zinaashiria au watu wakabainika wanafanya vitendo hivyo, waweze kuripoti katika mamlaka husika ili kila anayehusika aweze kuchukuliwa hatua za kisheria kama sheria inavyotaka."

Odemba: "Nani anayeteka watu..."

Odemba: Nani anayeteka watu hapa nchini?"

Kihongosi: "Ni ngumu kujua nani anateka watu hapa nchini."

Odemba: "Na je, vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vimeshindwa kuwabaini wanaoteka watu hapa nchini?"

Kihongosi: "Wapo baadhi ya watu ambao wamekamatwa wanaohusika na vitendo vya kihalifu, lakini wengine kama ambavyo wanasema uchunguzi unaendelea. Kwa hiyo vyombo vinavyohusika naamini vinafanya kazi yao kwa weledi na kutimiza wajibu. Na pale majawabu yanapopatikana huwa wanaleta kwa umma kwamba tumebaini moja, tumebaini mbili, tumebaini tatu."

Odemba: "Kama chama tawala, ni hatua gani ambazo mnazichukua katika kukomesha matukio haya ya utekaji?"

Kihongosi: "Jambo kubwa ambalo chama sisi tunafanya ni kuelimisha umma kwamba wananchi ndio walinzi wa nchi. Huwezi kulinda nchi bila wananchi. Wanapoona kuna matukio yanatokea katika maeneo yao, ni wajibu wa wananchi kwa kushirikiana kwa pamoja na serikali kuweza kuripoti taarifa ili wanaohusika waweze kuchukuliwa hatua za kisheria, au endapo watabaini kwamba kuna watu wanafanya mambo yasiyofaa waweze kutoa taarifa. Na kuna kipindi tulitoa hata statement katika mikutano tunayoifanya kwamba mwananchi usipokee pia mgeni usiyemjua. Kwa sababu huwezi jua amekuja kwa dhamira ipi, anaweza akaleta maafa na lawama zikenda kwa nchi kumbe aliyetekeleza uhalifu ni mtu mwingine. Kwa hiyo wajibu wetu kama chama ni kuzidi kuelimisha wananchi, kuchukua hatua pindi wanapoona kuna viashiria ambavyo vinahatarisha usalama wao au usalama wa nchi yao."

Odemba: "Uniamini ya kwamba hipo siku watu wasiojulikana watakuja kujulikana katika taifa hili?"

Kihongosi: "Ninaiamini."

Odemba: "Muda wake ni lini?"

Kihongosi: "Siwezi kusema muda wake ni lini, lakini naamini ipo siku wanaotenda vitendo visivyofaa watabainika na sheria itachukua mkondo wake. Hilo ninaliamini kwa asilimia mia moja."

Odemba: "Nani atakayewabaini?"

Kihongosi: "Vyombo vyetu vya usalama binafsi ninaviamini sana."

Odemba: "Kwa wakati huu vyombo vyetu vya usalama havipo?"

Kihongosi: "Vipo na vinafanya kazi nzuri sana."

Odemba: "Kwa hiyo wameshindwa kubaini wasiojulikana katika..."

Kihongosi: "Maswala ya uchunguzi Odemba sio jambo la kulala na kuamka. Swala la uchunguzi ni jambo la kitaalamu, ni jambo linalohitaji muda, ni jambo linalohitaji weledi ili usije kumuonea mtu mwingine. Ni lazima ulifanye kwa umakini wa hali ya juu. Kwa hiyo kwa kuwa mimi na wewe hatuna taaluma hiyo, naimani wenye taaluma hiyo wanaendelea kufanya hii kazi na ukweli utajulikana, ninaamini hilo."

Pia soma: Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana
 
Mji umejaa walugaluga na waporipori
Kila anaekamatwa wao wanaona ametekwa, wanadhani huku watu wanakamatwa kama vijijini walikotoka ambapo mwenyekiti wa kijiji anakuja na sungusungu kukukamata
 
Abdul mtoto wa Samia ndo anateka watu. Mimi ni chombo na naomba uniamini. Ukikataa naandika kwa Verified ID.

Kihongosi, namba yangu unayo na tunajuana na hii ID unaijua. Badoo naamini umeongea kutetea ugali. Though bado nakuheshimu

Pumzika kwa Amani Mdude Nyagali 😭
Unadhani yeye hamjui anayeteka?
 
Abdul mtoto wa Samia ndo anateka watu. Mimi ni chombo na naomba uniamini. Ukikataa naandika kwa Verified ID.

Kihongosi, namba yangu unayo na tunajuana na hii ID unaijua. Badoo naamini umeongea kutetea ugali. Though bado nakuheshimu

Pumzika kwa Amani Mdude Nyagali 😭
Yaani ndondocha wa maporini unakaa huku iringa, halafu mtoto mdogo umemaliza chuo juzi ulikuwa huna hata hela ya joho la mhafali leo hii unadanganya walugaliga wenzako wa huko vijijini kwenu kuwa unamjua kihongosi wakuone wa mjini?

 
Huyu naye ni was hovyo tokeapo, sijui CCM wana Wana waokota wapi hawa wapuuzi.
Mxxxiiiieeew
 
Mji umejaa walugaluga na waporipori
Kila anaekamatwa wao wanaona ametekwa, wanadhani huku watu wanakamatwa kama vijijini walikotoka ambapo mwenyekiti wa kijiji anakuja na sungusungu kukukamata
Bishana na kihongosi.
 
Back
Top Bottom