#COVID19 Kihongosi: Polepole uwe na nidhamu na adabu kama ulivyokuwa Awamu ya Tano

#COVID19 Kihongosi: Polepole uwe na nidhamu na adabu kama ulivyokuwa Awamu ya Tano

Huyo Polepole ni wa kuwamvua hata huo ubunge wa dezo akajipange upya. Uzuri kashalikoroga, hana support ndani ya ccm, wala kwa wapinzani waliompaisha kipindi cha katiba mpya.
Waslaiti wote njia yao ni moja. Kukosa support na kuishia kuisoma namba tu.
 
Huyu Kihongosi mbona anatumia nguvu sana kupambana na wenzake!! Ila aweke akiba ya maneno maana hizi siasa Zina kurasa nyingi sana.
Anatakiwa awajibu kina zito na kina heche.
Kabisa mkuu!
Ajifunze kwa kina Halima na Slaa
 
Katibu mkuu wa Uvccm, Kenani Kihongosi amemtaka Mbunge Humphrey Polepole awe na nidhamu na adabu katika serikali ya awamu ya 6 kama alivyofanya kwa serikali ya awamu ya 5. Up

Hiyo ni baada ya Polepole kupinga chanjo, jambo linalochukuliwa kama kupingana na Rais.

Una maoni gani kwa wana ccm hao?
View attachment 1885601
Kihongosi aache ujinga bana,si kila mtu sababu yupo CCM basi aseme yale yanayomfurahisha kiongozi wao, kama mwenyekiti wake anasema kuchanja ni hiari na Polepole anasema hachanjwi tatizo lipo wapi? katibu wa jumuia ya vijana wa CCM ndio kawa msemaji wa CCM? nchi hii kila mtu yupo huru kusema lolote maadamu havunji sheria, sasa kwa kifungu kipi cha sheria au katiba kinasema ukisema tofauti na raisi ni kosa, huyu dogo aache kutoa matamko na kiherehere chake cha kujikomba hakitamsaidia kitu.
 
Hivi sasa hivi kupingana na mawazo au na mitazamo ya walio wengi ni makosa? Duuh.
Ndio Ni makosa makubwa sana na hili walianzisha jiwe,polepole na wenzake so acha wachume walichokipanda.
 
Guys kila mtu anahuru juu ya hili kwanini umulazimishe akubaliane tu kuchnanywa..overall polepole hajafika miaka 50 ndo maana nashangaa hata kilongozi kwanini amechanjwa wakati hajafika 50 unless kama anamagonjwa
Hata uchanjwe vipi siku ikifika hiyo chanjo inakuwa maigizo tu, muhimu tunza afya yako kwa kula chakula chenye virutubisho,kula matudna fanya mazoezi n.k
 
Ccm walikaa kimya Magufuli alipoingiza tabia ya kuzuia free speech. Leo wanafungana midomo kwa style Ile ile ya Magufuli. Huyo Polepole alikuwa ni mmoja wa waliosupport mwenendo mbovu wa Magufuli kuua uhuru wa maoni, acha avune matunda ya siasa chafu alizoshiriki kuzipandikiza.
Utamuota sana Hayati Magufuli wewe nyumbu badala ya kwenda kumwona Gaidi Mbowe huko Segerea! Unajisahahurisha mkuu!!?
 
Kelele zote chanjo dozi zenyewe milioni moja tu.tena za kutembeza bakuli!je mngenunua si mngewapa wasiochanja kesi za uhujumu uchumi na ugaidi.tuondoleni makelele nunueni za kutosha za Aina tofauti kuwe na chaguo
 
Huyu rockMwakibinga

Ni timu moja na yule aliyekuwa katibu wa VP

Mzee wa rambirambi hao wote ni walewale

Mama ongea na Mwanao....


Chini ya mtajwa hapo juu
Hahaha umemuona kumbe na Waziri nae kampiga biti Pole pole

Hivi kapanda nae ikulu au kabaki kwa Mpango?
 
Utamuota sana Hayati Magufuli wewe nyumbu badala ya kwenda kumwona Gaidi Mbowe huko Segerea! Unajisahahirisha mkuu!!?

Unapanick mpaka unashindwa kuandika vizuri, unajisahahirisha ndio nini?
 
Back
Top Bottom