#COVID19 Kihongosi: Polepole uwe na nidhamu na adabu kama ulivyokuwa Awamu ya Tano

#COVID19 Kihongosi: Polepole uwe na nidhamu na adabu kama ulivyokuwa Awamu ya Tano

Kweli ukiuvaa ukada wa chama kindakindaki au ukiendekeza tumbo unakuwa unaongozwa na unafiki au unatumia 40% tu ya uwezo wako kufikiri.

Hivi hapa Kihongosi ametumia angalau 20% ya uwezo wake kufikiri?

Kosa la Polepole ni lipi hasa?
Kutamka msimamo wake au kuhoji usalama wa chanjo?
Kenani alikuwa wapi wakati wa Magufuli kuhoji kwanini aruhusu chanjo kama anaona chanjo ndiyo adabu na heshima kwa raisi wake?
 
Kuna mawili!

Either hapa bavicha wanapotezwa maboya juu ya ishu ya Mbowe au
Nw i get you- At least ume-confirm kwamba mashtaka ya Mbowe ni bogus na ni mkono wa serikali. 🤣 🤣 🤣
 
Kwa sababu jiwe angeamua raia wote wachanjwe slowslow asingejitokeza kupinga
Guys kila mtu anahuru juu ya hili kwanini umulazimishe akubaliane tu kuchnanywa..overall polepole hajafika miaka 50 ndo maana nashangaa hata kilongozi kwanini amechanjwa wakati hajafika 50 unless kama anamagonjwa
 
Sio sasa hivi, Tangu zamani sasa. Bila shaka wewe utakuwa mtoto wa miaka ya 2000
Hivi sasa hivi kupingana na mawazo au na mitazamo ya walio wengi ni makosa? Duuh.
 
Mwakibibi
Polepole
Kenani
Gwajiboy
Shaka
Bashiru
Ni vibaraka kwa wakati maalumu.
Angalau ajitokeze Bashe na hoja aweza kueleweka japo unaibu umemnyima Uhuru wa mawazo kama mbunge
 
Huyu Kihongosi mbona anatumia nguvu sana kupambana na wenzake!! Ila aweke akiba ya maneno maana hizi siasa Zina kurasa nyingi sana.
Anatakiwa awajibu kina zito na kina heche.
Hajui kwamba siasa hubadilika ghafla.....
 
Katibu mkuu wa Uvccm, Kenani Kihongosi amemtaka Mbunge Humphrey Polepole awe na nidhamu na adabu katika serikali ya awamu ya 6 kama alivyofanya kwa serikali ya awamu ya 5. Up

Hiyo ni baada ya Polepole kupinga chanjo, jambo linalochukuliwa kama kupingana na Rais.

Una maoni gani kwa wana ccm hao?
View attachment 1885601
Mpumbavu na mpumbavu Sana Kihongozi ,,Kama wanataka basi waseme kuwa Chanjo ni lazma Wasiwe wanafiki wakusema kuwa Chanjo ni hiari huku kila anaeenda tofauti na kuchanjwa anaonekana kuwa msaliti, ,Hivyo watoe Tangazo kuwa kila mtanzania kwa lazma atachanjwa CHANJO,
 
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Ndugu Kenani Kihongosi amemtaka Mbunge wa kuteuliwa wa CCM na aliyewahi kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Ndugu Humphrey Polepole kuwa na nidhamu na adabu kipindi hiki cha Serikali ya awamu ya 6 iliyo chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kama aliyokuwa nayo kipindi cha awamu ya 5 iliyokuwa inaongozwa na Hayati Rais Magufuli na kumuonya kuwa kama Vijana hawatakubali na kuvumilia mtu yeyote ndani ya Chama hicho kuvunja heshima au kupinga maelekezo ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniah Mhe Samia Suluhu Hassan.

Ndugu Kihongosi amesema hawatavumilia maneno ya kejeli, dhihaka na mengine ya aina hiyo ambayo yanabeba dhamira ya kutia doa dhamira njema ya Rais Samia kwa nchi hii na kumtaka Ndugu Polepole kuacha mara moja mijadala yake kuhusu chanjo ambayo amekuwa akiibua siku za hivi karibuni.

Kihongosi ameenda mbali zaidi kwa kusema wanasikitika sana na matendo ya upotoshaji ya Polepole kuhusu suala la chanjo na kumtaka kukaa kimya kama hahitaji kuchanja lakini sio kujificha kwenye suala la chanjo kuipinga Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ambayo imeonyesha nia njema ya kuwalinda Watanzania.

Mwisho na tena kwa kukazia Ndugu Kihongosi akamtaka Polepole kuelewa kwamba CCM sio Chama cha kiharakati bali ni Chama kilichojijenga katika misingi ya kutii na kuheshimu viongozi hivyo jambo la kupingana na kuendeleza mijadala ambayo Mwenyekiti wa CCM ameshaitolea maelekezo ni utovu wa nidhamu.

Maneno hayo ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kenani Kihongosi ya kusikitishwa kwake na mienendo ya Mbunge Polepole yanakuja baada ya kushuhudia siku za hivi karibuni Ndugu Polepole akishiriki mijadala ya kwenda kinyume na maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Mhe Samia Suluhu Hassan, maelekezo ya Chama na Serikali kuhusu chanjo ya Uviko-19.

#MtumishiWaWote
#KaziIendelee
 
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Ndugu Kenani Kihongosi amemtaka Mbunge wa kuteuliwa wa CCM na aliyewahi kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Ndugu Humphrey...
Tanzania ya miaka hii siielewi, ila kuna Tanzania zangu Mbili hivi ( nazihifadhi ) Watu 'Wanafkki' kama huyu 'Taratibu' na Yule 'Mchokozi' wa sasa 'Mtu Huru' wangeshakuwa Historia ya 'Kiuhai' Kitambo mno na tumeshawasahau.
 
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Ndugu Kenani Kihongosi amemtaka Mbunge wa kuteuliwa wa CCM na aliyewahi kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Ndugu Humphrey Polepole kuwa na nidhamu na adabu kipindi hiki cha Serikali ya awamu ya 6 iliyo chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kama aliyokuwa nayo...
Mwosha yanamnyemelea. Pole pole peleka moto.
 
Kihongosi kulinda ugali kunahitaji bunduki kabisa siyo vijinenoneno tu.
 
Wakimalizana na wapinzani wataanza kugombana wao kwa wao.
 
Back
Top Bottom