Kipangaspecial
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 20,778
- 28,722
Acha walipuane mabomuWakimalizana na wapinzani wataanza kugombana wao kwa wao.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Acha walipuane mabomuWakimalizana na wapinzani wataanza kugombana wao kwa wao.
Humphrey Polepole ni mpuuzi na mnafiki sana! Hayati Rais Magufuli aliondoka kipindi ambacho hawakutegemea!Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Ndugu Kenani Kihongosi amemtaka Mbunge wa kuteuliwa wa CCM na aliyewahi kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Ndugu Humphrey Polepole kuwa na nidhamu na adabu kipindi hiki cha Serikali ya awamu ya 6 iliyo chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kama aliyokuwa nayo kipindi cha awamu...
Na bado laana zitawamaliza wote kama si Coronelia basi hata ukimwa.Mugambo wanaruka na kukanyagana.
Pole pole na Gwajima ni wanafiki.CCM inasemewa na Stephen Nyerere.!? Maskini Tanzania ndio tulipofikia hapa. Uhiari wa chanjo unafungwa na Rais kuchanja? Kwa nini waliochanja wawe na haki ya kuhimiza wasio chanja kuchanja. Wasio chanja wasiwe na haki ya kuhimiza watu waikatae chanjo nyenye walakini mwingi.
Kwa nini Mh Polepole na sio Mh Askofu Gwajima? Ubunge wa Polepole alipewa na JPM hili nalo UV-CCM hawalijui? Heshima hailazimishiwi itakuja yenyewe kutokana na matendo yako kwa jamii.
Polepole ndo atajua kuna haraka haraka!Yaani huyo Boya anamtishia Polepole.?
Mwenyekiti aliyepita alitoa Maelekezo gani?"Chama cha Mapinduzi (CCM) sio chama cha harakati bali ni chama kilichojijenga katika misingi ya kutii na kuheshimu viongozi, hivyo jambo lolote la kupingana au kuendeleza mijadala ambayo Mwenyekiti wa CCM Taifa ameshalitolea maelekezo ni utovu wa nidhamu" hayo yamesemwa leo tarehe08.08.2021 na Ndugu Kenani Kihongosi ambaye ni katibu wa umoja wa vijana ccm taifa
"Maendeleo hayana vyama lakini tuheshimu uhuru wa maoni yoyote ya kila mwananchi kutoa maoni yake siyo dhambi wala siyo kupinga kila mtu anamitazamo yake"
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Ndugu Kenani Kihongosi amemtaka Mbunge wa kuteuliwa wa CCM na aliyewahi kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Ndugu Humphrey Polepole kuwa na nidhamu na adabu kipindi hiki cha Serikali ya awamu ya 6 iliyo chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kama aliyokuwa nayo kipindi cha awamu ya 5 iliyokuwa inaongozwa na Hayati Rais Magufuli na kumuonya kuwa kama Vijana hawatakubali na kuvumilia mtu yeyote ndani ya Chama hicho kuvunja heshima au kupinga maelekezo ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniah Mhe Samia Suluhu Hassan.
Ndugu Kihongosi amesema hawatavumilia maneno ya kejeli, dhihaka na mengine ya aina hiyo ambayo yanabeba dhamira ya kutia doa dhamira njema ya Rais Samia kwa nchi hii na kumtaka Ndugu Polepole kuacha mara moja mijadala yake kuhusu chanjo ambayo amekuwa akiibua siku za hivi karibuni.
Kihongosi ameenda mbali zaidi kwa kusema wanasikitika sana na matendo ya upotoshaji ya Polepole kuhusu suala la chanjo na kumtaka kukaa kimya kama hahitaji kuchanja lakini sio kujificha kwenye suala la chanjo kuipinga Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ambayo imeonyesha nia njema ya kuwalinda Watanzania.
Mwisho na tena kwa kukazia Ndugu Kihongosi akamtaka Polepole kuelewa kwamba CCM sio Chama cha kiharakati bali ni Chama kilichojijenga katika misingi ya kutii na kuheshimu viongozi hivyo jambo la kupingana na kuendeleza mijadala ambayo Mwenyekiti wa CCM ameshaitolea maelekezo ni utovu wa nidhamu.
Maneno hayo ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kenani Kihongosi ya kusikitishwa kwake na mienendo ya Mbunge Polepole yanakuja baada ya kushuhudia siku za hivi karibuni Ndugu Polepole akishiriki mijadala ya kwenda kinyume na maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Mhe Samia Suluhu Hassan, maelekezo ya Chama na Serikali kuhusu chanjo ya Uviko-19.
#MtumishiWaWote
#KaziIendelee