Sehemu ya Nukuu za Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndugu. Kenani Kihongosi Akimjibu Mbunge wa Kuteuliwa na Rais Ndugu Humphrey Polepole.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi - UVCCM, Ndugu. Kenani Kihongosi amesema, wanasikitishwa na matendo yanayofanywa na mbunge Humphrey Polepole kuhusu suala la chanjo ya corona, kwani Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameshasema kwamba chanjo ni hiyari na maamuzi yake lazima yaheshimiwe.
"Tunapenda kumwambia mbunge Humphrey Polepole kwamba awe na nidhamu na adabu kama aliyokuwa nayo wakati wa Utawala wa Awamu ya Tano. Nidhamu ile ile aiendeleze pia katika utawala huu wa awamu ya Sita Inayoongozwa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan " Kenani Kihongosi, Katibu Mkuu wa UVCCM.
"Mijadala yake (Humphrey Polepole) kuhusu chanjo ni bora akakaa kimya kama hahitaji kuchanja lakini sio kujificha katika kivuli cha chanjo kuipinga serikali." Kenani Kihongosi, Katibu Mkuu wa UVCCM.
"Tunamuonya na tunamtaka Humphrey Polepole aache mara moja mijadala yake kuhusu chanjo kwani hatutakubali kiongozi yoyote avunje heshima ya Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan au kupinga yale aliyoyaelekeza" Ndugu Kenani Kihongosi, Katibu Mkuu wa UVCCM.
"Hatutovumilia utovu wowote wa nidhamu kwa Rais. Humphrey Polepole kuendelea kutengeneza maneno ya kejeli, dhihaka na mengine ya aina hiyo yanabeba mazingira yanayotia shaka dhamira yake aliyonayo kwa Mwenyekiti wetu na Rais wetu, hivyo tunamtaka aache mara moja" Kenani Kihongosi.
"Chama cha Mapinduzi (CCM) siyo chama cha harakati bali ni chama kilichojijenga katika misingi ya kutii na kuheshimu viongozi, hivyo jambo lolote la kupingana au kuendeleza mijadala ambayo Mwenyekiti wa CCM Taifa ameshalitolea maelekezo ni utovu wa nidhamu" Ndugu Kenani Kihongosi.
Ndugu. Kenani Kihongosi
Katibu Mkuu wa UVCCM.
View attachment 1885779
View attachment 1885780