#COVID19 Kihongosi: Polepole uwe na nidhamu na adabu kama ulivyokuwa Awamu ya Tano

#COVID19 Kihongosi: Polepole uwe na nidhamu na adabu kama ulivyokuwa Awamu ya Tano

Gwajima hana njaa!
Pesa zake zipo Tanzania shughuli zake zipo Tanzania kwenda nje hawezi hajachanja.Katiba yetu mbovu imempa madaraka makubwa mtu mmoja. Hivi wakimfanyia figisu kanisa lake likafungwa,akaunti zake zikawafreezed kupisha uchunguzi utasema Gwajima Hana Njaa?

Kama Kweli Gwajima mwamba kwanini kwenye kauli zake anamponda waziri lkn hapohapo anasema anamuunga Mkono Rais hampingi?
Anachotakiwa Gwajima Ni kutokujisahau na kuvuka Mstari.
 
Ni kweli serikali imeshasema suala la chanjo ni hiari,hivyo anachofanya mh.Polepole siyo sawa kuwachanganya wananchi kwani yeye siyo mtaalam wa afya.ilikuwa ni lazima kuleta chanjo kwa makundi ambayo huwezi kuwanyima fursa hiyo kama mabalozi,...
Polepole amepinga na kuzuia kuletwa chanjo kwa wanaotaka?
 
Pesa zake zipo Tanzania shughuli zake zipo Tanzania kwenda nje hawezi hajachanja.Katiba yetu mbovu imempa madaraka makubwa mtu mmoja.Hivi wakimfanyia figisu kanisa lake likafungwa,akaunti zake zikawafreezed kupisha uchunguzi utasema Gwajima Hana Njaa?..
Gwaji vita vyake ni vya kiroho..ukilianzisha naye anakufuta kwenye ulimwengu wa kiroho na unapotea mazima..muulize mstaafu rc
 
Guys kila mtu ana uhuru juu ya hili kwanini umlazimishe akubaliane tu kuchnanywa..overall polepole hajafika miaka 50 ndo maana nashangaa hata kilongozi kwanini amechanjwa wakati hajafika 50 unless kama anamagonjwa
Hajalazimishwa, chanjo ni HIYARI imeshaelezwa. Sasa yeye kama hataki akae KIMYA siyo kuja kwenye mitandao kupinga chanjo kwa ujumla wake.
 
Gwaji vita vyake ni vya kiroho..ukilianzisha naye anakufuta kwenye ulimwengu wa kiroho na unapotea mazima..muulize mstaafu rc
Gwajima anapigana Vita ya Kiroho?
Gwajima huyuhuyu aliyedanganya anafufua watu kumbe uongo,Gwajima huyuhuyu aliyesema hawezi kuwa Mbunge Mana kazi anayofanya Ni kubwa kuliko Ubunge au Urais lakini leo Ni Mbunge,au Kuna Gwajima mwingine anayepigana Vita ya Kiroho sio Huyu?
 
Namkumbuka sasa. Huyu ndiye aliyekuwa anachapa watu viboko Arusha. Huyu akikuambia ujihadhari Ina maana anataka kukuchapa viboko. Ha ha ha.

Akiwa Iringa kama katibu wa uvccm aliwahi kusema hadharani pia kwamba wapinzani wa serikali ya hayati wanapaswa kuuwawa. Muda si mrefu baada ya hapo alizawadiwa u-DC wa Arusha. Ni mtaalamu mzuri wa kuramba miguu ya wakuu.
 
Katibu mkuu wa Uvccm, Kenani Kihongosi amemtaka Mbunge Humphrey Polepole awe na nidhamu na adabu katika serikali ya awamu ya 6 kama alivyofanya kwa serikali ya awamu ya 5. Up....
Kamarada H.Polepole anafeli wapi?

Mbona sote tunaijua CCM vyema kwa kuheshimu na kutii wenyeviti wa awamu zote?

Anafeli wapi ndugu huyu?

Mbona haya ni mapya?

Aliyemuondoa katika nafasi ya UENEZI ni hayati JPM na si mh.mwenyekiti Rais SSH.

Anafeli wapi kaka yetu huyu?
 
Akiwa Iringa kama katibu wa uvccm aliwahi kusema hadharani pia kwamba wapinzani wa serikali ya hayati wanapaswa kuuwawa. Muda si mrefu baada ya hapo alizawadiwa u-DC wa Arusha. Ni mtaalamu mzuri wa kuramba miguu ya wakuu.
CCM sio wa kuwashangaa
 
Katibu mkuu wa Uvccm, Kenani Kihongosi amemtaka Mbunge Humphrey Polepole awe na nidhamu na adabu katika serikali ya awamu ya 6 kama alivyofanya kwa serikali ya awamu ya 5. Up...
Mbona waliokubali chanjo hawasumbuliwi,kila mtu ana mtazamo wake na suala la afya ya mtu ni jambo la hiari.
 
Mimi sina shida kupinga au kuunga mkono. Ukipinga walau uwe na sababu - mfano umefanya utafiti kwamba chanjo tulizopokea Tanzania zina madhara A-Z na utafiti wako huo uwe pia unaonyesha mbadala. Vinginevyo ni porojo tu - za mara mabeberu mara nini wakati huo huo umevaa nguo zao, tai yao, viatu vyao, unatumia komputa yao, simu yao, TV yao, gari lao etc na wewe mwenyewe mwenye porojo hakuna mchango wako wowote chanya ambao umeshaufanya kwa dunia leo hii in terms of science and technology, achilia mbali humanitarian aid kama kukitokea maafa au janga fulani.
 
Katibu mkuu wa Uvccm, Kenani Kihongosi amemtaka Mbunge Humphrey Polepole awe na nidhamu na adabu katika serikali ya awamu ya 6 kama alivyofanya kwa serikali ya awamu ya 5. Up

Hiyo ni baada ya Polepole kupinga chanjo, jambo linalochukuliwa kama kupingana na Rais.

Una maoni gani kwa wana CCM hao?

---
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi - UVCCM, Kenani Kihongosi amesema, wanasikitishwa na matendo yanayofanywa na mbunge Humphrey Polepole kuhusu suala la ya Covid-19, kwani Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameshasema kwamba chanjo ni hiyari na maamuzi yake lazima yaheshimiwe.

"Tunapenda kumwambia mbunge Humphrey Polepole kwamba awe na nidhamu na adabu kama aliyokuwa nayo wakati wa Utawala wa Awamu ya Tano. Nidhamu ile ile aiendeleze pia katika utawala huu wa awamu ya Sita Inayoongozwa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan "

"Mijadala yake (Humphrey Polepole) kuhusu chanjo ni bora akakaa kimya kama hahitaji kuchanja lakini sio kujificha katika kivuli cha chanjo kuipinga serikali."

"Tunamuonya na tunamtaka Humphrey Polepole aache mara moja mijadala yake kuhusu chanjo kwani hatutakubali kiongozi yoyote avunje heshima ya Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan au kupinga yale aliyoyaelekeza"

"Hatutovumilia utovu wowote wa nidhamu kwa Rais. Humphrey Polepole kuendelea kutengeneza maneno ya kejeli, dhihaka na mengine ya aina hiyo yanabeba mazingira yanayotia shaka dhamira yake aliyonayo kwa Mwenyekiti wetu na Rais wetu, hivyo tunamtaka aache mara moja"

"Chama cha Mapinduzi (CCM) siyo chama cha harakati bali ni chama kilichojijenga katika misingi ya kutii na kuheshimu viongozi, hivyo jambo lolote la kupingana au kuendeleza mijadala ambayo Mwenyekiti wa CCM Taifa ameshalitolea maelekezo ni utovu wa nidhamu"

Ndugu. Kenani Kihongosi
Katibu Mkuu wa UVCCM.
Hivi nyie watu mna akili au hamnazo? Yes Samia is our president hamna anaepinga hilo, ila linapokuja suala la chanjo ni suala la mtu binafsi..kama una influence watu wapige chanjo vile vile watu kama sisi tuta influence watu wasichanje kwa sababu za kisayansi kabisa...sio watu wanaopinga chanjo niwajinga. There's a lot of evidences hizi chanjo zinaweza kuwa na madhara makubw kwa binadamu. Afya yangu ni yangu sio ya rais wala ya bill gates wala binadamu yoyote yule...nilizaliwa wenyewe nitakufa mwenyewe.

Hili suala linaweza kugawa taifa vibaya sana. Kwanza wakristo wengi hawataki hii chanjo wanalihusisha na suala la kiimani. Isipotumika busara ni hatari sana huko mbeleni.

Pia mnafanya kazi kwa data zipi? Vijana hawafi na corona..na hili taifa ni la vijana almost 65% mnataka kumchoma nani hizo experimental vaccine?
 
Mama Samia angetawala vizuri na kwa mafanikio makubwa kama angeshirikiana na wapinzani kuliko hao wanafiki ndani ya CCM. Weka kikao ongea na wapinzani - wape way forward ya katiba mpya ambayo ndiyo takwa lao kubwa kwa sasa - mkikubaliana time frame then muanze kujenga nchi kwa pamoja mkisubiri muda huo ili kuifufua katiba mpya ya Jaji Warioba.

CCM hii itamwingiza mama chaka asipokuwa makini.
 
Guys kila mtu ana uhuru juu ya hili kwanini umlazimishe akubaliane tu kuchnanywa..overall polepole hajafika miaka 50 ndo maana nashangaa hata kilongozi kwanini amechanjwa wakati hajafika 50 unless kama anamagonjwa

Kigezo cha umri ni kwa hizi chanjo za bure 1,000,000 zilizo kuja mwanzo na ziko chache ndio maana kuna makundi ya kipau mbele. Kama utaenda kuichanja kwingine au zikija kwa wingi kigezo hicho hakipo.
 
Gwajima anapigana Vita ya Kiroho?
Gwajima huyuhuyu aliyedanganya anafufua watu kumbe uongo,Gwajima huyuhuyu aliyesema hawezi kuwa Mbunge Mana kazi anayofanya Ni kubwa kuliko Ubunge au Urais lakini leo Ni Mbunge,au Kuna Gwajima mwingine anayepigana Vita ya Kiroho sio Huyu?
Huyohuyo...ni mpaka upate ufunuo wa kumwelewa
 
Guys kila mtu ana uhuru juu ya hili kwanini umlazimishe akubaliane tu kuchnanywa..overall polepole hajafika miaka 50 ndo maana nashangaa hata kilongozi kwanini amechanjwa wakati hajafika 50 unless kama anamagonjwa
Delta haziangalii miaka.... Inasomba kote kote.
 
Back
Top Bottom