Kiingereza cha Rais Samia

Tunahitaji Mpendwa Mheshimiwa Rais wetu awe anajua Kiingereza cha kawaida tu , hatuhitaji awe mtaalamu wa hiyo lugha kama vile anaenda kufundisha Oxford Univ.

Tunamsitiri Rais wenu Biden jinsi dishi lilivyoyumba katika hotuba zake ..
 
Kwenye kutojua facts ndogo ndogo kwa level ya Mkuu wa nchi nitaungana na wewe kwasababu inaonesha uvivu au uzembe wa kutojishughulisha kufahamu Mambo. Hili ni janga kwa viongozi wengi

Hata hivyo, hapa kwenye ujuvi wa lugha huu ni mwendelezo wa utumwa wa kifikra!. Kudhani kujua lugha vizuri ya kizungu ndo usomi na ujuvi wa Mambo huu ni uhayawani

Tunapoelekea watakuja wajukuu/ vitukuu wetu na watatucheka sana wanakapokuta mijadala ya kutukuza lugha za wenzetu huku yetu ikitushinda

Huwa nashangaa sana! Lugha ni sehemu ya utamaduni wa binadamu na hakuna binadamu aliyepiga hatua kimaendeleo kwa kuamua kudharau vya kwake na kutukuza vya watu. Huu ni uhayawani
 
Kwani wao Wamarekani wanaongea vizuri Kiswahili? Hebu mchukue Biden, anaweza kuzungumza Kiswahili (bila kukoseakosea?)..Acha hizo Ngabu!
 
Uwezo wake mkubwa sana kwa lugha ya malkia kulinganisha na mwendazake. Huyo alikuwa ni aibu sana.
 

Wewe ni miongoni mwa Watanzania wachache wenye akili.
Watanzania wengi tunafikiri kujua kiingereza ndio kuwa na akili. Sijui ni nani aliye turoga na kutujaza ujinga huu.
Mara nyingi tuna pima uwezo wa viongozi wetu kwa kuangalia uwezo wao wao wa kuzungumza kiingereza badala ya kuangalia ufanisi wao wa utendaji kazi.
Jamini tuamke kiingireza sio kipimo cha akili au uwezo wa kuongoza. Kiingereza ni lugha kama lugha zingine. Tutoke huko utumwa wa fikra.
 
Kuiinganishal hata hicho chenye walakini Cha Samia na cha hayati Mwendakuzimu ni matusi makubwa.
 
Wanajilinganisha na waingereza kwenye lugha

Ova
 
Wabongo ni wajinga sana, Sasa unalazimisha azungumze kama muingereza wakati sio lugha yake?
 
Ikiwasaidia wao ,Tzn inafaidia..
 
1. Ndugu Nyani Ngabu, ni kweli katika eneo la kuimudu lugha anaweza asiwe mzuri, however, huyu mama is far better than Mr Magufuli..

2. Kwa upande mwingine, inaeleweka kuwa, lugha ya kiingereza ni lugha ya tatu kwetu sisi Watanzania baada ya lugha zetu za asili na kiswahili. Na kwa hiyo, wote hatukimudu kiingereza unless uwe umekulia huko huko kwa wanaotumia lugha kiingereza kwa mawasiliano ya kila siku..

3. Kwa ishu ya kujiamini ktk platforms za kimataifa, nakubaliana na wewe kuwa, lipo kwa huyu mama na lilikuwa kubwa zaidi kwa aliyemrithi kiti hicho, Magufuli;

Tatizo hili liko kwa watanzania wote tokana na zifuatazo..

✓Mfumo wetu wa elimu ya kuchapana viboko unawatia hofu badala ya kujiamini watoto wetu..

✓Mfumo wetu wa kisiasa na kiutawala unajenga hofu kwa watu badala ya kujiamini..

✓Kwa viongozi wetu akiwemo Rais Samia ni kukosa international exposure. Na kwa kuwa ni Rais, basi ndiyo tu anaipata kwa sasa. I am sure akifanya PC briefing kama hii mbili au tatu huko nje, kutampa kujiamini..
 
Hata Uingereza kwenyewe ukiishi hapo unakuja kugunduwa kingereza hicho wana tofauti England, Irish na Scotland.
Alafu kuna mtu humu anakuambia kiswahili hakina maana kwa mzungu/mgeni Hahaha
Wakati wanaokuja kuwekeza wanafanya juu chini mpaka wakifahamu lugha hii

Ova
 
Marais wa Tanzania waliotuwakilisha vizuri kwenye hii lugha walikuwa ni Julius Nyerere na Benjamin Mkapa tu, hawa wengine hakuna kitu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…