Kiingereza cha Rais Samia

Kiingereza cha Rais Samia

Halafu hivi ni mimi tu [maana nisije kuwa na nitpick] au mbele/ pembeni ya Kamala, Hangaya kaonekana kama hana gravitas?

IMG_0843.png
 
Akiwa anasoma, kuna afadhali kidogo.

Lakini akiwa anaongea kutoka kichwani ambayo hayajaandikwa [hajaandikiwa], anapata shida sana.

Yaani Magu na Hangaya walichaguana wote wakiwa weupe kwenye hiyo lugha pendwa.

Muangalie na msikilize kwenye video hapo chini. Yale ambayo hayajaandikwa [hajaandikiwa] kwenye karatasi, anapata shida kuyaongea.

Anajiuma uma tu. Hajiamini. Mpaka hata taarifa za ukweli [facts] anazikosea.

Uchaguzi mkuu wa Marekani wa 2020 haukuwa uchaguzi wa kwanza wa nchi hiyo kuwa na mwanamke kama mgombea umakamu wa Rais.

Wakati Geraldine Ferraro anagombea kwenye tiketi moja na Walter Mondale, Hangaya alikuwa wapi?

Wakati Sarah Palin anagombea na John McCain, Hangaya alikuwa wapi?

Au alitaka kusema kuwa 2020 ndo mara ya kwanza kwa mwanamke kuwa katika tiketi iliyoshinda uchaguzi lakini akajiuma uma na akakosea hizo basic facts?

Halafu, ni ‘the United States and Tanzania have enjoyed excellent relations [siyo relation], for the last [past sounds much better] 60 years’.

Halafu kuna watu wanadai eti Hangaya yuko vizuri kwenye Kiingereza 🤣. Ama kweli hii lugha ni janga la kitaifa.

Maana mtu yeyote aijuaye vizuri hiyo lugha hawezi kusema eti Hangaya yuko vizuri.

Hangaya na Magu labda wanapishana kwenye lafudhi tu. Magu alikuwa na lafudhi nzito/ nene zaidi. Hangaya ya kwake si nzito kivile, hivyo kuonekana kama vile anaimudu, kumbe wapi!

Kwenye sintaksia, semantiki, sarufi, kunyambua vitenzi, n.k., hawapishani sana. Wote mulemule tu.

Kizungu atakijua wapi na ilmu yake yakuunga unga
 
Kuhusu facts ndogo ndogo nimewahi kuuliza wanao muandalia speech wanakuwaga na lengo Gani na yeye kwa nini huwa hazikagui,

Hofu yangu huyu bibi ni mvivu Fulani ni mtu wa kulishwa Kila kitu...

Nilishangaa na Mimi kusikia Kamala ndio mgombea wa kwanza mwanamke...

Kingine Samia siyo mtu wa kusikiliza na kutoa arguments, Bali wa Ndiyo ndiyo Kila unapomwabia kitu, nilisikia hii wakati Kamala anazungumza

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
IMG_0821.jpg
 
Hapana.

Fluency haihusiani na kusoma vilivyoandikwa.

Ni kwamba hana lafudhi nzito/ nene. Hicho ndicho kinachomfanya aonekane ana afadhali.

Lakini maneno mengi sana yanampa shida kuyatamka.

Hata yale maneno ya kawaida ya hiyo lugha hawezi kuyatamka vizuri.

Ukimwandikia neno kama ‘xylophone’ au ‘discombobulation’, anaweza kupoteza fahamu akijaribu kuyatamka.

IMG_0891.jpg

Ndio alivyo,tuombe Mungu watu wanaomzumguka wawe smart vinginevyo ni hatari
 
Kuhusu facts ndogo ndogo nimewahi kuuliza wanao muandalia speech wanakuwaga na lengo Gani na yeye kwa nini huwa hazikagui,

Hofu yangu huyu bibi ni mvivu Fulani ni mtu wa kulishwa Kila kitu...

Nilishangaa na Mimi kusikia Kamala ndio mgombea wa kwanza mwanamke...

Kingine Samia siyo mtu wa kusikiliza na kutoa arguments, Bali wa Ndiyo ndiyo Kila unapomwabia kitu, nilisikia hii wakati Kamala anazungumza
Marekani ishakuwa na wagombea wawili wanawake wa katika nafasi ya umakamu wa Rais kutoka vyama vyao viwili vikubwa kabla ya Kamala.

Hangaya hajui hayo!

Hata Wikipedia huwa hachungulii?
 
Huyu alizaliwa na kukulia Butiama huko.

Hebu mcheki hapo. Super impressive.

Hasomi popote.

Huyu alikuwa bright sana na ana exposure kubwa..Tatizo nature ya eneo analotoka mzee Ngabu,kule kwao mwaka jana matokeo ya form four kisiwa kizima hakuna division one ni wazi kuwa weng wao kujishughulisha kupata Knowledge mpya ikiwemo hii ya Lugha ni mtihan sana tu
 
Kwa aina ya wananchi wetu mama anajua sana na anajitahidi. Kumbuka lugha huwa ina kuwa affected na mothertongue.

Mimi nimefurahi raisi wangu anapoongea kwenye platform kama hiyo, kuachilia mbali wanawake wengi wanauoga kuongea mbele za watu haswa wa kiislamu. Anatamka maneno tunayaelewa makosa madogomadogo ni kawaida. Huwezi kumlinganisha Raisi wa ghana na George weah kwenye pronounciation, choice of words and mannerism when they conversate.
 
😂😂mwenzako hajakaa Marekani kama wewe mkuu,mtu wa Huku Kizimkazi katembea sana ni hapa Dar na Dodoma unataka kumuweka daraja sawa na mtu wa Cleveland,Salt lake,Idaho,wichita,New york na Atlanta?? Tumvumilie tu mkuu yatakwisha
Kuijua lugha si lazima uishi huko, miaka ya sitini wanafunzi walikuwa wanakijua vizuri kiingereza ndiyo sababu iliwawezesha kupata krediti kwenye mitihani ya Kembriji, fahamu walikuwa wa shule za serikali.
 
Hahahha yaani ukiwa kichwa panzi we kichwa panzi tu! Yaani taarifa za akina Hillary Clinton walishawahi kugombea!
 
Hapana.

Fluency haihusiani na kusoma vilivyoandikwa.

Ni kwamba hana lafudhi nzito/ nene. Hicho ndicho kinachomfanya aonekane ana afadhali.

Lakini maneno mengi sana yanampa shida kuyatamka.

Hata yale maneno ya kawaida ya hiyo lugha hawezi kuyatamka vizuri.

Ukimwandikia neno kama ‘xylophone’ au ‘discombobulation’, anaweza kupoteza fahamu akijaribu kuyatamka.
Gazeti la New York times nimeona kuna kipande wamemtaja kwamba ms Samia who is "soft spoken" sa sijui wamependa uongeaji wake huo au wamemind?
 
Sioni kama ni tatizo kubwa sio mother tongue yao JPM na Samia sio lazima waongee fluently.

Mfumo wetu wa elimu wa zamani kiingereza hakikupewa nafasi kubwa hata uwe na PHD hauwezi ongea fluent English.

Siku hizi English medium ndio zinasaidia kuwa fluent sababu watoto wanajua kirahisi zaidi.

Tunamjudge kiongozi wetu kwa vigezo muhimu vipaumbele ktk policies,Diplomacies etc sio kiingereza.
 
Kwa aina ya wananchi wetu mama anajua sana na anajitahidi. Kumbuka lugha huwa ina kuwa affected na mothertongue.

Mimi nimefurahi raisi wangu anapoongea kwenye platform kama hiyo, kuachilia mbali wanawake wengi wanauoga kuongea mbele za watu haswa wa kiislamu. Anatamka maneno tunayaelewa makosa madogomadogo ni kawaida. Huwezi kumlinganisha Raisi wa ghana na George weah kwenye pronounciation, choice of words and mannerism when they conversate.
“Conversate” is nonstandard English.

The correct word is ‘converse’.
 
Back
Top Bottom