Kiingereza cha Watanzania wengi ni cha kuandika, kusoma na kuongea kwa kusoma maandishi. Tatizo ni kusikiliza, kuelewana na kuongea freely

Kiingereza cha Watanzania wengi ni cha kuandika, kusoma na kuongea kwa kusoma maandishi. Tatizo ni kusikiliza, kuelewana na kuongea freely

Kujua kiingereza halafu huna mbuni kipande mfukoni ni uharibifu wa lugha za watu tu.
Kiingereza hakipaswi kuwa kipimo cha maendeleo, kiingereza ni lugha kama ilivyo kisukuma tu.

Putin anajambisha dunia sasa hivi lakini ni nadra kumsikia akiongea kiingereza na si kwamba hakijui, lakini kwake hakina umuhimu wala si kipimo cha mafanikio yake.

Huyo wa ze ze ze angekuwa kituko kama angevurunda kwenye kiswahili, lakini kwa lugha ya watu mbona huyo ni shujaa tu maana ana uthubutu tena anapaswa kupigiwa makofi kama anavyoshangiliwa mzungu akiongea kiswahili broken.

Mambo ya kusifia sana lugha za kigeni ndio tunaambulia watu design ya mkalimani Matungwa, aliyekuwa anatupiga fix kwenye msiba wa Magufuli.
Putin haongei kingereza na mtu. Ukiongea naye lazima uongee lugha yake au uwe na mkalimani. Vile vile rais wa China, aliyekuwa chancellor wa Ujerumani Angela Merkel, rais wa Korea Kaskazini...
 
CCM badala ya kutuma ndege ziwafate raia wake huko Ukraine wao wametoa ka-barua eti kakutoa ushauri, ujanja ujanja tu kila kitu

Kwani walipelekwa na serikali?

Mbona hupigi kelele bibi yako akikwama kule Chitipa serikali ikamchukue au walio nje ni bora sana kuliko wa ndani?
 
Kiingereza cha watanzania wengi kinawasaidia na kinaishia kwenye kuandika status, kuelewa kilichoandikwa kwa kiingereza mfano magazetini na pale kinapotumika kuongea kwa kufatiliza maneno ambayo yameshaandikwa kwa mpangilio kwamfano kutoa hotuba kwa kufatiliza speech iliyochapishwa kwenye karatasi.

Ukija kwenye kiingereza cha kuwasiliana, wengi kusikia maneno na kuyaelewa inakuwa shida, pia kwenye kuongea kwa uhuru mfano kujielezea inakuwa kazi sana tofauti na pale wanaposoma speech, hapa panakuwa na ze ze ze izi izi izi zati.

Nakumbuka hata mwalimu wa kiingereza wa sekondari alikuwa haelewi chochote kwenye nyimbo za marekani zilizojaa matusi, hii ilikuwa mpaka chuoni wengi walikuwa hawaelewi kinachoimbwa zaidi ya ku enjoy biti, flow, kucheza pamoja na kuiga mtindo wa maisha ya wasanii hao wakidhani kwamba kinachoimbwa kina uzito kumbe ni uharo mtupu.

Pia watanzania huwa tunakosea sana tunapoona mtu kasoma speech kwa kiingereza na kumpongeza tukidhani anajua, LA HASHA!! huku ni kupotoshana, wa kupongezwa inabidi awe muandaaji alietumia utashi wake na muda mwingi kupangilia hayo maneno, kuanzia grammer, prepositions, n.k. maana bila hivyo hata huyo ambaye anafatiliza maneno hataweza, tukiachana na kiingereza cha kufatiliza maneno hicho, wengi wakiambiwa waongee kwa uhuru wa kutunga swntensi zake kichwani kama anavyoongea kiswahili, hapo inageuka kuwa aibu.hata mzungu ambae nae kiswahili kinampiga chenga akiandikiwa hotuba anaweza kuonekana anajua kiswahili.

Kwa watu maarufu wanaojua kiingereza kwa hapa Tz naweza kusema ni kina Vanessa mdee, Wema Sepetu, P Funk, n.k. hawa kidogo hata shule na maisba waliyokulia walikuwa exposed na lugha ya kiingereza katika maisba yao.

Pia nawakumbusha kujua kiingereza si9 kipimo cha akili.
Mkuu ulivyosema ni kweli kabisa. Mfano kuna Mtanzania mmoja alijitosa kwenye kipindi cha maoni kwenye channel ya Voice of America nimekisahau jina. Kwenye kipindi muandaaji anaalika watu studio na wengine wanaunganishwa kwa simu ili kujadili mada fulani iliyoandaliwa mfano EFFECTS OF COVID19 TO THE AFRICAN NATIONS. Kinafanana na HARD TALK cha BBC World service.
Mtanzania alipopewa nafasi ya kuchangia yaani haeleweki kabisa kuanzia kiingereza anachoongea hata mada yenyewe yaani kama haijui hata mada yenyewe .
Mtangazaji akampotezea akaendelea na wachangiaji wengine hadi mwisho wa kipindi. Yaani ni bora hakuwa studio sijui angesingizia nini ili aondoke asije akajikojolea. 😆😅😅
Sijui alikuwa anatafuta umaarufu kwa nini alikubali mwaliko huo?🤔🤔
 
Pia kulikuwa na mashindano ya Airtel ya vyuo mbali mbali nchi za Afrika.

Tanzania ilikuwa Vyuo kama Udsm vilikuwa vinagaragazwa hata na vyuo vya kati tena vya kilimo vya Malawi.

Maswali yanaulizwa vijana wetu wanabaki kushangaa tu, Wanaenguliwa haraka zile hatua za mwanzo kabisa, Chuo flani cha Arusha walikuwa wanachanganya na wakenya kidogo kilikuwa kinafikabali
 
Bahati mbaya akili ya kuwa kujua kiingereza ndiyo usomi haitakuja kuisha.
 
Hata Kiswahili cha Waingereza ni hivyo hivyo mkuu.
Kama wangesoma Kiswahili miaka 4 secondary zao

miaka miwili A level au Diploma kwa Kiswahili

chio kikuu miaka 3 hadi 5 kwa Kiswahili

jumla 4+2+3=9 miaka 9 kwa Kiswahili halafu wasijue inapaswa wachekwe.
 
CCM badala ya kutuma ndege ziwafate raia wake huko Ukraine wao wametoa ka-barua eti kakutoa ushauri, ujanja ujanja tu kila kitu
Mkuu hiyo ni ngumu kwasababu anga la Ukraine limeshakuwa chini ya Warusi, hivyo hiyo ndege wanaweza kuitungua kabla ya kutua.
 
Kumudu kuongea lugha ni confidence tu, Idd amin kiingereza chake kiliuwa kibovu hakuna mfano lakini alikuwa anaongea na confidence kibao na majigambo akienda huko uingereza na kupewa nafasi ya kuongea, kama wanamwelewa au la hilo halimsumbui, lakini yeye alijua anaongea ngeli.......
 
Nimependa jinsi ulivyo hitimisha. Ukipata muda sikiliza kiswahili cha Waingereza, lazima uvunjike mbavu kwa kicheko.
 
Hili tatizo langu kabisa, I've been working on it!, kwa cha kuandika unaeza feel nmesoma oxford
 
Back
Top Bottom