Kiingereza cha Watanzania wengi ni cha kuandika, kusoma na kuongea kwa kusoma maandishi. Tatizo ni kusikiliza, kuelewana na kuongea freely

Putin haongei kingereza na mtu. Ukiongea naye lazima uongee lugha yake au uwe na mkalimani. Vile vile rais wa China, aliyekuwa chancellor wa Ujerumani Angela Merkel, rais wa Korea Kaskazini...
 
CCM badala ya kutuma ndege ziwafate raia wake huko Ukraine wao wametoa ka-barua eti kakutoa ushauri, ujanja ujanja tu kila kitu

Kwani walipelekwa na serikali?

Mbona hupigi kelele bibi yako akikwama kule Chitipa serikali ikamchukue au walio nje ni bora sana kuliko wa ndani?
 
Mkuu ulivyosema ni kweli kabisa. Mfano kuna Mtanzania mmoja alijitosa kwenye kipindi cha maoni kwenye channel ya Voice of America nimekisahau jina. Kwenye kipindi muandaaji anaalika watu studio na wengine wanaunganishwa kwa simu ili kujadili mada fulani iliyoandaliwa mfano EFFECTS OF COVID19 TO THE AFRICAN NATIONS. Kinafanana na HARD TALK cha BBC World service.
Mtanzania alipopewa nafasi ya kuchangia yaani haeleweki kabisa kuanzia kiingereza anachoongea hata mada yenyewe yaani kama haijui hata mada yenyewe .
Mtangazaji akampotezea akaendelea na wachangiaji wengine hadi mwisho wa kipindi. Yaani ni bora hakuwa studio sijui angesingizia nini ili aondoke asije akajikojolea. 😆😅😅
Sijui alikuwa anatafuta umaarufu kwa nini alikubali mwaliko huo?🤔🤔
 
Pia kulikuwa na mashindano ya Airtel ya vyuo mbali mbali nchi za Afrika.

Tanzania ilikuwa Vyuo kama Udsm vilikuwa vinagaragazwa hata na vyuo vya kati tena vya kilimo vya Malawi.

Maswali yanaulizwa vijana wetu wanabaki kushangaa tu, Wanaenguliwa haraka zile hatua za mwanzo kabisa, Chuo flani cha Arusha walikuwa wanachanganya na wakenya kidogo kilikuwa kinafikabali
 
Bahati mbaya akili ya kuwa kujua kiingereza ndiyo usomi haitakuja kuisha.
 
Hata Kiswahili cha Waingereza ni hivyo hivyo mkuu.
Kama wangesoma Kiswahili miaka 4 secondary zao

miaka miwili A level au Diploma kwa Kiswahili

chio kikuu miaka 3 hadi 5 kwa Kiswahili

jumla 4+2+3=9 miaka 9 kwa Kiswahili halafu wasijue inapaswa wachekwe.
 
CCM badala ya kutuma ndege ziwafate raia wake huko Ukraine wao wametoa ka-barua eti kakutoa ushauri, ujanja ujanja tu kila kitu
Mkuu hiyo ni ngumu kwasababu anga la Ukraine limeshakuwa chini ya Warusi, hivyo hiyo ndege wanaweza kuitungua kabla ya kutua.
 
Kumudu kuongea lugha ni confidence tu, Idd amin kiingereza chake kiliuwa kibovu hakuna mfano lakini alikuwa anaongea na confidence kibao na majigambo akienda huko uingereza na kupewa nafasi ya kuongea, kama wanamwelewa au la hilo halimsumbui, lakini yeye alijua anaongea ngeli.......
 
Nimependa jinsi ulivyo hitimisha. Ukipata muda sikiliza kiswahili cha Waingereza, lazima uvunjike mbavu kwa kicheko.
 
Hili tatizo langu kabisa, I've been working on it!, kwa cha kuandika unaeza feel nmesoma oxford
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…