Kiini cha Falsafa, dini za Uislamu na Ukristu ni Afrika

Kiini cha Falsafa, dini za Uislamu na Ukristu ni Afrika

Mzee2000

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2009
Posts
528
Reaction score
221
Wandugu.

Katika topic hii nitathibitisha kuwa, kiini cha hizi dini ambazo waafrika wengi hasa hapa Tanzania na Afrika kwa ujumla tunazozifuata zina kiini Afrika. Kwa maana hii, namaanisha, waisraeli waligeza mawazo ya Mungu ya Afrika na kuyageuza kuwa mawazo yao na mwisho kuyageuza/ distortion mawazo yetu na kuturudishia sisi katika form ya ukristu/ uislamu.

Vilevile nitaongelea falsafa ya wagiriki na nitaonyesha kuwa kiini cha hii falsafa( kwa mfano aristotle, socrates) ni Afrika hasa ya weusi, hasa misri ya kale.

Nitakaribisha wasomi wote hasa wa falsafa kutoka seminari kwa mawazo yao.

Nitaendelea, Nakaribisha hoja.
 
mshana jr,

Nakubali kuwa materials(evidence) nyingi sana nimeikunja( condense) katika maneno mafupi niliyoandika hapo juu. Lakini topic ikizidi kuendelea ndio itakavyozidi kuonekana namaanisha nini.

naomba subira.
 
Last edited by a moderator:
Katika topic hii nitathibitisha kuwa, kiini cha hizi dini ambazo waafrika wengi hasa hapa Tanzania na Afrika kwa ujumla tunazozifuata zina kiini Afrika. Kwa maana hii, namaanisha, waisraeli waligeza mawazo ya Mungu ya Afrika na kuyageuza kuwa mawazo yao na mwisho kuyageuza/ distortion mawazo yetu na kuturudishia sisi katika form ya ukristu/ uislamu

Hivi unajua kuwa Wayahudi hawaukubali Ukristo?

Wayahudi na Uislam wapi na wapi?
 
Mzee2000,

Hata hueleweki, kwanza uko kundi gani? Realism, materialism au idealism?
 
Last edited by a moderator:
Wandugu,

Katika topic hii nitathibitisha kuwa, kiini cha hizi dini ambazo waafrika wengi hasa hapa Tanzania na Afrika kwa ujumla tunazozifuata zina kiini Afrika. Kwa maana hii, namaanisha, waisraeli waligeza mawazo ya Mungu ya Afrika na kuyageuza kuwa mawazo yao na mwisho kuyageuza/ distortion mawazo yetu na kuturudishia sisi katika form ya ukristu/ uislamu.

Neno la Mungu liko wazi. kugeza, kugeuza na blah blah nyingine unazoweka ni jinsi unavyotumia uhuru wako wa kuandika lakini cha msingi ni neno la nne la post yako. THIBITISHA.
 
Nakubali kuwa materials( evidence) nyingi sana nimeikunja( condense) katika maneno mafupi niliyoandika hapo juu.Lakini topic ikizidi kuendelea ndio itakavyozidi kuonekana namaanyisha nini.

naomba subira.

Topic ikiendelea? isipoendelea? kwanini kuja nusu nusu katika madai ambayo unadhani ni ya msingi? Atheists mnahangaika sana kwa kweli.
 
Mzee2000,

God is still a delusion, whether it originates from Afrika or Middle-East or Europe.

Yes, I would have preferred a black god, but he/she does not exist, anyway. Nevertheless, this could be a nice disccussion on the history of Ibrahimic religions and their relation to Afrikan belief systems.

Samahani wandugu nimeingiza Kinyamwezi, hii topic kwangu ngumu kwa kutumia kinyumbani (yaani Kiswahili).
 
Una hakika Mungu hayupo au unadhani hayupo?
 
Una hakika Mungu hayupo au unadhani hayupo?

Nina uhakika "a personal god" hayupo.

Yaani hivi, nina uhakika hamna mungu ambaye amekuwa defined na Waislamu, Wakristo, Wayahudi, au dini zote ambazo zina amini kuna jamaa uko mbinguni ambaye katuumba, anatupenda, atatuchukua, ata wathibiti walio mshiti, ana tulinda kupitia malaika, kaumba ulimwengu kwa siku s(?), anataka tumsujudu, kajiumba mwenyewe :A S 11:, n.k.

Now, do I know if the bigbang theory is 100%? Of course, NOT.

But, it is so far, the best explanation of our beginnings. It has many supporting evidences (such as back ground radiation being and the ratio of hydrogen to helium).

Do I think the evolution theory is true? YES, it has mountains of evidence and many practical application have been derived through our understanding and application of the theory.

As a free-thinking, non-mystical person, my interest and goals are to understand my existence to the best of my knowledge, while at the same time, acknowledge my limitation (or the limitation of our collective understanding as humans in this period). I am not interested in finding hope through false assumptions just to make me feel good. No, that is primitive. We now know that diseases are caused by virus, bacteria, and the likes, and not by a curse from the devil or god! It is a pity that some of us have not yet moved away from those primitive thoughts.

I know that, given the current progress of our scientific understanding, future generation will know more about our universe than what we know right now. Therefore, I don't see or feel the need to invoke superstitious ideas in order to explain the origin of the world or life!
 
Nina uhakika "a personal god" hayupo.

Yaani hivi, nina uhakika hamna mungu ambaye amekuwa defined na Waislamu, Wakristo, Wayahudi, au dini zote ambazo zina amini kuna jamaa uko mbinguni ambaye katuumba, anatupenda, atatuchukua, ata wathibiti walio mshiti, ana tulinda kupitia malaika, kaumba ulimwengu kwa siku s(?), anataka tumsujudu, kajiumba mwenyewe :A S 11:, n.k.

Acha maneno mengi niwekee ushahidi hapa kuwa hayupo ...!!
 
Samahani wandugu nimeingiza Kinyamwezi, hii topic kwangu ngumu kwa kutumia kinyumbani (yaani Kiswahili).
PlanckScale,

Huu ni ufinyu tu wa fikra kama kigezo cha lugha kinakutoa nje utawezaje kudadavua hoja za kiundani?

Je hicho kinyamwezi chako kinajitosheleza kichwani kwako? Je,hicho kinyamwezi chako kinatosheleza kuelezea dhana za kiimani na kihistoria kutoka katika muktadha wa kiafrika, kiarabu, kigiriki, kiebrania, kimharaki, kilatin na kimisri?

Lugha ya mkopo haiwezi kukutosheleza aidha, hakuna lugha inayoshindwa kuelezea dhana" concept" za lugha nyingine. Na ndio maana utamaduni wa kiafrika au kihindi(mf.Kigujarati) unaweza elezwa kwa kiingereza japo waingereza hawana msamiati kwa kila neno na dhana ya kiafrika au kihindi.

Wewe ulipaswa useme hivi kwa kuwa suala ninaloenda kulijadili ni pana nitalazimika kuchanganya msimbo. Hili ni jambo la kawaida katika lugha, je hivi unajua kwamba % 40 ya maneno ya kiingereza yamekopwa na kutohorewa kutoka kifaransa? Je unajua kwamba maneno ya kisayansi takribani % 80 katika kiingereza yanatokana na kigiriki na kilatini? Ndivyo kwa kijapan, kichina, kirusi nk.

Hivyo basi, ukitumia lugha ya kiswahili kujadili mada yako huku ukitupia maneno ya kirejista na kiistilahi utakuwa unaikuza lugha ya kiswahili.
 
Last edited by a moderator:
Wandugu,

Katika topic hii nitathibitisha kuwa, kiini cha hizi dini ambazo waafrika wengi hasa hapa Tanzania na Afrika kwa ujumla tunazozifuata zina kiini Afrika. Kwa maana hii, namaanisha, waisraeli waligeza mawazo ya Mungu ya Afrika na kuyageuza kuwa mawazo yao na mwisho kuyageuza/ distortion mawazo yetu na kuturudishia sisi katika form ya ukristu/ uislamu.
Embu thibitisha hiyo kitu!

Vilevile nitaongelea falsafa ya wagiriki na nitaonyesha kuwa kiini cha hii falsafa( kwa mfano aristotle, socrates) ni Afrika hasa ya weusi, hasa misri ya kale.

Sikutambua kuwa misri ya kale ilikuwa na watu weusi. Jee watu hao waliishia wapi?

Nitakaribisha wasomi wote hasa wa falsafa kutoka seminari kwa mawazo yao.

Nitaendelea, Nakaribisha hoja.

1 Ivi unamanisha source ya imani ya uwepo wa Mungu ilianza kwa waafrika weusi?

2 Ni waafrika wa nchi gani waliotoa hiyo falsafa iliyorudishwa ktk form ya ukiristo na uislamu?

3 Kwanini waafrika hao walikuwa na imani hiyo?

4 Jee imani hiyo ilitoka vipi kwa wafrika weusi na ilirudishwa vipi katika form ya ukiristo na uislamu?

5 Na jee vile vitabu (bible na quran) viliandikwa na nani?
...
Naomba unijibu maswali hayo kwa kuzingatia namba.

Naomba unipe na miaka kwa kila epoch utakayoelezea.
 
Back
Top Bottom