Mzee2000 kwanza hongera kwa mada nzuri inayo fikirisha na kupanua akili!
Swali langu kwako ni;je unatambua ya kuwa utaratibu wa kutahiri haukuanza kwa moses bali kawa ibrahim kwa upande wa kimaandiko,hii ikijumuisha wayahudi(maana ibrahim ni babu wa moses,kwamba yeye ni way back before moses?.HOJA YANGU ni je hapa unaweza vp kutrace utaratibu huu kama ni asili ya Misri kwa kupitia moses ili hali kabla yake yeye ibrahim alisha ongozwa kufanya tena eneo tofauti na misri?
Hongera kwa mada nzuri!.Nawasilisha!
Ahsante kwa swali lako, ni kweli kabla ya Moses waisraeli walitahiri kuanzia enzi za Ambraham, lakini ukiangalia amri kumi za Mungu na taifa la Israel chanzo kikuu cha sheria zao ni Moses, na huyu ni nabii muhimu wa Judaism, na alikulia Misri.Vilevile Abraham anasemwa kwamba aliishi Misri wakati kuna njaa Canaan, kwa hiyo alikuwa esposed na mila za wamisri.Vilevile wakati Abraham anaishi ( hapa tuna-assume alikuwa real historical character) wamisri/ waafrika walikuwa washaanza kutahiri. Kwa kufafanua:
1) Wataalamu wa timeline ya biblia, wanakubaliana kuwa historia ya agano la kale sanasana kuhusu Abraham iliandikwa takriban
500BC. Kwa kupiga mahesabu nyuma vizazi/matukio vilivyoandikwa kwenye bible,( wanasayansi kwa kulinganisha na sayansi ya archeology na rekodi nyingine) hayaendi zaidi ya
2000BC ( at the latest). Wayahudi hawakuwa literate( hawakuweza kuandika) kabla ya huo mwaka (500BC) kwa hiyo yaliyoandikwa ni ‘oral traditions' za zamani za wayahudi. Sasa wamisri wa kale walikuwa ‘literate' miaka mingi sana nyuma, yaani walianza kuandika historia yao
kuanzia 3100BC ( kumbuka alfabeti tunayoitumia sasa hivi chanzo chake Misri).Na Katika historia yao iliyoko kwenye maandishi( na miili yao ) inaonyesha kuwa walifanya circumcision kabla hata ya Abraham yaani kabla 2000BC. Kwa kifupi, wamisri walikuwa ni ‘wazee' zaidi ya nabii yoyote yule wa waisraeli.
2) Waisraeli/ watu wa mashariki ya kati( middle east) walikuwa na mawasiliano mara nyingi na wamisri, wengine waliishi huko kama wafanyakazi/wavamizi. Kumbuka Misri ya kale ilikuwa empire kubwa sana yenye utajiri mwingi na kuna wakati ilitawala karibu maeneo yote ya Middle east, hata mpaka ugiriki, kwahiyo inawezekana walisambazo mila za kutahiri kama jinsi Herodotus alivyoandika kwenye post yangu hapo juu.
3) Angalia vilevile na sababu zinayotolewa na makabila ya Kiafrika kuhalalisha Kutahiri. Ukiangalia argument ya waafrika inaenda sana kiundani zaidi ya waisrel ambao wanasema tu ‘Mungu ametuambia'. Circumcission ya kiafrika inafanywa kwa sababu nyingi zikiwemo, kumfanya kijana kuingia kwenye uanaume. Zaidi, katika Afrika yako makabila yanayotahiri hata wanawake, na hii kitu huwezi kuona middle east. Kwa hiyo kutahiri Afrika kuko very DIVERSE/ DEEPER kimaumbile na kisababu ( justification) kuliko middle east na hu ni uthibitisho tosha kuwa waisraeli walijifunza hii mila kutoka kwa wamisri/ waafrika.
Kama hakuna maswali mengine nitaendelea na mada.