Mkuu
Mzee2000 nimesoma post zako lakini napata kuona ya kwamba unajaribu sana kulazimisha jambo ambalo halilazimiki.
Kuna makabila zaidi ya 200 Afrika, sasa eti kwa sababu kati ya hayo kuna ambayo wanatahiri na hivyo basi Moses na Abraham kuiga hio tamaduni ya kutahiri basi kunaufanya Uyahudi kuwa na source ya Black Africans pamoja na Ukristo na Uislam is a very very far fetched idea.
Ni sawa na mtu aje aseme chimbuko la kingereza ni kiswahili sababu kwenye kingereza kuna neno "safari".
Sijui ni kwanini unataka kufanya kuwa hizi dini kuu zina originate kutoka black africans wakati vitabu vyao wenyewe havisemi hivyo na hakuna imani hata moja ya kiafrika yenye kufanana na Abrahamic religion yeyote ukiachilia mbali swala la kutahiri ambalo katika makundi hayo linabeba maana tofauti kabisa kama wewe mwenyewe ulivosema.
Kwa WaAfrika ni initiation process ya kuashiria mtoto kuwa mwanaume na kwa waYahudi waliambiwa ni ishara ya kuwatofautisha wao na gentiles.
Ni kweli historia kama ilivyoandikwa na watu wengine imekandamiza sehemu ya mwafrika lakini hii imefanya baadhi ya waAfrika kudai vitu ambavyo kwa kweli ni a stretch of the imagination sana.
Kama hili nalo ni a strech of the imagination to the limits of elasticity. Sisi waAfrika imani zetu sio monothiest, sio za kuamini Mungu mmoja bali imani zetu ni za kuamini miungu wengi kama wahindi, wachina na hata hao ma Pharaoh.
Sasa inashangaza kuwa imani ambazo msingi wake ni miungu wengi ndio ziwe chimbuko la imani za Mungu mmoja.
Halafu hoja yako unaanza kuijenga kwenye fallacy. Yani msingi wa hoja yako yenyewe ni wa mashaka sana. Maana ili ikubalike kuwa chimbuka la Abrahamic religion ni black African religions inabidi kwanza tukubali kuwa ma Pharaoh na ancient Egyptians were black people.
Kwanza mimi namashaka na proof zenyewe ila hata kama zipo kuwepo kwa watu weusi hapa africa kuna maanisha ndio walikua waafrika hawa kama walivyo wa sasa kusini mwa sahara?
Swala la Pharaohs kuwa black africans nalo ni debatable, halafu kumbuka kuwa tunaongelea rangi ya ngozi au originality? Maana hapo kati kuna persians,arabs na wahindi weusi sana lakini sio bantus.
Unajaribu pia kuwaleta wa Ethiopia katika equation ili kujaribu kulink muafrika mweusi na Abrahamic religion. Lakini ndugu a xhosa from south africa na a shona from hapo zimbabwe wako sooo unrelated na mu ethiopia ambaye yuko karibu zaidi na wayahudi na persians.
Kwahio, hapana mwafrika mweusi kama tumjuavyo leo alishapoteza kwa kiasi kikubwa tamaduni zake, unachokifanya hapa ni kujenga a false premise ambayo badala ya kujenga inatupotezea zaidi vizazi vyetu vijavyo.
Hivyo basi mimi binafsi mpaka hapo ulipofikia sijaweza kushawishika ya kwamba kiini cha Uislam na Ukristo ni Black Africans (Bantus) kama tuwajuavyo leo! Ancient Egyptians, Ethiopians wana undugu zaidi kivyao kuliko watu weusi wa west africa, central africa na south. Hatuna chetu humo, una force.