Kiini cha matatizo ya Zanzibar, Mapinduzi ya mwaka yaliyomwondoa Sultani

FNyie watoto wa juzi hamuoni historia kwa kutambua kuwa waliouliwa kabla ya mapinduxi walikuwa wengi zaidi ya unavyofikiri.
Na hilo ndo tatizo kubwa la Zanzibar, kuondoa tofauti baina ya pande hizi mbili ni ngumu sana maana zimejengeka karne na karne.
Habari nyingine mwajichotea vijiweni, nendeni Zanzibar mukaishi ile hali halisi muone msuguano huo wa chini kwa chini.
 
Maalim Seif Sharif Hamad yupo kundi katika hayo matatu?

Maalim Seif ni mshirazi, nusu mwarabu na nusu mwafrika.. ila hawa waShiraz kuna ambao wako kiarabu zaidi na ambao wako kiafrika zaidi, inategemeana na jinsi alivyolelewa na hurka zake.
 

Wanaogopa kumtangaza maalim seif kwa sabbu wanajuwa wazi maalim atakata mirija yote ya kinyonyaji iliyowekwa na mkoloni mweusi zidi ya wananchi wa zanzibr,haiwezekani kwa nchi moja kuipora kijeshi nchi nyengine mamlaka yake ya kujiamulia,hakuna neno zaid ya udikteta tu.
 
Last edited by a moderator:

Msikae makadanganya watu.. hakuna mtoto tena hapa wa kudanganyika. kizazi cha sasa cha wazanzibari (vijana) hawana habari kabisa na unachokiongea na ndio wapiga kura waliowengi ni wao na ndio waliochagua upinzani.

Mimi ni mzanzibari wazee wangu walikuwa wakubwa serikalini na mimi na wengine kama mimi tulichagua CUF au niseme mabadiliko. wazanzibari ni wamechoshwa na hali ya kiuchumi na ukandamizaji ndani ya nchi yao, hawana mahakama, hawana polisi hawana matibabu, hawana.......

Kitendo cha kuwanyima haki yao ya kidemokrasia halafu mkasingizia kisingizio cha kihistoria ni kupotezeana muda. Acheni kudanganya uma kwa kueneza propaganda chafu kwa sasa haina nafasi tena imeshapitwa na wakati.


kwa ufupi CCM hakuna tena Zanzibar .. hata hayo majimbo mulioyaiba kama itatokea ukifanywa uchaguzi ulio huru na wa haki basi Wallah hamuyapati.

Cha muhimu kwa sasa ni kuheshimu matwakwa ya wazanzibari na si vyenginevyo. Mukae mkijua kwamba hamna ujanja tena is just a matter of time kila mchumia tumbo mtatafuta pa kukimbilia.
 

Kwanza mimi si mtoto. Pili acha kuhamaki, ukitaka kujifunza nenda taratibu.

Nchi nyingi si Zanzibar tu zimepitia migawanyiko, zimeponya majeraha na sasa zinakwenda mbele.

Kuongelea habari za kurudi Sultan ni kichekesho cha karne. Hayo ni maneno ya vitisho waliyokuwa wanapewa Wananchi na "class mpya ya watawala weusi" (najua hujui hili, unajua class ya Sultan na Mwarabu). Leo hii wengi wanaona kama geresha tu za Kisiasa japo wapo wenye fikra kama zako.

Na mfano ni namna Seif anavyozidi kupenya Unguja tofauti na mazoea.

Ulisema kulikuwa na mauaji makubwa kabla ya mapinduzi? Tupe reference kidogo ambazo zimekuwa documented (si stori za vijiweni)
 
ASP au Wabara ndo waloshika mpini ? hao sawa na Buthelezi aliekubali Bantunstan ili awe mfalme wa wazungu. au Abdel Muzorewa wa Zimbabwe alie wekwa na Ian smith atawale. hao ni sawa na hawa wazanzibari halisi hawataki ujinga wa kutawaliwa.
usultani zaidi ya huu wa ccm upi tena mwengine?
 
Nimekusoma katika comment zako kwenye hii thread nikagundua unajichanganya sana kihoja au unatumia unafiki katika kujenga hoja.

Mara unasema Wazanzibari ni wamoja, hapo hapo tena unadai kina balozi Seif iddi, hassan mitawi, hamza ni wavamizi wa Zanzibar na pia ni ajent wa mkoloni mweusi. Huyu mkoloni mweusi hujasema ni nani?
 

Ww pumbaa kbs unataka tuendeleee kutawaliwa na hawa wakolon weuc sio
 
Waliompa kura Rais Shein ni watu wa wapi?
 
CCM bhana.

Zanzibar hakuna tatizo ulilolieleza kweye mada yako.
Hii ni propaganda ya CCM ili iendelee na mchezo mchafu; kubaka demokrasia na kung'ang'ania madaraka.

Kama utakuwa mkweli na si mnafiki, tatizo la Zanzibar ni CCM kutoheshimu maamuzi ya wapiga kura na propaganda chafu ya sultani atarudi ikiwa CUF itachukua madaraka.
Tatizo jengine ambalo Nyani Ngabu ameliona hapa Tanzania ni upoyoyo wa wananchi. CCM na serikali zake wanatumia upoyoyo huo wa wananchi na vyombo vya dola kung'angania madaraka.

Kwa kweli hakukua na sababu ya kuwepo mkwamo Zanzibar kwa sababu umeshataja hapo kuwa Zanzibar ni lazima waunde serikali ya umoja wa kitaifa. Ni takwa la kikatiba.

CCM waache kung'ang'ania madaraka, ZEC inajua ni nani ameshinda, watangaze matokeo yaliyobakia na mshindi aapishwe aunde serikali na shughuli za maisha ziendelee.

Tume ZEC ikimalizia kutangaza matokeo ya majimbo yaliyobakia au isitangaze. Matokeo yanajulikana tayari kwa sababu yalishatangazwa majimboni na kubandikwa ukutani na wasimamizi wa majimbo.

CCM ndio watavuruga amani ya nchi hii.

Magufuli angekuwa mnufaika mkubwa wa siasa kwa kipindi hiki kama Zanzibar ikiongozwa na Chama cha upinzani. Tawala zote zitataka kujikita katika mikakati kuleta maendeleo na kukuza uchumi. Mashindano ya kiuchumi na kuinua hali za maisha ya walalahoi.

Acha propanganda chafu na za kijinga, ambia Chama chako kiachane na ulafi na ung'ang'anizi wa madaraka au kifute mfumo wa vyama vingi kama haina nia ya kuachia madaraka inaposhindwa kupitia kisanduku cha kura.

Wewe huna tofauti na Lukuvi.

 
Last edited by a moderator:
boya tu wewe hujui historia ya zanzibar na mapinduzi yalivyotokea
uliza ufahamishwe
 

mapinduzi yalikuwa ya uvamizi ya visiwa vya zanzibar wazanzibari wote walikuwa kitu kimoja
kuanzia wale wenye asili za warabu, waafrika na wahindi walikuwa wanaishi vizuri tu na kupendana mpaka watu wenye chuki na wazanzibari ndio wakaleta fitna zao na kuupoteza uhuru wa zanzibar wa 1963.......waliofanya mauwaji na kuwakamata wanawake wa kizanzibari kwa nguvu wote walikuwa ni wageni sio wazanzibari
 
Hapa bado tunao uunguja na upemba, angalau tungefanya ari tukaacha kuijengea tanganyika tukaboresha huko kwetu pemba, hili ni tatizo
 



WALIPOTEA KI VIPI HAWA WANA MAPINDUZI? WAZANZIBARI WALIOKUWA WASOMI MIAKA ILE WALIPOTAKA KULETA MAENDELEO NA UTAWALA BORA KWA NCHI YAO JAMHURI YA WATU WAZANZIBAR...NINI KILIWAFIKA?
 

Attachments

  • BRZ.jpg
    24.1 KB · Views: 514
WALIPOTEA KI VIPI HAWA WANA MAPINDUZI? WAZANZIBARI WALIOKUWA WASOMI MIAKA ILE WALIPOTAKA KULETA MAENDELEO NA UTAWALA BORA KWA NCHI YAO JAMHURI YA WATU WAZANZIBAR...NINI KILIWAFIKA?


Pichani ni Baraza la Mawaziri la mwanzo la Jamhuri ya Watu wa Zanzibar likiwa pamoja katika jumba la Beit el-Ajaib tarehe 13 Januari, 1964, siku chache baada ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Kutoka kushoto kwenda kulia ni Abdulaziz Twala (Msaidizi Waziri katika Ofisi ya Rais), Aboud Jumbe (Waziri wa Siha na Majumba), Hasnu Makame (Waziri wa Fedha na Maendeleo), Othman Shariff (Waziri wa Elimu na Mila), Abdulrahman Babu (Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara), Abeid Karume (Rais wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar), Abdallah Kassim Hanga (Makamu wa Rais), Saleh Saadalla (Waziri wa Kilimo), Idris Abdul Wakil (Waziri wa Kazi, Njia na Nguvu za Umeme) na Hassan Nassor Moyo (Msaidizi Waziri wa Kazi, Njia na Nguvu za Umeme) ZANZIBAR

 

Sasa chaguzi ni za nini kama tayari maamuzi ya nani atawale yalishamalizwa ??????????!!
 


asante sana mkuu!!
 
Last edited by a moderator:
Maalim Seif ni mshirazi, nusu mwarabu na nusu mwafrika.. ila hawa waShiraz kuna ambao wako kiarabu zaidi na ambao wako kiafrika zaidi, inategemeana na jinsi alivyolelewa na hurka zake.

Washirazi ni waajemi kutoka Iran hawahusiani na waarabu,hadi Leo kuna mji unaitwa Shiraz huko Iran,ndiko asili ya washirazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…