Kiini cha matatizo ya Zanzibar, Mapinduzi ya mwaka yaliyomwondoa Sultani


You are a stupid man with a long and windy foul tale which your low thinkig capacity cannot make sense out of it all.

So stupid that you might as well finish the tale by explaining the deep love for slavery that prompted the 1964 mapinduzi tea party.

Your billowing of hot foul air aint making it.
 
Mister dont waste your time arguing with a peanut brained punjabi!
 
Ccm wakishindwa uchaguzi wanaleta story za ubaguzi.
 
Hapo hakuna Mzanzibari wote kutoka bagamoyo na Uganda, kama unataka kujua siri ya mapinduzi soma kitabu cha kwa heri ukoloni
Ni hivyo atiiii.... na waliotoka Oman vipii???
 
Unakuja kuja lakini bandiko lako ndio linapalilia mgawanyiko zaidi!
Mkuu inbidi pawepo na msimamo tofauti pande zote juu ya kutatua matatizo ya kimsingi yaliyotokana na matukio ya 1964.
Yale ya 1964, yalikuwa na umuhimu wa kutokea lakini sasa mazingara yako tofauti na kuna haja ya pande zote kukubali hilo.

Kuna ambao wala hawaji kilitokea nini, hata huko Zenj, na kuna walioathirika kifamilia na kisaikolojia, na kuna waliopata unafuu wa maisha kwa yaliyotokea.
Na wote wako zizi moja.

Ndio maana nasema juhudi kubwa zaidi ifanyike , kwanza kukubali yaliyotokea, pili kuondoa hali ya uhasama wa kihistoria ambao hadi leo upo, na tatu kuwaondoa watu katika hali ya kuweka msimamo ya kisiasa na kujikita katika kuondoa umasikini na kufanya kazi kwa bidii Zaidi.

Mtu akiwa na maisha bora, hata siasa zinakuwa only a 2nd option.
 

Nakubaliana na wewe
 
Hawa watu hata ukiwafahamisha kwa bunduki hawafahamu! Tokea lini Zanzibar na mfaranyaki, natepe!!!!??? Hapo hakuna hata mmoja mzanzibar original.
Umeulizwa tena na tena, muzanzibari orijino kwako wewe ni yule toka Omani?
 

Kiini cha matatizo ya Zanzibar, ni CCM kung'ng'ania madaraka wakati hawatakiwi na wazanzibari waliowengi. Wazanzibari wanaotaka mamlaka kamili ya nchi yao. CCM pamoja na kushikilia dola kwa hisani ya CCM Tanganyika haina wafuasi wengi na ndio maana Dr. Shein amepitwa kwa zaidi kura 25,000 na maalim Seif.

Vile vile ni kweli kuwa kwa sasa waliowengi wanaoiunga mkono CUF ni wale waliopinduliwa ( washiraz) na wanaoiunga mkono CCM ni waafrika wenye asili ya bara walioipindua serikali halali ya Muhammed Shamte. mshirazi/mswahili wa Pemba.
usipoteshe watu iliopinduliwa ni serikali halalI ya muuungano wa vyama viwili ZNP/ZPPP vilivyoshinda uchaguzi na kuongozwa na Wazari Mkuu Muhammed Shamte na si Sultani. Sultani alikuwa hana mamlaka ya uongozi wala bendera ya Zanzibar. Waliopindua si wazanzibari, bali ni Mganda John Okello na kusaidiana na wakata mkonge wa Tanga na wamakonde.Ndio maana yalitokea mauaji ya kiimbari kwa vile wauaji walikuwa hawana ndugu wala familia.
 
Ubaguzi ndo unawamaliza.
Sasa kama walipindua waafrika toka bara, na nyie wa Omani mlitoka wapi?
Maana huku si kwenu!
 
divide and conquer,ndio sera iliyofeli zanzibar,hakuna kabila la wapemba wala waunguja,pemba na unguja ni visiwa vyenye watu wa makabila yote ya zanzibar,lakini mkoloni ni mkoloni tu hawezi kushindwa kuwagawa watu,ndio maana watu wa bara wanachanginyikiwa vp mwanamapinduzi kindakindaki nasoro moyo yupo na maalim seif,mansour himidi mtoto wa brigedia yusuf himidi comrade wa nasoro moyo,yupo na maalim seif,amani karume,fatma karume,eddy riyami,ismail jusa babu duni mtoto wa dadake komandoo salmin amour naweza kuandika kitabu HUO UBAGUZI HIYO HISTORIA IKO WAPI YA KUHALALISHA KUFUTA MAMLAKA YA WANANCHI KUCHAGUA MUSTAKBALI WAO?
 
Umeulizwa tena na tena, muzanzibari orijino kwako wewe ni yule toka Omani?

Historia inatuonyesha wageni wa kwanza kukanyaga Zanzibar (Waarabu) waliwakuta wenyeji wa asili wa visiwa vya Zanzibar na hata huyo mkoloni wa kwanza kuitawala Zanzibar (Mreno) aliwakuta wenyeji wa asili wa Zanzibar.

Hizo habari zenu za kuwa wazanzibar wanaasili ya Tanganyika na wameletwa Zanzibar na waarabu wakati wa utumwa tunawaachia wenyewe! Lakini ukweli Zanzibar inao watu wake wa asili ya visiwa na miongoni mwao ni watumbatu, wakojani na wengineo wengi wenye asili ya Pemba na Unguja.

Muomani hawezi kuwa mzanzibar wala mzanzibar hawezi kuwa muomani.
 
Hujajibu swali!
Kama mu Omani ni wa kuja, nani mwenye haki zaidi ya uzalendo wa ki Unguja?
 

Hiyo -ekundu ndio ambayo CCM imeshindwa kufanya kwa miongo 5. Sasa ikae pembeni tuone kama CUF itaweza kutekeleza ahadi walizotoa. CUF wameweza kuwashawishi wapiga kura huko kuwa wao wataweza kuleta maisha bora. Umeshasema watu wakiwa na maisha bora, siasa wataweka pembeni. Kwa hiyo CCM imekuwa ndio kikwazo cha kufikia maisha bora.Waache kung'ang'ania madaraka. Wakubali nchi isonge mbele. CCM- Zanzibar wajifunze kutoka kwa Jonathan wa Nigeria, wajifunze kutoka Myanmar na wajifunze kutoka Argentina. Hizo nchi zimefanya uchaguzi na wapinzani wameshinda na waliokuwa madarakani wamekubali kushindwa na kuacha utawala mpya kuchukua nafasi yake.

Link Myanmar's 2015 general elections explained - BBC News

Link2. Mauricio Macri is elected Argentina's next president: 2015 Argentine presidential election second-round result | The Economist


 
Last edited by a moderator:

Umemsifia huyo bwana lkn nyote katika historia ya Zanzibar ni mbumbumbu,hakuna mnalojua!
Huwezi kuiongelea historia kwa kuangalia mwisho wake na kuacha mwanzo na katikati!
Historia ya Zanzibar inaanzia mbali kabla hata ya huyo Sultani. Hebu rudini darasani kidogo! Someni historia ya Zanzibar vizuri kisha ndo mje hapa kujambajamba!
 
Hapa watu hawaelewi hata wanaongelea nini! Mtoa mada kakwepa kusema ukweli kwamba kinachoendela Zanzibar ni kundi la watu wachache kukatalia madarakani na wapo tayari kwa lolote!
Huwezi kusema mgogolo wa Zanzibar chimbuko lake ni Mapinduzi ya Sultani wa Zanzibar mwaka 1964! Huyo mama unaemsemea na matamshi yake ya kijinga pale Dodoma hata hawajui walioshiriki Mapinduzi.
Ukweli ni kwamba hata hao ASP wengi wao hawakuelewa mipango ya Mapinduzi ilianza lini. Ni Chama cha Umma ndicho kilichokuwa kinaongoza mipango ya Mapinduzi kwa kuwashirikisha vijana wachache wa ASP wakati huo. Hili linahitaji muda kulielezea!
Huwezi kutenda haki kwa kuiongelea historia ya Zanzibar kwa kuanzia na Mapinduzi. Historia ya Zanzibar ni ndefu. Wala sio sahihi kuongelea historia mwishoni na kuacha mwanzo wake ama katikati!
Kinachoendelea leo Zanzibar ni matokeo ya ulafi wa madaraka na sio kitu kingine! Ndani yake bado kuna mapambano ya uhuru wa kweli ambao Wazanzibar wanadai umepokwa na ndugu zao wa Tanganyika! Waasisi wa CUF ni watu waliokuwa viongozi ndani ya CCM na Taifa kwa ujumla. Hawa waliondoka CCM kutokana na misimamo yao juu ya haki na uhuru wa Zanzibar! Walikubali kupoteza uongozi na starehe za muda ili kuitafutia Zanzibar uhuru wake. Sio kweli kwamba wanatumiwa na Waarabu. Jiulize Mzee Jumbe alitumiwa na Waarabu? Yupo wapi leo? Kosa lake ni lipi? Huko Unguja mwaka huu wa uchaguzi CCM imekataliwa na Wazanzibar kama ilivyokuwa Pemba, jiulize sababu ni zipi?
Kuna watu wanakatalia madarakani kwa nguvu kwa kisingizio dhaifu cha Mapinduzi wakati hata hawawajui waasisi wa Mapinduzi. Na hata kama wanawajua, mpaka leo hii hawataki kuwakubali! Tatizo ni uroho wa Madaraka!
Wanaosema Wapemba wanataka sultani arudi,mbona hajarudi huyo Sultani kwenye uongozi wa Dr. Shein ambaye ni Mpemba?? Karume alipokubali kushirikiana na CUF nae alitaka Waarabu warudi Zanzibar???
Tukubali ukweli,kuna tatizo katika Muungano na wenzetu sasa wanataka suluhisho! Kuichagua CUF ni njia ya kutafuta uhuru wao kama Taifa!
Nina amini hata uchaguzi ukirudiwa leo na kukawa na usimamizi wa haki,CCM itashindwa vibaya zaidi Zanzibar!
 
Sasa wewe unaijua historia ya Zanzibar vizuri mbona hushiriki kutatua matatizo yake huko huko kwenu.
Siyo siri wazanzibari kwa midomo na kuongelea matatixo hamjambo, kimbembe ni akili ya kuyatatus hayo matatixo.

Kila anayeongekea utatuzi anaruka kama mmanga na kurushia Tanzania Bara utafikiri suala halimhusu!
Watu wanaendekea kuishi katika vibanda na hawafanyi kazi ya maana kutwa kunywa gahwa na kupiga stori.

Na ukimwuliza kwanini hafanyi kazi ati jibu yake hiyo ni kero ya muungano.
Kwa kupenda kubebwa kama mabebi hamjambo.

Sasa maalim tumia historia yako ili upande mikarafuu zaidi na uache kuagiza maboga, mchele , nyama na kuku toka Bara .
Hapo tutakuelewa kuwa kwa historia uliyo nayo, umeamua kujitegemea na kwuka utu wako mbele.
Ukiwa tegemezi kwa watu masikini vile vile wa Tanganyika, hueleweki ilhali una akili, siha njema na ardhi nzuri tu ya kuendeleza watu wenu.
 
Mkuu ukipenda kubebwabebwa hata iwe vipi, wewe ni masikini tu, na hilo ni mpaka uamue kuondokana na fikra ya kuishi kiutegemezi kwa watu masikini wa Bara.
Limeni, wekezeni, fanyeni kazi.
Mbaya zaidi hata viongozi wenu mambo yakiwaenda vizuri wanajenga DSM badala ya kwao, balaa tupu.
 

Ngozimbili,
Napenda kukuunga mkono kuhusu historia ya Zanzibar.

Wengi hawaijui vyema historia ya Zanzibar pamoja na Mapinduzi ya Zanzibar.

Kutoijua historia ya Zanzibar kunakwenda hata kwa viongozi wetu wa juu na
ndiyo maana utasikia wanasema maneno ambayo huwashangaza Wazanzibari
wenyewe na kujiuliza kama kweli hawa viongozi wanaizungumza Zanzibar au
nchi nyingine.

Naweka hapa chini barua aliyoniletea rafiki yangu mmoja Mzanzibari akieleza
hali ya Zanzibar ilivyo:

''Hawa wenye siasa kali za kigozi (kibaguzi) za kuwaangalia watu kwa rangi
zao na asili zao hapana shaka hawawajui Wazanzibari walivyo.

Sielewi mtu anazungumza nini anapotaja "Black Africans" yaani "Waafrika
Weusi" kukhusiana na Zanzibar!

Bora nitoe mifano michache asaa wakatuelewa Wazanzibari tulivyo.

Nadhani kwa hawa magozi, mtu kama hayati Mhishimiwa Abedi Amani
Karume
ni mfano mzuri kwao wa "Black African" kwani alitoka bara na kuja
Zanzibar.

Lakini, ikisha baada ya hapo alifanya nini ili watoto wake wabakie kuwa
"Waafrika Weusi?"

Jawabu ni kuwa: alimwoa mwanamke wa Kizanzibari ambaye kwa aliye gozi
hatamkubali Bi. Fatma kuwa ni "Mwafrika Mweusi" mwenziwe, kwani rangi
yake Bi. Fatma si ya "Mwafrika Mweusi" kwa mujibu wa fikra za aliye gozi.

Tusisite hapo; tuje kwa wanawe Wahishimiwa Amani na Ali Karume.
Wote wawili wamewaoa Wazanzibari wenzao lakini wenye asili za Kiarabu.

Tusisite hapo, tuje sasa kwa wajukuu wa hayati Mhishimiwa Abedi Karume,
utakuta mpaka Mzungu ameolewa nao.

Tusisite hapo, sasa angalia wake wa wahishimiwa wengi pia.

Mfano mzurini wa hayati Brigadier Yusuf Himid ambaye alimwoa Bi. Fatma
Jinja
ambaye ni Mwarabu aliyechanganya nasaba; huyu ni mama yake mzazi
Mhishimiwa Mansour Yussuf Himid.

Aliwaoa pia na wanawake wengine wenye asili za Kiarabu.

Tusisite hapo; tuje sasa kwa aila ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha
Afro-Shirazi, hayati Mhishimiwa Thabit Kombo Jecha.

Naye alimwoa pia Mzanzibari mwenye asili ya Kihindi na kumzaa Mhishimiwa
Mahmoud Thabit Kombo.


Mhishimiwa Mtoro Rehani Kingo, mwenye asili ya bara, ambaye alikuwa
Mhariri wa gazeti liitwalo Afrika Kwetu (gazeti ambalo lilikuwa sauti ya Chama
cha Waafrika kukhusu siasa za Zanzibar tokea miaka ya 1950), baadaye alikuwa
pia Mkuu wa Chama cha Afro-Shirazi, na bada ya hapo akawa Memba wa Braza
la Mapinduzi (MBM), naye huyu pia alimwoa bibi wa Kiarabu aitwaye Fatma
Mbarak
.

Mhishimiwa Said wa Shoto naye pia alikuwa Memba wa Baraza la Mapinduzi la
mwanzo, ni Myamwezi kutoka Tanganyika; alikuwa akitisha sana kwa vitendo
alivyowafanzia Wazanzibari, naye alimwoa mwanamke wa Kiarabu aitwaye
Saada "Mgeni" Mbarak Al-Alawy.

Mhishimiwa Said Ali Bavuai alikuwa pia Memba wa Baraza la Mapinduzi,
naye pia alimwoa msichana wa Kiarabu aitwaye Fawziya Al-Bahri na kuzaa
naye.

Mhishimiwa Ibrahim Makungu aliyekuwa katika jopo la siri la Watu Kumi
na Nne ("Commeettee of 14") ambalo likiamua uuwawe, basi roho yako haikuwa
na salama Zanzibar, naye pia alimwoa msichana wa Kihindi aitwaye Katu Lalji
Punja
na pia alimwoa Nahida Sarhan, msichana wa Kiarabu.

Mwingine mwanajopo hili ni Ramadhan Haji ambaye alimwoa msichana wa
Kiarabu aitwaye Badriya Muhammad Seif.

Mhishimiwa Ali Muhsin naye pia aliwaoa wasichana wawili wa Kiarabu.

Dr. Salmin Amour, aliyekuwa Rais wa Zanzibar, alimwoa Bibi wa Kibaharani
anayeitwa Rukiya Khalil Mirza Al-Bahrani.

Kuna na wengine wengi tu waliokuwa wakijinata na Uafrika wao ambao wao
wenyewe waliwataka wasichana wa Kiarabu, wa Kibaharani na wa Kihindi na
kwa nguvu za Serikaliya Zanzibar walifungishwa ndoa za haramu na Serikali,
kwani wengi katika wasichana hao hawakuwa radhi kuolewa kwa mirututu ya
bunduki na nguvu za Serikali na wazee kufungwa jela na kuadhibiwa wakikataa
kutoa idhini ya kuwaozesha watoto wao wa kike.

Lakini pia, ni muhimu kusema kuwa kuna na wengi wengineo waliooana kwa
khiyari zao na kwa ridhaa za wazazi wao bila ya kulazimishwa na Serikali,
na haya ndiyo yaliyokuwa ya kidasturi tangu zama za zama.

Mifano ya waliokuwa wakijinata kwa "Uafrika" wao -- na kumfanya Mwarabu
ndiye adui wao mkubwa kabisa -- na wakati huohuo kuwaoa wasichana wa
Kiarabu ni mingi sana.

Jinsi Mhishimiwa Rais Abedi Amani Karume alivyotafakharia uamuzi wake
wa kulazimisha ndoa za aina hii, siku moja katika mwezi wa Januari 1968
aliwaamuru Wahishimiwa wote na wengineo waliofungishwa "ndoa" na
wasichana wa Kiarabu, Kifursi na Kihindi kufika katikaKarume House ili kupiga
picha pamoja.

Kwa hivyo yoyote asiyeijua Zanzibar na watu wake inataka aelewe vizuri nini
anasema anapozungumzia "Waafrika Weusi" kukhusiana na Zanzibar, kwani
hata watoto na wajukuu wa Mhishimiwa hayati Abedi Karume atawakuta
kuwasi "Waafrika Weusi" tena kwa walivyochanganya nasaba.

Wale leo wanaojinata kwa asili zao za "Uafrika Weusi" au za "Kibantu" au
zozote nyinginezo na kusema Waarabu na warudi kwao, watuelezee vipi
tuwakatekate vipande, kwanza, watoto na wajukuu wa hawa wahishimiwa
ilisehemu za miili yao zilizokuwa za Kiarabu tuzirejeshe Arabuni na sehemu
zilizokuwa za "Kibantu" tuzipeleke kuzizika Kamerun kwenye chimbuko la
Wabantu!

Kuna pia wale wanaojisemea ovyo kuwa "Wafrika Weusi" ndio walio wengi
Zanzibar.

Ukweli ni kuwa hakuna msomi anayezijua takwimu za watu wa Zanzibar
asiyejua kuwa ni Washirazi ambao ndio wenye idadi kubwa kabisa Zanzibar,
na kama walivyoandika katika barua yao wanachama wa African Association
tarehe 9 Julai, 1946 kumpelekea Balozi wa Kiingereza, kuwa Washirazi si
Waafrika ni Waasia.

Sasa, juu ya idadi ya Washirazi ongeza idadi ya wenye asili za Kiarabu na
za Kihindi, "Waafrika Weusi" vipi wanakuwa ndio wengi Zanzibar?

Tafadhalini, tukizungumzia jambo hadharani, kama katika mitandao, tuwe
tunapaelewa vizuri pahala tunapopazungumzia na tunaelewa vizuri asili za
watu wake zilivyo.

Vinginevyo itakuwa tunazungumzia tusiyoyaelewa vyema, tunapasuana vichwa
na kupotezeana wakati.''

Wanamajlis,
Hii ndiyo historia ya Zanzibar na hao ndiyo Wazanzibari ambao ndiyo leo hawa
wamekuwa kila wakipiga kura kuanzia mwaka 1995 wamekuwa wakiichagua
CUF lakini kundi dogo la wahafidhina ambao wanadai wao ndiyo wenye haki ya
kutawala wamekuwa wakitumia nguvu kupora ushindi huo.

Hivi sasa tuko katika mvutano wa uchaguzi wa 2015.
CCM Zanzibar wamekataliwa kwa mara nyingine na Wazanzibari.

CCM imeamua safari hii kufuta uchaguzi na wanataka uchaguzi urudiwe.
 
Mkuu hadithi yako ingeekeweka kama ungeongekea vile vile , yaani wewe na mtu wako huyo aliyekuandikia barua jinsi watu wasio waafrika walivyoingia kisiwa cha waafrika.
Kusema kuwa waafrika walitoka huko bara na wakahamia Zanzibar, ni kujidanganya na kutoukubali ukweli wa waadrika waliokuwepo hapo kwa karne na karne.

Siyo siri, ni kasumba inayowamaliza waafrika wa huko unguja na Pemba , kupenda kuoa wale wasio asili yao.
Wengine hufanya hivyo ili kuonekana kuwa kastaarabika au amekuwa mwungwana.
Offspings za hao watu ndo wako mbele kuukana uafrika wao na kufanya allegience na asili za mama zao.

Hili nimeliona, its a weakness and strenrh at the same time!

Kwa mtu wa matamanio, angeweza kusema pengine baada ya karne Zanzibar itakuwa a mixed race country na hivyo kuondoa chokochoko zote za kisiasa, lakini hata leo si hivyo.
 

Masopyakindi,
Tufanye mjadala wa kistaarabu sote tufaidike mie na wewe na watazamaji.
Lugha za ''hadithi,'' mnakasha utaharibika kwani kejeli hazijengi.

Mimi si mpiga hadith.

Inawezekana kwa hakika kulikuwa na Waafrika katika visiwa hivyo wenyeji
na pia wakaja wahamiaji Waafrika na Waarabu kwa karne nyingi.

Historia hii kwa hivi sasa kwa kweli nionavyo mimi haina maana yoyote.
Zanzibar ya karne ya 18 si Zanzibar ya leo ya karne ya 21.

Mengi yamebadilika na ndiyo maana rafiki yangu akaniandikia barua hiyo
niliyoiweka hapo.

Ndiyo maana leo unaona mahasimu wakubwa wa miaka ya 1950 na kabla ya
mapinduzi leo wanaoleana bila kinyongo.

Wala wajukuu hawaelezwi uhasama uliopita kati ya babu zao hadi kufikia
kuuana.

Sitaki kutaja majina kwani kufukua makaburi hakujengi.

Tatizo kubwa linalowakuta watu wa Bara katika muungano ni kudhani kuwa
wenye haki Zanzibar ni hawa mahafidhina licha ya ukweli kuwa kila wakiingia
katika uchaguzi Wazanzibari wanawakataa sasa miaka 20.

Kitu cha kujiuliza hapa ni hii inasabishwa na nini?

Iweje hao wanaojigamba kuwa ni ''wanamapinduzi,'' leo wanakataliwa na
Wazanzibari?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…