Kijana acha kujiita jobless, chukua hii achana na ubishoo

Kijana acha kujiita jobless, chukua hii achana na ubishoo

Mwachiluwi

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2022
Posts
25,258
Reaction score
48,589
Kijana mimi leo nakupa connection hii hakuna mtu jf hapa ata kuja kukupa hii conenction kabisa nakwambia acha ubishoo tafuta chako si vyema kujiita jobless vyeti weka pembeni fanya hii kitu

Mahitaji karanga, mayai,siagi/blueband,sukari na chumvi

Kwanza changanya blueband na sukari

1739185139207.jpeg

Kisha chukua mayai nayo changanya vizur mimi nilitumia mayai 2

1739185190537.jpeg

Baada ya hapo weka unga kidogo kweny karanga af uwe unachanganya polepole
1739185267303.jpeg

Baada ya hapo weka ule mchanganyiko wako wa mayai pole pole kidogo kidogo na ukologe

1739185340825.jpeg

Ukiona karanga na unga zimeanza kukaa pamoja malizia mchanganyiko wako kuweka wote

1739185409281.jpeg

Kisha weka kwenye mafuta ambayo yamepata moto polepole kwa wewe ambae sio mzoefu kuepuka karanga zako kuungua ukisikia zinaanza kulia pa pa jua teyari geuza geuza ili ziwe na rangi moja kisha toa
1739185512257.jpeg

Kisha weka kwenye chombo kikavu na zipoe vizuri

1739185587485.jpeg

Kwakua wewe unataka kuuza tafuta vifungashio vile vya kishua weka nenda nazo pale St peter wanapo uza maua ukiona mtu kasimamisha gari ana chagua mau nenda na karanga zako pale muoneshe uza ata 1500 kwasababu karanga yako imeenda shule watanunua na utaona kama kuna shida ya ajira au


Mimi pia nimesoma ila ubishoo nileweka pembeni nipo hapa kwasababu ya upishi tu elimu yangu nilio somea natumia mala chache sana wakati wenzangu wanaonyesha vyeti vya elimu mimi nilishow kipaji basi

Watu walipelekwa zahanati wengine ofisi kuu ila mm nilishow kipaji na baadae walikuja kujua kuwa na elimu baada ya kutokea mgonjwa alie poteza kumbu kumbu kumbe kuna mtu alisema yeye kasomea psychology kumbe sio kweli alisomea kwa upande wa elimu

Pale nika waonyesha vyeti nikamtibu yule kama huduma ya kwanza baada ya wiki nikatoa wazo apelekwe lugalo kwa matibabu zaidi

Nini nataka kusema acheni aibu mimi wakati nafanya iki kitu wengi walikebehi na kuniambia kazi za kike ila leo Mungu kaniona kwanafasi yangu 🤲
 
Back
Top Bottom