Kijana afanya utani wa kutaka kumuua Rais Magufuli, aambuliwa kifungo cha miaka 2 jela

Kwa mwendo huu, mitandaoni kuna wafungwa wengi sana, hii ni takwimu ya kidunia.
 
Huyu katishia tu kwa maneno ..

Vipi wale waliokuwa wanamfatilia Lissu ,na hatimaye kumshambulia kwa risasi mchana kweupe, walishapatikana na kuhukumiwa...?
IGP Sirro amesema hawajapokea mashitaka ya mlalamikaji yeyote kwa hiyo hawawezi kufanya upelelezi, angekuwa amepigwa risasi policcm sijui kama wangesubiri mtu apeleke malalamiko
 
Kakiri kosa ndio maana imekua faster, kama umefanya upupu na ukakana uchunguzi ndio unachukua muda
 
Huyu jamaa amefungwa lakini ujumbe amewachia ndg na jamaa zake john kuwa haitwawezekana joh apendwe wakati yeye mwenyewe hashituki hata raia wanauliwa wanakufa yeye asiwe na hata mshipa wa kukemea mauaji. John aliyetajwa ndio wanasema ni nembo ya taifa acheni uongo ni nembo ya chama chao
 
Siku zake zilifika. Ila uache utani, mitani sasa hivi mtukufu mtakatifu anasemwa vibaya sana. Hapa karibu na kwangu kuna kijiwe cha magazeti basi ikawa ni kawaida vijana kwa wazee kumponda na kumkosoa malaika mkuu. Weee siku moja walikuja wazee utafikiri wanaenda vitani ila niliwasifu wananchi maana walizua timbwili na kuwageuzia kibao geshi la borisi. Vurugu zikawa kubwa mawe kurushwa kelele na vifijo mpaka wanawake nao waliingia mtaani. Hawakuondoka na mtuhumiwa hata mmoja. Ila jamaa walivyo wabishi usiku wakaja tena kurandaranda lakini wapi siku hio wananchi wote walijifungia ndani mapemaa
 
Lazima kusoma alama za nyakati.
๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€Ukiona kichaa kabeba mawe na kirungu inabidi utengeneze urafiki TU na Huyo kichaa ๐Ÿ™„
Ndicho wenye Akili hukifanya sasa
 
Wapi huko? Acha uongo na ID zako kibao.
Ikiwa mie nina ID zaidi moja basi nife leo lakini kama nina ID hii moja, basi wewe unatumia zaidi uti wa mgongo kuliko ubongo. Ungeweka ushahidi juu ya hizo ID nyingine. Kilichonishangaza ulivyoongea kwa uhakika wakati hata hujui lolote. Inawezekana kabisa wewe sio mtu
 
Wapi huko? Acha uongo na ID zako kibao.
Halafu nimekujibu mwanzo kabla ya kusoma michango yako mingine sorry sikujua wewe ni mtu wa aina gani. Nina hakika katika majibu yangu ya mwanzo huwezi na hutaweza kuelewa hata mwisho wa dunia
 
Kwa mtazamo binafsi uko sawa coz Kuna makosa makubwa zaidi ya hayo husamehewa but sometime Sheria haitaji kupinda pinda, Kama dogo angekataa hajafanya na Kama Kuna ushahidi uletwe Basi kungekuwa na uwezekano wa kuepuka adhabu hiyo[emoji1732][emoji1732][emoji1732][emoji1732][emoji1732][emoji1732]
 
Tatizo lenu kubwa hatuelewani, sijui nitumie lugha gani, na kwa sababu mmelogewa kuunga mkono serikali hii dhalimu, basi kila linalofanywa na wateuliwa wa rais mnaona liko sawa, nimehoji hapo juu, hivi kweli hilo lilikuwa kosa la kumpeleka mtu jela ?, ndio mimi nikajibu kwamba sijaona kosa la kumfanya huyo kijana afungwe, na mkae mkielewa, kule magereza kuna watu wengi sana wamefungwa kwa makosa either ya kusingiziwa au ya kuonewa, lakini pia kuna watu wengi sana wameachwa uraiani na wakati walitakiwa kuwa magereza, nasikitika watanzania tunafurahia watu wanaendesha nchi kama mali zao binafsi, kijana mmoja huko mkoani geita alihukumiwa kulia faini ya shs 40,000 au kwenda jela miaka miwili, hakua na hela pale kwa sababu alitokea magreza alipokuwa mahabusu, hakuna mtu wa kumsaidia hakimu hata jhakujisumbua kumuuliza kama anaweza kupata mtu wa kumuwesha kulipa hiyo, akapelekwa magereza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ