Tatizo lenu kubwa hatuelewani, sijui nitumie lugha gani, na kwa sababu mmelogewa kuunga mkono serikali hii dhalimu, basi kila linalofanywa na wateuliwa wa rais mnaona liko sawa, nimehoji hapo juu, hivi kweli hilo lilikuwa kosa la kumpeleka mtu jela ?, ndio mimi nikajibu kwamba sijaona kosa la kumfanya huyo kijana afungwe, na mkae mkielewa, kule magereza kuna watu wengi sana wamefungwa kwa makosa either ya kusingiziwa au ya kuonewa, lakini pia kuna watu wengi sana wameachwa uraiani na wakati walitakiwa kuwa magereza, nasikitika watanzania tunafurahia watu wanaendesha nchi kama mali zao binafsi, kijana mmoja huko mkoani geita alihukumiwa kulia faini ya shs 40,000 au kwenda jela miaka miwili, hakua na hela pale kwa sababu alitokea magreza alipokuwa mahabusu, hakuna mtu wa kumsaidia hakimu hata jhakujisumbua kumuuliza kama anaweza kupata mtu wa kumuwesha kulipa hiyo, akapelekwa magereza.