Hivi kweli utake kumuua raisi wa nchi utangaze kama hivi?unajuaje alikuwa anafanya masihara?
usifuatishe vichwa vya habari vya magazeti uozo yetu haya
masihara ni utetezi wake kizimbani, ambao mahakama imeukataa...
Hahaha,unamtisha kumuua John ukiwa kwenye meza ya John,lazima John amuokoe John mwenzie
Tatizo lenu kubwa hatuelewani, sijui nitumie lugha gani, na kwa sababu mmelogewa kuunga mkono serikali hii dhalimu, basi kila linalofanywa na wateuliwa wa rais mnaona liko sawa, nimehoji hapo juu, hivi kweli hilo lilikuwa kosa la kumpeleka mtu jela ?, ndio mimi nikajibu kwamba sijaona kosa la kumfanya huyo kijana afungwe, na mkae mkielewa, kule magereza kuna watu wengi sana wamefungwa kwa makosa either ya kusingiziwa au ya kuonewa, lakini pia kuna watu wengi sana wameachwa uraiani na wakati walitakiwa kuwa magereza, nasikitika watanzania tunafurahia watu wanaendesha nchi kama mali zao binafsi, kijana mmoja huko mkoani geita alihukumiwa kulia faini ya shs 40,000 au kwenda jela miaka miwili, hakua na hela pale kwa sababu alitokea magreza alipokuwa mahabusu, hakuna mtu wa kumsaidia hakimu hata jhakujisumbua kumuuliza kama anaweza kupata mtu wa kumuwesha kulipa hiyo, akapelekwa magereza.
Naona mambo yake yalikwenda haraka kwasababu pia yeye hakutaka kuisumbua Mahakama kukataa maneno yake. Ingekuwa hivyo ingekwenda hadi miaka kuja kukamirisha upelelezi.Katenda kosa tarehe 26/nov Leo tarehe 4/12 na hukumu tayari imeshatoka!!! Pongezi kubwa kwa Mahakama kwa kuendesha kesi ushaidi kukamilika na kutoa hukumu ndani ya wiki moja toka mshtakiwa kutenda kosa.Mahakama nyingine nchini kote ziige mfano huu maana kuna ndg, rafiki, jamaa zetu wengi sana wapo mahabusu bila kujua hatma ya mashtaka yao.
Ni kweli mku. Bora useme kile unachomanisha.Ni vema kusoma alama za nyakati, huu si wakati wa kufanya masihara.
Kosa halihalalishi kosaAlikosea sana
Narudia tena Sijaona Kosa hapo, nimetoa mifano michache ya hicho unachokiita sheria, Hivi unajua iKila raia ana haki sawa mbele ya sheria ?, hao askari walioua na huyu aliyetania kwamba ataua, nani ana kosa linalostahiri adhabu ?, huyo kijana amekiri kwamba alisema hayo maneno wewe unataka kulazimisha kwamba amekiri alitaka kumuu, !!, wewe ni mtetezi wa wapangaji wa Ikulu ?, naamini unajaribu kujifanya mwehu ilhali una akili timamu, huyo malaika wenu mnamtetea ili mteuliwe ?, wengine mko mbali sana sio rahisi kuonwa, Kijana mmoja raia wa Argentina alimfyatulia risasi Papa John Paul ll mwaka 1984 lakini Papa aliamuru huyo kijana aachiwe huru !!
Civics form two tumejifunza nembo za taifa zipo kwa makumiHiki cheti changu chenye degeree inabidi kifutwe. Mimi miaka yote najua nembo ya taifa ni hii View attachment 1281372
Jamani, hivi kuna watu ni wanoko kiasi hicho hadi uende ukaripoti utani polisi?
Ni kweli Mkuu, wengi sana wamepandishwa vyeo kwa kuwafanyia mbaya watu wanaosema kinyume na anavyotaka rais, lakini mkuu mimi naamini hivyo vyeo wanavyopewa kama hawa akina makonda vinakuwa havina hata raha, kwa sababu mtu nafsi yako inakuwa inakusuta kila usikuNdugu yangu yanayondelea kwenye Utawala huu yanafurahisha kama siyo kinyume chake..!!
Watanzania wengi wamejaa unafiki, chuki na hasira kwa mambo ya kijinga jinga tu...!!! Utawala wa Jiwe umezidi kudhihirisha tabia za Watz( Displaying their real colours) za unafiki.
Kwamba kwa tabia ya Rais aliyeko madarakani kwa sasa ukijikomba, ukijipendekeza na kuwachongea wenzako hasa wapinzani wa Jiwe basi UNAWEZA KUAMBULIA japo UKUU WA MKOA, WILAYA au UKURUGENZI n.k.
Usije ukashangaa huyu Hakimu aliyetoa hukumu kwa kijana huyu maskini ukasikia amepanda daraja/cheo na kuwa Hakimu Mkazi, Jaji n.k. Watu wanapata vyeo au kupanda vyeo kwa kuumiza wenzao...ni aibu!!
Hivi kweli utake kumuua raisi wa nchi utangaze kama hivi?
Sijajua umesimamia upande upi, wa wale wanaoshabikia kwamba alistahiri adhabu hiyo au sisi tunaosema hakustahiri adhabu hiyo ?, kiswahili chako kigumu sana.ametangaza kwa sababu kutishia lazima utangaze
hajataka kumuua Rais, hakuna paliposemwa alitaka kumuua Rais
amefungwa kwa kosa la kutishia kumuua Rais
vitu viwili tofauti, kisheria makosa tofauti, adhabu tofauti...
Sijajua umesimamia upande upi, wa wale wanaoshabikia kwamba alistahiri adhabu hiyo au sisi tunaosema hakustahiri adhabu hiyo ?, kiswahili chako kigumu sana.
Uko sahihi mkuuuNi bora utishie kumuua Mungu utapona, lakini usijaribu kutishia kumuua John, hata ukiota ndoto tu kuwa John amekufa kaa kimya kabisa wakikusikia kuwa umeota ndoto Kama hiyo ujuwe utaishia gereza la Kisongo, Kama kuna mtu anabisha akamuulize Lema
Maelezo yako ni marefu sana na yalianza kunivutia, ila ulivyomalizia umeharibu kila kitu, umejivunjia heshima Mkuu.sio Kiswahili changu kigumu, tatizo vyombo vyetu vya habari vinapotosha umma kwa upeo wao finyu wa kuripoti masuala ya kimahakama.
Kuna:
1/ Kuua
2/ Kujaribu kuua
3/ Kula njama kuua
4/ Kutishia kuua
Hakuna kutaka kuua.
Hivyo hatuwezi kuongelea suala la ni kweli alitaka kuua au hakutaka, au alitania, kwa sababu, again, hakuna kosa la kutaka kuua!
Letu hapa ni kutishia kuua. Kutishia kuua hakujalishi kama kweli ulikuwa na uwezo wa kuua au whether ulimaanisha au ulikuwa unachimba "mkwara mbuzi." In other words, ukimtisha mtu kummwaga ubongo kwa jambia wachunguzi na waendesha mashitaka hawatakwenda nyumbani kwako kuangalia je kweli unalo hilo jambia au kiwembe au msumeno. Watatafuta uthibitisho mmoja tu, wenye pembe mbili: ulitamka vitisho (actus rea), na ulinuwia kutamka (mens rea).
Amefungwa kwa sababu alitamka tishio na alinuwia kutamka, mahakama imefanya sawa.
Me
Me mvivu kusoma.