Kijana ajiua akihofia kudaiwa Sh 45,000

Kijana ajiua akihofia kudaiwa Sh 45,000

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2021
Posts
590
Reaction score
1,648
Marehemu-Bukindu-new3072e9d13ac8.jpg

Kijana anayefahamika kwa jina la Bukindu Bukindu (22), mkazi wa kijiji cha Ihega, Kata ya Bukoli wilayani Geita amefariki kwa kunywa sumu ya panya, akihofia kudaiwa Sh 45,000 aliyoagizwa kununua soda.

Akizungumuzia tukio hilo, mama wa marehemu, Shija Anthony, amesema mwanaye alijiua siku ya sikukuu ya Krismasi, Desemba 25, 2022, ambapo alipatiwa fedha hizo na muuza duka kufuata vinywaji duka la jumla.

Amesema baada ya kufika duka la jumla alilipia na kukabidhiwa vinywaji na alipotaka kuondoka alizuiwa na kuamriwa kurejesha vinywaji na alipoeleza ameshalipia wahusika hawakumuelewa.

“Basi akaja kwa yule bosi wake aliyekuwa amemtuma, akaja kumueleza, ikabidi waende na yule bosi, walipofika kule wakaambiwa huyu mtoto hela ya vinywaji hajalipia.

“Yule bosi naye akamwambia, wewe dogo mimi nataka hela yangu, ukija dukani uje na hela, baadaye sasa wakati mimi napika akaniomba funguo, akatoka na kikombe cha maji, akaingia kwake akafunga,” amesema na kuongeza kuwa mwanawe alihitimu darasa la saba mwaka huu.

Ameeleza akiwa ndani mwanaye alikunywa sumu na kuanza kutapika na baada ya kubaini walifanya juhudi za kumpeleka zahanati kupata huduma ya kwanza, lakini hawakufanikiwa kuokoa uhai wake.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP), Ally Kitumbu amethibitisha tukio hilo na kueleza uchunguzi unaendelea kupata kiini halisi cha tukio hilo.

Habari Leo
 
Maisha haya yana siri nyingi bila kusahau taabu na mateso ya dunia, usikute alikuwa anavurugwa na mambo mengine pia ya kimaisha ukiongeza na hilo akaona bora kufa
 
Kwani alikuwa na tatizo lolote la afya ya akili? Maana miaka 22 ni mtu mzima na anauelewa wa kuweza kujitete na kudai haki yake.
Wasukuma ushamba mwingi Sana,waoga Sana,hawana exposure,Mimi was hukohuko
 
Kwani alikuwa na tatizo lolote la afya ya akili? Maana miaka 22 ni mtu mzima na anauelewa wa kuweza kujitete na kudai haki yake.
Halafu ndio amehitimu std 7 mwaka jana at 22? Dogo chaneli zilikua hazisomi vizuri.
 
Back
Top Bottom