Kijana ajiua akihofia kudaiwa Sh 45,000

Kijana ajiua akihofia kudaiwa Sh 45,000

Maisha haya yana siri nyingi bila kusahau taabu na mateso ya dunia, usikute alikuwa anavurugwa na mambo mengine pia ya kimaisha ukiongeza na hilo akaona bora kufa
Tieli this is something other people won't talk about, but it's 💯 correct 😔
 
Pumziko La Amani Apate huyo Dogo.

Ingawa hii taarifa bado ina walakini, ni Mtu wa tatu ndiye unasema Dogo alilipa pesa...si vizuri kusemea jambo usiloweza kuthibitisha tofauti na Muhusika mwenyewe.

Sio kosa kwa mtoa pesa kudai pesa yake maana asingeweza kuambiwa tu nililipa naye akasema "ok sawa".

Wafanye utafiti kuona tatizo lilikuwa wapi ingawa hapo tayari wanamkosa shahidi muhimu.
 
Polisi wawachunguze hao wa duka la jumla sio poa kukumbatia matapeli wamekatisha uhai wa kijana
 
Kama dogo ni huyo pichani hawezi kuwa na miaka 22 hii mbona ni miaka ya jitu zima lenye mke na watoto hata kama kuna wanaoanza primary wakubwa haiwezekeni mtu mwenye 22 awe amehitimu std 7 2022
 
W
Mm nmehitimu chuo na 19 afu we na 25 ujakosea umri kweli?

It's not about age it's about mentality pal, we've just lost an innocent soul here ,
I insist adhabu kali ichukuliwe kama itathibitika kua kaonewa.😔
Watoto wakisukuma huwa wanaanza shule akifika darasa la tatu anaacha anakaa miaka hata minne nyumbani badae anajipeleka tena shule kuanza darasa la kwanza
 
Kauli tata hapo iliposemwa alilipia na kukabidhiwa mzigo.

Uchunguzi wa kina ufanyike.
 
Hai Kuna mwingine kanywa sumu kiss alibarikiwa juma mosi sherehe ikawa juma nne na mwingine kajinyonga nae alibarikiwa juma mosi chanzo hakijajulikana
 
View attachment 2459915
Kijana anayefahamika kwa jina la Bukindu Bukindu (22), mkazi wa kijiji cha Ihega, Kata ya Bukoli wilayani Geita amefariki kwa kunywa sumu ya panya, akihofia kudaiwa Sh 45,000 aliyoagizwa kununua soda.

Akizungumuzia tukio hilo, mama wa marehemu, Shija Anthony, amesema mwanaye alijiua siku ya sikukuu ya Krismasi, Desemba 25, 2022, ambapo alipatiwa fedha hizo na muuza duka kufuata vinywaji duka la jumla.

Amesema baada ya kufika duka la jumla alilipia na kukabidhiwa vinywaji na alipotaka kuondoka alizuiwa na kuamriwa kurejesha vinywaji na alipoeleza ameshalipia wahusika hawakumuelewa.

“Basi akaja kwa yule bosi wake aliyekuwa amemtuma, akaja kumueleza, ikabidi waende na yule bosi, walipofika kule wakaambiwa huyu mtoto hela ya vinywaji hajalipia.

“Yule bosi naye akamwambia, wewe dogo mimi nataka hela yangu, ukija dukani uje na hela, baadaye sasa wakati mimi napika akaniomba funguo, akatoka na kikombe cha maji, akaingia kwake akafunga,” amesema na kuongeza kuwa mwanawe alihitimu darasa la saba mwaka huu.

Ameeleza akiwa ndani mwanaye alikunywa sumu na kuanza kutapika na baada ya kubaini walifanya juhudi za kumpeleka zahanati kupata huduma ya kwanza, lakini hawakufanikiwa kuokoa uhai wake.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP), Ally Kitumbu amethibitisha tukio hilo na kueleza uchunguzi unaendelea kupata kiini halisi cha tukio hilo.

Habari Leo
Hi tabia ya ya kuzingiziwa ujalipa bili Ni mbaya San kwenye jamii

Kuna siku namm kidgo nikajijongee [emoji3] nikikula nyama choma pale ngaramtoni. Bas nikamliza nikampa dogo pesa elf 10 bas yule cashier akasema hajanipa hella na mm nilikuwa Nina elf 10 tu alimuita mpk manager Kuja kunidai Kama siyo nilikuwa jasiri bas jamaa angebaki na simu nilikataa kata kata

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom