Kijana alichanganyikiwa na urembo wa mwalimu wake wakati anafundisha, amuoa baada ya kuhitimu

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000


Mwanaume mmoja wa nchi ya DRC, Hassan Remy amemuoa aliyekuwa mwalimu wake wa sekondari na kusema alishindwa kumsikiliza alipokuwa akifundisha darasani.

Remy amesema alimchumbia Maombi Jeannette aliyemzidi miaka 12 baada ya kumaliza shule na baadaye kumuoa, licha ya uhusiano wao kupigwa vita na watu wengi.

Remy amesema anafurahia ndoa yake na mkewe, Maombi na sasa wamebarikiwa kupata watoto wawili.

Akifanya mahojiano na chaneli ya Afrimax English, baba huyo wa watoto wawili amesema alishindwa kuzingatia masomo wakati Maombi alipokuwa akifundisha.

"Nilikuwa najiuliza kama yeye na mimi tunaweza kuwa pamoja. Nilijua ningekabiliana na upinzani mkubwa, ikiwemo umri wake mkubwa kwangu," amesema Remy.
 
The same story ya Emmanuel Macron, rais wa Ufaransa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…