Kijana amuua mama wa kambo akidai amemroga. Umasikini ni mbaya kuliko Corona

Kijana amuua mama wa kambo akidai amemroga. Umasikini ni mbaya kuliko Corona

Bravo snr

Senior Member
Joined
Aug 16, 2020
Posts
182
Reaction score
477

IN SUMMARY

  • Grace Chacha (67), mkazi wa kijiji cha Guta Wilaya ya Bunda mkoani Mara amefariki dunia baada ya kukatwa mapanga na mwanaye wa kambo, Matiku Chacha akidaiwa ni mchawi.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara, Daniel Shillah amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akiahidi kutoa taarifa baada ya kupata maelezo ya kina.

Akizungumzia tukio hilo mtoto wa marehemu, Joseph Chacha amesema tukio hilo lilitokea Aprili 22, 2021 saa 4 asubuhi katika kijiji cha Guta.

Amebainisha kuwa mama huyo anadaiwa kuuawa na kijana huyo aliyekuwa akiishi jirani na Grace, na kwamba kabla ya tukio hilo mtuhumiwa huyo anadaiwa kutamka maneno ya vitisho kwa marehemu akimtuhumu kuwa chanzo cha yeye kuwa na maisha magumu.

Chacha amesema kuwa siku ya tukio mama yake akiwa anatoka shambani alikutana na Matiku aliyeanza kumshambulia kwa mapanga sehemu mbalimbali.

"Alimkata na panga kwenye mkono wake wa kulia kisha begani baadaye akamkata maeneo mbalimbali mwilini..., alimkata puani na kutenganisha sehemu ya chini ya macho na pua kisha kuendelea kumkata kichwani hadi akapoteza fahamu,” amesema.

Chacha amesema mama yake hakupata msaada wa haraka kwa kuwa kitendo hicho kilitokea asubuhi na watu wengi walikuwa shambani akidai wivu ndio chanzo cha kijana huyo kufanya tukio hilo.

" Alikuwa anasema mama yetu ana maisha mazuri kwa sababu watoto wake wote wana kazi nzuri na wanamjali na kudai kuwa yeye ana maisha magumu kwa sababu mama yetu amemloga wakati sio kweli,” amesema.

Mwenyekiti wa mtaa wa Ihale, Marwa Mataga amesema, “sijawahi kushuhudia tukio la kikatili kama lile, yaani mama huyu aliuwawa kikatili sana alikatwakatwa kama mnyama nilipofika pale alikuwa bado anapumua lakini hakuwa na uwezo wa kuongea kutokana na hali aliyokuwa nayo.”

“Nitoe wito kwa vijana kuachana na hizi imani potofu na wafanye kazi kwa bidii ili waondokane na umasikini kuliko kukaa bila kujishughulisha na kuanza kulaumu watu kwa uzembe wao wenyewe," amesema Mataga
 
Dawa ya mchawi ni kumtia shoka la kichwa tu.

Wakiwa gizani wanaroga sana hawa na kuharibu hatima za watu.

Wana roho mbaya na chafu kama mashetani.

Kwahiyo dawa ni SHOKA tu.

Na mimi nasema KATA SHOKA.

Maneno ni mawili tu... K.A.T.A S.H.O.K.A.
 
Dawa ya mchawi ni kumtia shoka la kichwa tu.

Wakiwa gizani wanaroga sana hawa na kuharibu hatima za watu. Wana roho mbaya na chafu kama mashetani...
Umamjuaje mtu kuwa ni mchawi?

Kama kigezo cha kuwa na maisha mazuri ni uchawi, basi na yeye angetafuta uchawi awe na maisha mazuri sio kuua
 
Huyo kijana sio mwendawazimu. Kuna jambo nyuma ya pazia.

Haiwezekani tu amrukie na kumtia mapanga ya kichwa.

Hawa wachawi huwa wanajifanya wakarimu sana na unaweza kushawishika kuwaonea huruma, lakini wakiwa gizani wanakushughulikia haswa mpaka wanakumaliza.

Hata biblia inasema USIMUACHE MWANAMKE MCHAWI AISHI.

KATA SHOKA LA KICHWA.

Ukikamatwa na serikali waambie nimeua kwa madhumuni ya KUJILINDA na KUJIHAMI.
 
Umamjuaje mtu kuwa ni mchawi?
Kama kigezo cha kuwa na maisha mazuri ni uchawi, basi na yeye angetafuta uchawi awe na maisha mazuri sio kuua
Mkuuu ulishawahi ishi kwa mama wa kambo wewe, ndugu yangu ni washirikina haswaaa na hawapendi upate maendeleo huo ndiyo ukweli

Mama wa kambo mwenye upendo wa kweli ni wachache mno mno.
 
Huyo kijana sio mwendawazimu. Kuna jambo nyuma ya pazia.

Haiwezekani tu amrukie na kumtia mapanga ya kichwa...
Acha uvivu wewe! Fanya kazi kwa bidii ili ufanikiwe. Uchawi ni imani potofu! Kiufupi tu, HAKUNA UCHAWI!

Na ushahidi uko wazi, wanao amini uchawi karibia wote ni watu masikini na wasio na elimu! Asilimia chache zilizobaki, ndiyo huchukuliwa na wanasiasa wa ccm, na baadhi ya viongozi wa vilabu vya mpira wa miguu.
 
Acha uvivu wewe! Fanya kazi kwa bidii ili ufanikiwe. Uchawi ni imani potofu! Kiufupi tu, HAKUNA UCHAWI!
.
Kuandika tu kwa 'italics' kunathibitisha kwamba una mongolism na matatizo mengine madogo madogo ya kiakili.

Hii inaonesha hata maandishi yako mwenyewe hauyaamini mpaka uyakoleze kwa kuyalaza.

Kama wewe mwenyewe haukiamini unachokiandika, mimi nawezaje kukupa umuhimu wowote!?

Kwahiyo, naamini wewe ni mtu dhaifu unayejificha kwenye 'italics' ili ujitutumue angalau kunikoromea.

Na si ajabu wewe ni MCHAWI pia.

Hapa unajibaraguza tu huku umedumbukiza hirizi mkunduni.
 
Eti elimu duni! Hahaa

Haujaijua vizuri hii dunia wewe mtoto mdogo unayenyonya!

Hiyo elimu yako ya CIVICS si lolote lile. Kuna elimu ya juu kuliko hiyo.

Na kusema kweli, wewe ndio mwenye elimu duni.
Kwa kuwa humu hatujuani tulicho somea ngoja nitulie, ila ukiamini uchawi lazima uwe duni kimaendeleo hata ukiumwa malaria yale yanayo leta ukichaa utasema umelogwa, hapo ndo umuhimu wa elimu unajulikana. Wenzetu wanajikita kwenye programming (OOPS ) sizani kama utakuwa unajua maana hii tunaijua tulio somea civics tu, wewe jikite kutafuta uchawi tuone kama unaendelea.

Ngoja nikuambie kisa kimoja labda utaelewa, miaka ya tisini kuna kaka yangu alifaulu kwenda special school, nikiwa mdogo niliwasikia watu walisema haiwezekani mtu afaulu kama vile bila kuwa mchawi, ingawa nilikuwa mtoto ilinikatisha tamaa sana maana nilikulia katika mazingira ya dini hadi nikawa najisemea kuwa mimi Sitaweza kuwa msomi ikiwa uchawi unahusika, ila mpaka hapa nimefika na utu uzima wangu sijawahi feli katika mitihani yangu yote na sina hata chale mwilini.

Na wale ambao nawakumbuka walikuwa wanamsema ndugu yangu hawana chochote, tukienda likizo ni kutuomba pesa utafikiri walitukopesha. Amini katika uchawi ufe masikini au uwe mtumwa wa tunguli.
 
Uchawi ni kitu halisi na unarudisha nyuma sana maendeleo yetu

Huwezi pata ushahidi wa uchawi kwa kutumia simu ya kisasa

Biblia imeshasema adhabu ya mchawi ni kifo

Sina ushahidi kuwa mwendazake ni mchawi ila uchawi ni kitu hatari sana
 
Back
Top Bottom