Kijana jitunze, kuteremkia miaka 40+ kuna zimwi linaitwa Kisukari na Presha. Mkeo atakuvumilia?

Yeah! Andiko limekosa mantiki baada ya kubainisha kuwa lengo la kutunza afya ni ili usipungukiwe nguvu za kiume.

Waafrika tunakuza sana hii ishu ya nguvu za kiume kana kwamba maisha kwa ujumla wake maana yake ni nguvu za kiume! NONSENSE!

Andiko Lina mantiki kubwa mno. Sema bado hujapata upeo wa kuchambua maandiko ya namna hii.
 
Haya yote kwanza kabisa maisha yawe settled alafu mpaka maisha kuwa settle ni kuanzia 40+ alafu iyo 40+ ambayo maisha yanaanza kuwa settled ndo hayo malazi yanaanza kukuandama.. katika maisha kikubwa uhai tu
Kikubwa afya,unaweza kuwa hai na maisha yakakuchapa,magonjwa yanakuandama,ukatamani bora usingezaliwaga.
 
Taikon wa Fasihi umelitendea haki jina lako.
 
Asante
 
Kifo kipo pale pale, hakikwepeki; tunaweza tu kuongeza siku za kuishi, lakini kifo hakizuiliki.
 
kifupi kama una kazi inayokutoa jasho kisukari utakisikia tu,kama ni mtu wa ofcn mazoezi ni muhimu sana kama ulivosema.
Aisee usijidanganye
Kuna watu nawajua kazi zao zilikuwa za kutumia nguvu na bado kisukari hakijawaacha.Yaani kazi anayofanya mtu ni ngumu kiasi hakuna haja ya mazoezi.
Labda pia life style na chakula vinachangia.
Au ni ule ugonjwa wa kurithi unakuta familia ina historia toka vizazi
 
Wanawake wa siku hizi na staili za maisha yao ni vigumu sana kuwaridhisha! Tuombe sana Mungu na kumcha pia, usimfanyie mwenzako kile usichopenda kufanyiwa [emoji1431]
 
Andiko Lina mantiki kubwa mno. Sema bado hujapata upeo wa kuchambua maandiko ya namna hii.
ROBERT HERIEL, wewe ni kijana mdogo sana, naweza kutabiri uko kwenye 20's, na ndio maana umri uliotaja wa miaka 40 unauona ni mkubwa kiasi cha kuutabiria magonjwa..

Miaka 40 ni umri mdogo sana, mimi nimeshaupita na bado naonekana mdogo,.. Sina hizo dalili za visukari sijui na vitu gani ulivyosema...

Nimeelezea hayo kwa sababu wewe unadhani mimi sijapata upeo wa kuchambua ulichokiandika..., ngoja nirudi kwenye mada..

Ulichokiandika kina uhalisia fulani, ulichoharibu tu ni kuweka msisitizo kwenye nguvu za kiume na kuchapiwa, hayo ni mawazo ya watoto wadogo, wanaowaza ''kusimamia kucha" ili usichapiwe.. Ukishafika umri wa utu uzima kama wangu, mambo hayo utayaona ni IRRELEVANT!
 
aise tutaponea wap sasa.
 

Mkuu miaka yenu na yetu ni tofauti kabisa.
Sasa Kama kijana wa 20's anatumia Mkongo au busta yoyote Ile ili mambo yamuendee unafikiri hiyo 40+ atakuwaje.

Mpaka nimeeleza Jambo hili ujue nimeshalifanyia upembuzi na uchunguzi Mkuu.

Kama umesoma vizuri kuna sehemu nimeandika Kwa mwanaume 40 bado ni kijana Mdogo. Lakini wengi waliofikisha umri huo Kwa miaka hii wanakuwa Hoi.

Waulize wanawake watakuambia, kaa na wanawake Kwa akili watakueleza, pia jihusishe kwenye mambo ya uzazi na nguvu za kiume utakutana na wanaume wengi WA namna niliyoeleza.

Ingawaje ulichosema ukweli lakini hakuna uhalisia katika Zama hizi
 
Kama mlikuwa mmefundwa ndio haina namna itabidi Mkeo iopujakuheshimu (aende akafanyie uchafu mbali)
Kuna kipindi unajikuta una Kisukari una Presha na Moyo umeshapanuka kwa Pombe za ujanani huna mtoto huna Nyumba hela zote ulifungulia zipu Ujanani.

Unaishia kuwa mpiga mbizi mashuhuri ili kulinda ndoa isibumbuluke😂🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…