Kijana jitunze, kuteremkia miaka 40+ kuna zimwi linaitwa Kisukari na Presha. Mkeo atakuvumilia?

Wanawake wa siku hizi na staili za maisha yao ni vigumu sana kuwaridhisha! Tuombe sana Mungu na kumcha pia, usimfanyie mwenzako kile usichopenda kufanyiwa [emoji1431]

Lengo sio kuwaridhisha Bali mwanaume kuweza kujimudu na kuepuka aibu na huzuni.
 
Kuna kipindi unajikuta una Kisukari una Presha na Moyo umeshapanuka kwa Pombe za ujanani huna mtoto huna Nyumba hela zote ulifungulia zipu Ujanani.

Unaishia kuwa mpiga mbizi mashuhuri ili kulinda ndoa isibumbulukeπŸ˜‚πŸ€£

Mungu aepusheπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Ujanja wote Keisha! Kudadadeki!
 

Wengine wanasema kisukari kinapata watu wenye vipatoπŸ˜‚πŸ˜‚
 
Umeandika vizuri..

Ngoja na mimi nijaribu kufafanua.
Suala la nguvu za kiume ni Conspiracy, ni njama. Kuna watu wanalikuza maksudi ili wafanye biashara.

Matokeo yake watu wasio na tatizo hili wanajengwa kisaikolojia na wanadhani wanalo, wanaanza kutumia hiyo mikongo na matokeo yake wanaharibikiwa kweli, wanakuwa tegemezi wa hiyo mikongo!

Tendo la ndoa sio vita, unaweza ukaenda raundi moja tu na wewe na mwenzako mkaridhika!, Lakini siku hizi, hata anaeweza kufanya raundi mbili ndani ya usiku mmoja anataka kuaminishwa kuwa ana tatizo.., Sio kweli! Suala hili lipo kisaikolojia zaidi..

Kwa hiyo TAIKON, unaposema kuwa hili ni tatizo kubwa unaweza ukawa unasaidia katika njama labda bila hata wewe kujua. Sikatai kwamba halipo, lipo ila siyo kwa kiwango kinachosemwa.

Otherwise, umeandika vizuri mkuu!
 

Umeongea vizuri Sana.
Mimi sipo katika propaganda ya kukuza kuwa kuna tatizo la nguvu za kiume.

Ila naeleza kuwa ugonjwa wa kisukari na presha ukimpata mtu moja ya athari zake ni pamoja na ukosefu wa nguvu za kiume.
Ndio maana nimeandika andiko hili ili kujikumbusha na kukumbusha watu kujihadhari na mitindo mibaya ya maisha ili tusijejikuta katika magonjwa hayo.

Hiyo ya nguvu za kiume ni kidokezo au kichomekeo ili kuwafanya watu waone uhatari na unyeti wa Jambo lenyewe.

Uliwahi kukaa na wagonjwa wanaume wa Sukari au Presha?
Kama uliwahi kukaa nao basi huwezi shangazwa na nilichoandika
 
Na sisi ambao tumeanza punyeto toka Primary mpaka leo hii tupo ndani ya ndoa na tunaendeleza tufanyeje??????
 
Uzi mzuri sana! Bahati mbaya hayo magonjwa yanapiga mpaka vijana wa 30+.

Nimezika bro ile march 12 siku chache kabla ya JPM.
Yaani mnavyozungumzia haya magonjwa napata uchungu sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole Mkuu
Mbaya zaidi ukute yapo kwenye familia.
Kwa upande wa baba yangu sukari ipo inatembea kizazi hadi kizazi.
Basi nasi tunajua huko mbeleni kuna tutakaokuwa nao.
Imagine familia ya watu saba watatu tu ndio hawana sukari hawa waliobaki wanapambana nao.
 
Hahahahaha!!!!
 
Ukifariki na mwili ulionona hata mchwa wanakuombea thawabu zikutangulie huko uendapo.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£ Daah! nimecheka kama chizi..
🀣🀣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…