Kijana jitunze, kuteremkia miaka 40+ kuna zimwi linaitwa Kisukari na Presha. Mkeo atakuvumilia?

Mweee.... ndiyo kwanza nimenunua serengeti lager inavuja jasho na hili andiko lako na hii wikiendi vitu viwili tofauti kabisa mpaka nimekumbuka enzi nakua babu yangu alikuwa hataki wakati wakula na kunywa udeal na mambo mengine leo nimeelewa babu kama aliiona hii siku, anyway kachupa kamoja, mbili n.k au hata kwa siku moja si dhambi.
 
Duh!🤦🏾‍♂️Starehe ya kwanza ya masikini.😄
hiyo sio starehe ya kwanza kwa maskini, hiyo ni starehe ya kwanza kwa kila mwanaume rijali haijalishi ni billionea ama zeronea.
 
Nabii Musa alikufa na miaka mingi (80 kama sikosei) na alikufa huku macho, meno yakiwa vizuri kama teenager. Enhee hapa wasemaje
Ni miaka 120, miaka 80 ndipo alipo itwa na Bwana kwenda kuwatoa wana wa Israel kwa farao Egypt
 
Hilo la nyege mshindo nalo ni neno!

Mimi ni mtu mzima nina ugonjwa wa mhemko wa balekhe!

Ninatamani kuishinda hii dhambi kwa mbinu mbali mbali lakini nakumbana na vikwazo lukuki!

Nikiona mwanamke anayevutia hisia zangu, kwanza huanza kujaa mate ya ugwadu mdomoni,hali initokeayo muda nionapo acidic fruits!

Hubaki nikijiuliza: hivi kila mwanaume, tamaa zake humsumbua kama mimi au nina ugonjwa halisi?

Sasa kwa kuwa umri umesonga najitahidi kujibaraguza kama sijaona kitu ili nisiadhirike, lakini wapi bwana!

Hujikuta navunja shingo bila kutarajia ili kumfuatilia mwanamke aelekeako ili kufaidi msura wake, hiyo sasa siyo kwa hiyari ni kwa lazima.

Nikiisha kuzindukana, hujikuta naongea peke yangu kujadili kutokukubaliana na umbo la mlimbwende huyo, kwamba hawezi kuwa vile, hilo lote si kweli kuwa ni la kwake, kajaladia ama la mchina, mbona anaringa sana hasalimii wazee na mawazo tele ya namna hiyo ya kipumbafu pumbafu nk nk.

Nikaona kujiepusha na ufedhuli huu, niitint gari pia ninunue miwani tinted glass kabisa, ili haya ya dunia niyaangalie kwa shadow kupunguza maumivu ya kuona live!

Mpaka hapo kujiheshimu nimeshindwa maana shetani akinipanda kichwani hunishawishi kuvua miwani ili kuondoa "arosto", sasa ninatafuta dawa.

Ninaomba kiongozi unipe njia halisi ya kujiepusha na hii fadhaa inayotesa uzeeni.
 
One of the best thread i have met so far jn 2022.

SUBSCRIBED ikiwezekana wenye confessions waje pia for good
 
Ukiwa na "mitindo mibaya ya maisha, kula na kunywa," mwili unasusa kuzalisha insulin ?????

Answer that.
Mtindo mbaya wa maisha hupelekea seli za mwili kujenga usugu wa insulin...yaani insulin resistance.

Hii hupelekea kisukari kwa vile unakula sukari ubongo unatoa maelekezo kuwa insulin izalishwe kuzipa signal seli za mwili kutumia sukari hiyo.

kwa vile seli zimejenga usugu dhidi ya insulin basi zinagoma kuitumia ile sukari, na matokeo yake sukari inakuwa nyingi kwenye damu. Mwili unazidi kuzalisha insulin zaidi kuzishinikiza seli kutumia sukari ambayo hupelekea hyperinsulinemia.

ili kukunusuru mwili hukufanya uhisi kiu kikali ili unywe maji na kuikojoa ile sukari iliyogomewa na seli za mwili...Ndiyo maana diabetics wengi huwa na hii dalili ya kiu kikali.

Ubongo hutafsiri kuwa mtu huyo hajala kwa vile seli zake zimeshindwa ku metabolize sukari...kitendo ambacho hufanya Ubongo utoe maelekezo ya kuzalishwa homoni ya kukufanya uhisi njaa ilihali umetoka kula muda si mrefu.

Hicho ndiyo kisukari kiletwacho na usugu wa seli dhidi ya insulin na si aina ile ya kisukari kijacho kwa kongosho kushindwa kuzalisha insulin ya kutosha.
 

Nafikiri wengi tupo hivyo sema tunajizuia tuu.
Nitaanzisha thread moja kuhusu hilo.

Huo ni ugonjwa wa wengi nikiwa mmoja wao.
 
Ahsante mzee baba hii imekaa vizuri.
Inakuwaje na hawa wanaofikia huko na pressure imeanza kuonekana ananyemelea na wanawake under 30 na muda ungine kuoa kabisa...!!!!
 
Mkuu mbona unataka kupingana na baiolojia?

Ukikumbwa na "menopause" kwenye 50's bado tu utaendelea kutamani?

Au kwa kuwa siku hizi mnabwia "vinasaba"?

Naomba maswali yote niyaelekeze kwako....

Masubiria majibu.....!😊
 



Mkuu mbona unataka kupingana na baiolojia?

Ukikumbwa na "menopause" kwenye 50's bado tu utaendelea kutamani?

Au kwa kuwa siku hizi mnabwia "vinasaba"?
 
"Gender" tofauti mkuu ndiyo maana nikanyooka bila kuuma uma maneno.

Neno "kukoma" kibaiolojia sisi halituhusu, lakini nyie linawahusu na wewe unaelewa vizuri tu, ndiyo nikahoji hivyo.
 
Ukiwa na "mitindo mibaya ya maisha, kula na kunywa," mwili unasusa kuzalisha insulin ?????

Answer that.
Kadiri umri unavyoenda organs za mwili zinapungua ufanisi. Mfano zinazozalisha insulin. Sasa inabidi uzisaidie Kwa kujiangalia mwenendo wa maisha yako.
Uwezo wa figo za mtu mwenye umri wa miaka 18 sio Sawa na figo za mtu mwenye miaka 60 kuna wear and tear sasa kama umezi-abuse wear and tear inakuwa kubwa.
 
Ni yule Dr nin?
 
Shukran mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…