Kijana jitunze, kuteremkia miaka 40+ kuna zimwi linaitwa Kisukari na Presha. Mkeo atakuvumilia?

Kijana jitunze, kuteremkia miaka 40+ kuna zimwi linaitwa Kisukari na Presha. Mkeo atakuvumilia?

Mtindo mbaya wa maisha hupelekea seli za mwili kujenga usugu wa insulin...yaani insulin resistance.

Hii hupelekea kisukari kwa vile unakula sukari ubongo unatoa maelekezo kuwa insulin izalishwe kuzipa signal seli za mwili kutumia sukari hiyo.

kwa vile seli zimejenga usugu dhidi ya insulin basi zinagoma kuitumia ile sukari, na matokeo yake sukari inakuwa nyingi kwenye damu. Mwili unazidi kuzalisha insulin zaidi kuzishinikiza seli kutumia sukari ambayo hupelekea hyperinsulinemia.

ili kukunusuru mwili hukufanya uhisi kiu kikali ili unywe maji na kuikojoa ile sukari iliyogomewa na seli za mwili...Ndiyo maana diabetics wengi huwa na hii dalili ya kiu kikali.

Ubongo hutafsiri kuwa mtu huyo hajala kwa vile seli zake zimeshindwa ku metabolize sukari...kitendo ambacho hufanya Ubongo utoe maelekezo ya kuzalishwa homoni ya kukufanya uhisi njaa ilihali umetoka kula muda si mrefu.

Hicho ndiyo kisukari kiletwacho na usugu wa seli dhidi ya insulin na si aina ile ya kisukari kijacho kwa kongosho kushindwa kuzalisha insulin ya kutosha.
Mtindo wa maisha gani ndio unafanya seli ziwe sugu kwa insulin ?

Tafadhali usinieleze details za symptoms za kisukari, kiu, kukojoa, ubongo umesema hivi njaa ikafanya vile... please!

Just answer the question.
 
Mtindo wa maisha gani ndio unafanya seli ziwe sugu kwa insulin ?

Tafadhali usinieleze details za symptoms za kisukari, kiu, kukojoa, ubongo umesema hivi njaa ikafanya vile... please!

Just answer the question.

pitia hiyo article.
 

pitia hiyo article.
Nimepitia hiyo article. Inasema hivi:

What causes insulin resistance and prediabetes?​


Researchers don’t fully understand what causes insulin resistance and prediabetes, but they think excess weight and lack of physical activity are major factors.

Watafiti hawajui kinachosababisha insulin resistance na kisukari. Kwa sasa wanabahatisha sababu za hapa na pale.​

Usinipe lecture za juu juu kwa kitu ambacho hujakaa maabara kukitafiti.​

 
Pimwa upone......kwakweli hii ni dawa but c rahisi kuipokea
 
Utakuwa unaumwa wewe, una kilo Kama za kuku?
Hapana, ni aina ya maisha niliyokulia(nimekulia maisha ya shida na ni mtu mwenye mawazo sana ninapokuwa peke yangu), pia kiumbo ni mwembamba na ni mfupi 5.3' sikumbuki mara ya mwisho kuugua ilikuwa lini na juzi nimefanya chekup npo ok
Kwa Bed naperfom vizuri
Namshukuru Mungu kwa kuniweka salama mpaka sasa

KAMA NI UGONJWA LABDA UNIAMBUKUZE WEWE
 
Kaka ubarikiwe sana kwa andiko hili. Watakaobahatika kusoma mpaka mwisho wakazingatia, hakika watafadika. Mimi ni shuhuda wa hili.

Niko 55, nilipokuwa 40 niliyumba kidogo performance yangu ya ndoa haikuwa nzuri kiviiile kwa sababu ya pombe nyingi na kubugia misisi bila utaratibu.

Ilipogonga 50 nikapunguza na 53 nikaacha kabisa pombe na kula bila mpangilio na nikawekeza sana pia katika shughuli za kiroho. Kwa kweli niko supa mpaka mwenza wangu ananishangaa.

Sent from my SM-A325F using JamiiForums mobile app
Aisee Mimi Nina miaka 53 imetokea mwaka Jana nikiwa na 53 nikapata mtoto watu wengi wamenishangaa sana lakini kiikweli Niko vzr kama kijana tu kwa mambo hayo na namshukuru Mungu.Changamoto itakuja labda kwenye malezi.He unadhani asilimia kubwa ya vijana wa sawa hivi wakifikia umri wangu wayayaweza hayo?...Na mtoto amechangamka kweli na namuona ana utambuzi kwa kiwango cha juu.Nampenda na kumtunza mfano lishe nzur ! Unga wa mbegu za maboga n.k.
 
Daah afadhari maana nna 36yrs now ila bado naona damu inachemka balaa na huu ushauri umekuja muda muafaka wacha nianze kubalance kuanzia sasa
Utakapofikisha 41+ mshumaa utawaka zaidi unaweza tamani kuoa mke wa pili.Nina 53 nilipitia huko!!!!
 
Utakapofikisha 41+ mshumaa utawaka zaidi unaweza tamani kuoa mke wa pili.Nina 53 nilipitia huko!!!!
Nimeanza utaratibu wa kunywa maji robo lita ninapoamka, pia nina utaratibu wa kutumia asali na kula matunda kwa ajiri ya kuboresha afya yangu
Kinachonitatiza ni mawazo yananifanya niwe na kilo chini ya 50 japo najaribu kuyapunguza
 
Back
Top Bottom