Kijana jitunze, kuteremkia miaka 40+ kuna zimwi linaitwa Kisukari na Presha. Mkeo atakuvumilia?

Kijana jitunze, kuteremkia miaka 40+ kuna zimwi linaitwa Kisukari na Presha. Mkeo atakuvumilia?

Kwema Wakuu!

Hatufuatiliani wala hatupangiani maisha. Ila tunakumbushana huku nami nikijikumbusha pia Kwa Nia nzuri tuu. Ili baadaye tusijekujikuta katika Huzuni kuu.

Vijana tunapoambiwa tule na tunywe Kwa nidhamu sio Kwa sababu tunaonewa wivu au kuna mtu anataka kuwa juu yetu Kwa kutupa amri. HASHA! Bali ni Kwa faida yetu.

Kisukari na Presha sio magonjwa mazuri Kwa ustawi wa Ndoa zetu. Ukisikia pigo Baya basi ni kukosa nguvu za kiume. Tena Kwa miaka 40 Kwa mwanaume bado ni kijana. Na Kwa bahati nzuri miaka hiyo wengi neema ndio zinazidi kufunguka na wamesha-settle.
Sasa ume-settle alafu unajikuta huna nguvu za kiume. Asikuambie mtu inahuzunisha Sana..

Ukiona Taikon anaelezea Jambo Fulani basi kaa nalo macho, lizingatie Sana. Kwa sababu Taikon nipo kwaajili ya kujenga na wala sio kubomoa.

1. Kula na kunywa vizuri,
i. Kula Mbomboga Kwa wingi, Kula Protein Kama nyama nyeupe, maziwa, mayai, Kwa wingi,
Kula wanga kidogo Sana. Mfano unapoka maharage mengi alafu unakula na wali kidunchu, au ugali kidogo na Samaki au nyama au maharage mengi.

ii. Matunda, pendelea Kula matunda,
Kama umeoa, pendelea Ndizi zilizoiva angalau kila siku moja hasa usiku, hii itafanya uume wako kuwa na nguvu kutokana na madini ya Potassium,
Mkeo aweke Kachumburi yenye Nyanya, vitunguu, limao na pilipili hizi zinaongeza Libido.
Safisha figo Kwa Matikiti, matango, usisahau mapapai na maembe, pia machungwa huku utapata vitamini

Kula Milo miwili ukiwa age ya 25-50 iwe balanced.

iii. Kunywa maji mengi, angalau Lita mbili na nusu mpaka tatu na nusu Kwa siku.
Pombe kunywa kiasi Kwa STAREHE sio kujiumiza. Angalau kwa wiki mara moja na hakikisha usinywe mpaka ukazima.
Maji mengi ni dawa kwani yanafanya seli za mwili wako kufanya kazi Kwa ufanisi zaidi. Maji hupunguza pia sumu mwilini na kuufanya mwili wako kuwa na Nuru,
Yaani mtu anayezingatia kunywa maji ngozi yake hung'aa

Pia maji mengi husababisha mtu kutokuzeeka Kwa haraka. Na hii ni kutokana na Uzalishwaji wa seli za mwili kufanyika Kwa ufanisi


2. Fanya mazoezi,
Mazoezi hujenga mwili na kuufanya kuwa na Afya, kwani hufanya mzunguko WA damu kufanya kazi vizuri. Kumbuka Damu ndio hubeba virutubisho na kuvisafitisha mwilini. Kumbuka pia ndani ya damu ndio kuna Seli nyeupe zinazolinda mwili dhidi ya magonjwa, Seli nyekundu ambazo husafirisha hewa ya Oksijeni kuzipa Seli, tishu na ogani Uhai. Hasahasa Ubongo.

Hii ni kusema mazoezi yanaimarisha ufanyaji kazi WA viungo vya Mwili Kama vile Ubongo. Hii inafanya akili kuwa active.

Aina ya mazoezi
i. . Mazoezi ya Mwili
Haya yanalenga zaidi viungo na organ za mwili. Kukimbia, Push-up n.k.

ii. Mazoezi ya Akili/Ufahamu.
Haya yanalenga zaidi tafakuri, uchanganuzi, uchambuzi, n.k. haya ni Kwa kusoma Nyaraka na vitabu, michezo na Bangua bongo, Game zinazoshughulisha akili n.k.
Pia mazoezi ya ubongo hufanyika Kwa kujaribu kufanya vitu vipya ili kutafuta changamoto mpya. Kama ni biashara, au kazi au miradi unaanzisha ili akili ipate changamoto mpya.

iii. Mazoezi ya Kiroho na Nafsi.
Haya hulenga zaidi roho na Nafsi yako.
Kudhibiti Nafsi yako na matamanio yake, mfano Kufunga Kula na kunywa,
Kama unapenda kunywa pombe kujizuia kutokunywa Kwa muda wa siku kadhaa.
Kama unapenda Kulala na wanawake, kujizuia hata Kwa miezi sita bila kuchepuka, hayo ni mazoezi ya kiroho na nafsi.
Pia kutoa Zaka au Sadaka Ile inayouma. Ni zoezi la Nafsi au kiroho.

Hii itakusaidia kujidhibiti, pia kuzuia Nyege mshindo au ukosefu wa maamuzi.

3. Mapumziko na Burudani/STAREHE.
Angalau Kwa siku ulale masaa yasiyopungua Nane.
Starehe au burudani angalau Kwa wiki au Kwa mwezi mara moja. Hii itakufanya usiyachoke maisha na kuyaona hayana maana.

Usingizi utakusaidia kutunza Ubongo wako na hii itakusaidia nyakati za uzeeni kwani utakuwa haupotezi kumbukumbu kijinga jinga.
Kabla watu hawajaona uzee wako wewe mwenyewe utaanza kuuona Kwanza Kwa kujikuta unasahau sahau mambo, na hiyo huanza kutokea miaka 30+ kama hutokuwa mtu wa kuzingatia mapumziko.

Kijana wa sasa unapaswa ujidhibiti mwenyewe ili isijekula kwako ufikishapo miaka 40.
Hakuna kitu kibaya Kama kufikisha umri huo yaani 40+ alafu ujikute hauna pesa, alafu magonjwa Kama kisukari na Presha vikupige. Ni hatari Sana.
Kupigiwa nje nje! Yaani mwanamke wako wala hatakuwa na Woga, nawe utakuwa unajua na chakumfanya hauna.

Wale mnaolalamika andiko refu nimewasikia. Nipumzike sasa!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Taikuni umetisha sana ila pombe siachi
 
Siku hizi Vijana wadogo wanapigwa na Stroke mpaka unashangaa hawapimi presha zao halafu wanaenda kubugia K Vant wanagonga na Erecto matokeo yake anakuwa mtu wa kukaa ndani Mademu wanamkimbia.
 
Hili zimwi siijui kama nitapona..

Niko addicted na alcohol saa 12 jioni nimepiga tizi jasho kibao.

Chakushangaza saa 3 usiku nipo kwenye bia.

Ila nikaamua kulamba konyagi na ndimu za kutosha. Mtaalamu hapo vipi. Leo nimepiga konyagi nikichanganya na juis ya limao. Japo nahisi kilevi ila limao likikuwa Kwa wingi na sijalewa kivileeee. Najielewa vema
 
Hili zimwi siijui kama nitapona..

Niko addicted na alcohol saa 12 jioni nimepiga tizi jasho kibao.

Chakushangaza saa 3 usiku nipo kwenye bia.

Ila nikaamua kulamba konyagi na ndimu za kutosha. Mtaalamu hapo vipi. Leo nimepiga konyagi nikichanganya na juis ya limao. Japo nahisi kilevi ila limao likikuwa Kwa wingi na sijalewa kivileeee. Najielewa vema
@Bujibuji Simba Nyamaume njoo muone gILeSi huko[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Huu uzi umepata nguvu kwa sababu ndani yake kuna mambo na ngono na maudhui kama hayo, ambao kwa sasa sisi wabongo ndio mwelekeo wetu.

Yote ya yote ni uzi mzuri sana ambao kila mtu anapaswa auprint kwenye hard paper na pengine kubandika ukutani sebuleni na chumbani ili kila siku ukukumbushe kikupasacho kutenda kama kijana.
 
Kikubwa afya,unaweza kuwa hai na maisha yakakuchapa,magonjwa yanakuandama,ukatamani bora usingezaliwaga.
Kuimantain afya ndo inahitika hela na kuna wengine uwezo hauruhusu, mtu ambae hata kupata milo miwili kwa siku utata alafu umawambie ale matunda, afanye mazoezi, anunue vitabu kujisomea atakuelewa kweli? ndio maana nikasema kikubwa uhai yaani fanya mpaka pale uwezo wako unapoishia uko kwengine kunapobaki we shukuru tu upo hai.. anyway kama upo vzr kiuchumi uenda unaweza usinielewe ninachomaanisha
 
Umeongea ukweli,kama wapo watakao kuelewa watafaidika na ushauri wako,
Nina 48 na nimepata kisukari kipndi cha mafanikio yangu,ninachotaka napata ila ninamisi maisha halisi niliyojioangia iwapo ntafanikiwa,nilitamani niowe wake watatu ila sasa siweiz
Kuna vyakula natamani sana kula hivi sasa ni sumu kwangu nawanunulia watu tu na watoto wangu
Kuwa makini na kisukari ndugu
Kuna watu wengi watakufata kuwa wana dawa na watakula pesa zako na unabaki na kisukari chako hivho hivyo
Nayoandika hapa spambi habari ninapambana na hii hali wakati wote nikilazimisha furaha
KUWENI MAKINI KUJIRINDA DHIDI YA KISUKALI
 
Umeongea ukweli,kama wapo watakao kuelewa watafaidika na ushauri wako,
Nina 48 na nimepata kisukari kipndi cha mafanikio yangu,ninachotaka napata ila ninamisi maisha halisi niliyojioangia iwapo ntafanikiwa,nilitamani niowe wake watatu ila sasa siweiz
Kuna vyakula natamani sana kula hivi sasa ni sumu kwangu nawanunulia watu tu na watoto wangu
Kuwa makini na kisukari ndugu
Kuna watu wengi watakufata kuwa wana dawa na watakula pesa zako na unabaki na kisukari chako hivho hivyo
Nayoandika hapa spambi habari ninapambana na hii hali wakati wote nikilazimisha furaha
KUWENI MAKINI KUJIRINDA DHIDI YA KISUKALI
Pole sana Mkuu, kwahiyo dogodogo hupigi tena? Unaishia kula kwa macho tu..
 
Dunia yetu kila siku inatuonyesha watu wanavyokula bata viwanja mbalimbali lakini hatuoni foleni za clinic watu wanavyowahi foleni alfajili za matibabu muhimbili etc.Rate ya pressure na sukari ni kubwa Sana na now vijana above 35 ndio wanashika Kasi .. zamani ilikuwa 40 and above lakini saiv ni 30 and above ..life style ..unakuta kijana wa 30s anakitambi halafu anachukilia poa kabisa na anajiona maisha yamemkubali
 
Hili zimwi siijui kama nitapona..

Niko addicted na alcohol saa 12 jioni nimepiga tizi jasho kibao.

Chakushangaza saa 3 usiku nipo kwenye bia.

Ila nikaamua kulamba konyagi na ndimu za kutosha. Mtaalamu hapo vipi. Leo nimepiga konyagi nikichanganya na juis ya limao. Japo nahisi kilevi ila limao likikuwa Kwa wingi na sijalewa kivileeee. Najielewa vema
Spirit sio nzuri, kunywa light beer kama Windhoek, Heineken na frying fish au ukitaka kunywa hizi dry kama savanna na desperados
 
Vyote hivi nimekua navizingatia, nakiri ni raha sana yaani hata kitandani mke hupenda shughuli yenyewe na hata mchepuko sijawai kumuacha salama....sinywi pombe, sivuti sigara, nakula lishe bora, mazoezi kwa kwenda mbele fulu kujiachia...
 
Back
Top Bottom