Kijana jitunze, kuteremkia miaka 40+ kuna zimwi linaitwa Kisukari na Presha. Mkeo atakuvumilia?

Kwema Wakuu!

Hatufuatiliani wala hatupangiani maisha. Ila tunakumbushana huku nami nikijikumbusha pia Kwa Nia nzuri tuu. Ili baadaye tusijekujikuta katika Huzuni kuu.

Vijana tunapoambiwa tule na tunywe Kwa nidhamu sio Kwa sababu tunaonewa wivu au kuna mtu anataka kuwa juu yetu Kwa kutupa amri. HASHA! Bali ni Kwa faida yetu.

Kisukari na Presha sio magonjwa mazuri Kwa ustawi wa Ndoa zetu. Ukisikia pigo Baya basi ni kukosa nguvu za kiume. Tena Kwa miaka 40 Kwa mwanaume bado ni kijana. Na Kwa bahati nzuri miaka hiyo wengi neema ndio zinazidi kufunguka na wamesha-settle. Sasa ume-settle halafu unajikuta huna nguvu za kiume. Asikuambie mtu inahuzunisha Sana..

Presha na kisukari yatakufanya ukose Raha ya maisha sio tuu kwenye ndoa Bali hata katika ulaji wako. Utapangiwa nini ule na kipi usile. Vyakula vizuri utabaki kuvitazama tuu, utakula chukuchuku na michemsho mpaka Ulie.

Ni akheri ujipangie sasa hivi Kula Milo mizuri Kwa kufuata kanuni za Afya ya Mwili. Na ni akheri magonjwa hayo yakupate too late yaani huko miaka ya 80+ lakini sio 40+.

Ni hatari na utateseka Sana. Miaka 80+ huna ulichobakiza, hata wewe mwenyewe utakiri kuwa umekula chumvi nyingi vyakutosha. Lakini sio miaka 40-60. Hiyo ni miaka michache Sana.

Ukiona Taikon anaelezea jambo fulani basi kaa nalo macho, lizingatie Sana. Kwa sababu Taikon nipo kwaajili ya kujenga na wala sio kubomoa.

1. Kula na kunywa vizuri,
i. Kula Mbomboga Kwa wingi, kula Protein Kama nyama nyeupe, maziwa, mayai, Kwa wingi,
Kula wanga kidogo Sana. Mfano unapika maharage mengi halafu unakula na wali kidunchu, au ugali kidogo na Samaki au nyama au maharage mengi.

ii. Matunda, pendelea Kula matunda,
Kama umeoa, pendelea Ndizi zilizoiva angalau kila siku moja hasa usiku, hii itafanya uume wako kuwa na nguvu kutokana na madini ya Potassium.

Mkeo aweke Kachumburi yenye Nyanya, vitunguu, limao na pilipili hizi zinaongeza Libido.
Safisha figo Kwa Matikiti, matango, usisahau mapapai na maembe, pia machungwa huku utapata vitamini

Weka chumvi kiasi yenye ladha ya Kwa mbali. Usiweke chumvi nyingi. Kuweka chumvi nyingi kuna sababisha hatari ya kupata Presha "Hypertension" ambayo sio nzuri Kwa Afya yako.

Kula Milo miwili ukiwa age ya 25-50 iwe balanced.

iii. Kunywa maji mengi, angalau Lita mbili na nusu mpaka tatu na nusu Kwa siku.
Pombe kunywa kiasi Kwa STAREHE sio kujiumiza. Angalau kwa wiki mara moja na hakikisha usinywe mpaka ukazima.

Maji mengi ni dawa kwani yanafanya seli za mwili wako kufanya kazi Kwa ufanisi zaidi. Maji hupunguza pia sumu mwilini na kuufanya mwili wako kuwa na Nuru.

Yaani mtu anayezingatia kunywa maji ngozi yake hung'aa

Pia maji mengi husababisha mtu kutokuzeeka Kwa haraka. Na hii ni kutokana na Uzalishwaji wa seli za mwili kufanyika Kwa ufanisi

2. Fanya mazoezi,
Mazoezi hujenga mwili na kuufanya kuwa na Afya, kwani hufanya mzunguko WA damu kufanya kazi vizuri. Kumbuka Damu ndio hubeba virutubisho na kuvisafitisha mwilini. Kumbuka pia ndani ya damu ndio kuna Seli nyeupe zinazolinda mwili dhidi ya magonjwa, Seli nyekundu ambazo husafirisha hewa ya Oksijeni kuzipa Seli, tishu na ogani Uhai. Hasahasa Ubongo.

Hii ni kusema mazoezi yanaimarisha ufanyaji kazi WA viungo vya Mwili Kama vile Ubongo. Hii inafanya akili kuwa active.

Aina ya mazoezi
i. . Mazoezi ya Mwili
Haya yanalenga zaidi viungo na organ za mwili. Kukimbia, Push-up n.k.

ii. Mazoezi ya Akili/Ufahamu.
Haya yanalenga zaidi tafakuri, uchanganuzi, uchambuzi, n.k. haya ni Kwa kusoma Nyaraka na vitabu, michezo na Bangua bongo, Game zinazoshughulisha akili n.k.
Pia mazoezi ya ubongo hufanyika Kwa kujaribu kufanya vitu vipya ili kutafuta changamoto mpya. Kama ni biashara, au kazi au miradi unaanzisha ili akili ipate changamoto mpya.

iii. Mazoezi ya Kiroho na Nafsi.
Haya hulenga zaidi roho na Nafsi yako.
Kudhibiti Nafsi yako na matamanio yake, mfano Kufunga Kula na kunywa,
Kama unapenda kunywa pombe kujizuia kutokunywa Kwa muda wa siku kadhaa. Kama unapenda Kulala na wanawake, kujizuia hata Kwa miezi sita bila kuchepuka, hayo ni mazoezi ya kiroho na nafsi.

Pia kutoa Zaka au Sadaka Ile inayouma. Ni zoezi la Nafsi au kiroho.

Hii itakusaidia kujidhibiti, pia kuzuia Nyege mshindo au ukosefu wa maamuzi.

3. Mapumziko na Burudani/STAREHE.
Angalau Kwa siku ulale masaa yasiyopungua Nane.
Starehe au burudani angalau Kwa wiki au Kwa mwezi mara moja. Hii itakufanya usiyachoke maisha na kuyaona hayana maana.

Usingizi utakusaidia kutunza Ubongo wako na hii itakusaidia nyakati za uzeeni kwani utakuwa haupotezi kumbukumbu kijinga jinga.

Kabla watu hawajaona uzee wako wewe mwenyewe utaanza kuuona Kwanza Kwa kujikuta unasahau sahau mambo, na hiyo huanza kutokea miaka 30+ kama hutokuwa mtu wa kuzingatia mapumziko.

Kijana wa sasa unapaswa ujidhibiti mwenyewe ili isijekula kwako ufikishapo miaka 40.
Hakuna kitu kibaya Kama kufikisha umri huo yaani 40+ halafu ujikute hauna pesa, halafu magonjwa Kama kisukari na Presha vikupige. Ni hatari Sana.

Kupigiwa nje nje! Yaani mwanamke wako wala hatakuwa na Woga, nawe utakuwa unajua na chakumfanya hauna.

Wale mnaolalamika andiko refu nimewasikia. Nipumzike sasa!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Sijakuelewa kwa sababu mwanzo ulisema utapangiwa kula hivi au vile. Mwisho ukajumuisha watu wale vyakula vile vile ulivokataa mwanzo. Kifupi mimi naona umefeli kwenye uwasilishaji wa hoja yako.
 
Upo sahihi kuwa umefeli kuelewa uwasilishaji wangu.
Hilo kwangu sio tatizo mtu asiponielewa.
Kwani najua watu wanatofautiana Uelewa, na siku zote ili unielewe itakupasa uwe na uelewa kuanzia wa Kati kwenda Uelewa wa juu.
 
Rudia tena kusoma alafu uje na hiyo conclusion tena, fasihi siku zote huwa haikubaliwi kwa asilimia 100 na hadhara kama unavyotaka kuaminisha jukwaa. Na hiyo haikupi wewe kuwa na uelewa wa juu kama unavyojitanabaisha. Uelewa wa mtu haujengwi katika angle moja. Naamini kwamba hakuna tajiri asiyekuwa na cha kupokea na wala maskini asiyekuwa na chakutoa. Hivyo nakushangaa mtu unayejiita mwanafasihi ulazimishe andiko kukubaliwa na kila msomaji. Umeongea mwanzo kuhusu mpangilio wa kula, lakini kati ukasema "utapangiwa vitu vya kula mpaka ukome'' mwisho ukarudia tena kupanga vitu gani watu wale, wewe una uelewa wa juu kweli? Acha wanaomudu kula wanavyotaka wale, wewe unayekula unachopata nawe pambana kimpango wako. Mwisho siku kufa kupo na kwa mjibu wa biblia maisha yetu ya kuishi hapa duniani ni miaka 60 tu.
Sipingani na wewe ktk mpangilio wa vyakula na kufanya mazoezi, lah hasha. Pia tambua siyo wote wanaougua inatokana na chakula. Na mbona kila mara tunawaza sana nguvu za kiume?
 
Elewa kadiri ya Uelewa wako.
Sitaki uelewe vile ninavyoelewa Mimi au walivyoelewa wengine waliochangia,

KAZI yangu ni kuandika Kwa Uelewa wangu, kazi yako msomaji ni kuelewa nilichoandika Kwa Uelewa wako.
Umeelewa au haujaelewa Hilo halipo juu yangu.

Fasihi ndio ipo hivyo,
Hayo mengine hayana maana ikiwa kuna kitu umekipata au haujakipata katika andiko hili.

😀😀
 
Kwema Wakuu!

Hatufuatiliani wala hatupangiani maisha. Ila tunakumbushana huku nami nikijikumbusha pia Kwa Nia nzuri tuu. Ili baadaye tusijekujikuta katika Huzuni kuu.

Vijana tunapoambiwa tule na tunywe Kwa nidhamu sio Kwa sababu tunaonewa wivu au kuna mtu anataka kuwa juu yetu Kwa kutupa amri. HASHA! Bali ni Kwa faida yetu.

Kisukari na Presha sio magonjwa mazuri Kwa ustawi wa Ndoa zetu. Ukisikia pigo Baya basi ni kukosa nguvu za kiume. Tena Kwa miaka 40 Kwa mwanaume bado ni kijana. Na Kwa bahati nzuri miaka hiyo wengi neema ndio zinazidi kufunguka na wamesha-settle. Sasa ume-settle halafu unajikuta huna nguvu za kiume. Asikuambie mtu inahuzunisha Sana..

Presha na kisukari yatakufanya ukose Raha ya maisha sio tuu kwenye ndoa Bali hata katika ulaji wako. Utapangiwa nini ule na kipi usile. Vyakula vizuri utabaki kuvitazama tuu, utakula chukuchuku na michemsho mpaka Ulie.

Ni akheri ujipangie sasa hivi Kula Milo mizuri Kwa kufuata kanuni za Afya ya Mwili. Na ni akheri magonjwa hayo yakupate too late yaani huko miaka ya 80+ lakini sio 40+.

Ni hatari na utateseka Sana. Miaka 80+ huna ulichobakiza, hata wewe mwenyewe utakiri kuwa umekula chumvi nyingi vyakutosha. Lakini sio miaka 40-60. Hiyo ni miaka michache Sana.

Ukiona Taikon anaelezea jambo fulani basi kaa nalo macho, lizingatie Sana. Kwa sababu Taikon nipo kwaajili ya kujenga na wala sio kubomoa.

1. Kula na kunywa vizuri,
i. Kula Mbomboga Kwa wingi, kula Protein Kama nyama nyeupe, maziwa, mayai, Kwa wingi,
Kula wanga kidogo Sana. Mfano unapika maharage mengi halafu unakula na wali kidunchu, au ugali kidogo na Samaki au nyama au maharage mengi.

ii. Matunda, pendelea Kula matunda,
Kama umeoa, pendelea Ndizi zilizoiva angalau kila siku moja hasa usiku, hii itafanya uume wako kuwa na nguvu kutokana na madini ya Potassium.

Mkeo aweke Kachumburi yenye Nyanya, vitunguu, limao na pilipili hizi zinaongeza Libido.
Safisha figo Kwa Matikiti, matango, usisahau mapapai na maembe, pia machungwa huku utapata vitamini

Weka chumvi kiasi yenye ladha ya Kwa mbali. Usiweke chumvi nyingi. Kuweka chumvi nyingi kuna sababisha hatari ya kupata Presha "Hypertension" ambayo sio nzuri Kwa Afya yako.

Kula Milo miwili ukiwa age ya 25-50 iwe balanced.

iii. Kunywa maji mengi, angalau Lita mbili na nusu mpaka tatu na nusu Kwa siku.
Pombe kunywa kiasi Kwa STAREHE sio kujiumiza. Angalau kwa wiki mara moja na hakikisha usinywe mpaka ukazima.

Maji mengi ni dawa kwani yanafanya seli za mwili wako kufanya kazi Kwa ufanisi zaidi. Maji hupunguza pia sumu mwilini na kuufanya mwili wako kuwa na Nuru.

Yaani mtu anayezingatia kunywa maji ngozi yake hung'aa

Pia maji mengi husababisha mtu kutokuzeeka Kwa haraka. Na hii ni kutokana na Uzalishwaji wa seli za mwili kufanyika Kwa ufanisi

2. Fanya mazoezi,
Mazoezi hujenga mwili na kuufanya kuwa na Afya, kwani hufanya mzunguko WA damu kufanya kazi vizuri. Kumbuka Damu ndio hubeba virutubisho na kuvisafitisha mwilini. Kumbuka pia ndani ya damu ndio kuna Seli nyeupe zinazolinda mwili dhidi ya magonjwa, Seli nyekundu ambazo husafirisha hewa ya Oksijeni kuzipa Seli, tishu na ogani Uhai. Hasahasa Ubongo.

Hii ni kusema mazoezi yanaimarisha ufanyaji kazi WA viungo vya Mwili Kama vile Ubongo. Hii inafanya akili kuwa active.

Aina ya mazoezi
i. . Mazoezi ya Mwili
Haya yanalenga zaidi viungo na organ za mwili. Kukimbia, Push-up n.k.

ii. Mazoezi ya Akili/Ufahamu.
Haya yanalenga zaidi tafakuri, uchanganuzi, uchambuzi, n.k. haya ni Kwa kusoma Nyaraka na vitabu, michezo na Bangua bongo, Game zinazoshughulisha akili n.k.
Pia mazoezi ya ubongo hufanyika Kwa kujaribu kufanya vitu vipya ili kutafuta changamoto mpya. Kama ni biashara, au kazi au miradi unaanzisha ili akili ipate changamoto mpya.

iii. Mazoezi ya Kiroho na Nafsi.
Haya hulenga zaidi roho na Nafsi yako.
Kudhibiti Nafsi yako na matamanio yake, mfano Kufunga Kula na kunywa,
Kama unapenda kunywa pombe kujizuia kutokunywa Kwa muda wa siku kadhaa. Kama unapenda Kulala na wanawake, kujizuia hata Kwa miezi sita bila kuchepuka, hayo ni mazoezi ya kiroho na nafsi.

Pia kutoa Zaka au Sadaka Ile inayouma. Ni zoezi la Nafsi au kiroho.

Hii itakusaidia kujidhibiti, pia kuzuia Nyege mshindo au ukosefu wa maamuzi.

3. Mapumziko na Burudani/STAREHE.
Angalau Kwa siku ulale masaa yasiyopungua Nane.
Starehe au burudani angalau Kwa wiki au Kwa mwezi mara moja. Hii itakufanya usiyachoke maisha na kuyaona hayana maana.

Usingizi utakusaidia kutunza Ubongo wako na hii itakusaidia nyakati za uzeeni kwani utakuwa haupotezi kumbukumbu kijinga jinga.

Kabla watu hawajaona uzee wako wewe mwenyewe utaanza kuuona Kwanza Kwa kujikuta unasahau sahau mambo, na hiyo huanza kutokea miaka 30+ kama hutokuwa mtu wa kuzingatia mapumziko.

Kijana wa sasa unapaswa ujidhibiti mwenyewe ili isijekula kwako ufikishapo miaka 40.
Hakuna kitu kibaya Kama kufikisha umri huo yaani 40+ halafu ujikute hauna pesa, halafu magonjwa Kama kisukari na Presha vikupige. Ni hatari Sana.

Kupigiwa nje nje! Yaani mwanamke wako wala hatakuwa na Woga, nawe utakuwa unajua na chakumfanya hauna.

Wale mnaolalamika andiko refu nimewasikia. Nipumzike sasa!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Mada nzuri sana.Allah akubariki
 
Huwezi elewa mpaka yakukute.

Ukiwa katika Hali hiyo unanyimwa kabisa na huna lakufanya.
Na hakuna mwanamke atakayekutaka!

Sasa ni Bora uwe na Afya njema ili hata mkeo akifanya hayo uwe na jeuri ya kutafuta mwingine, sio kulialia na kujinyenyekeza ili akufichie Siri yako kuu
Ni kweli,Allah akubariki sana.
 
Ila mkuu unaongea kwa hisia sana! Kuna jamaa yangu ana mke bomba kweli kweli, sasa ana hiyo changamoto kweli mke amekuja kumfumania yuko na msela ameinamishwa! Mke huku nje analalamika mme ana kisukari shughuli hawezi tena sasa mimi ningefanyaje? Kazi kweli kweli!
Mtihani.
 
Heri ya sukari unaweza epuka kwa kua selective kwenye vyakula, Ila presha inaweza kukuandama tu kutokana na hasling zako, mfano unafanya kazi za pressure sanaa hasa kwa ndugu zetu makanjubai amini nakwambia ukifikia fote wewe jiandae tu na magonjwa ya pressure. (nasema kutokana na experience).
 
Noma sana
 
Sasa mwanaume anakuwa zaidi lakini Hana nguvu[emoji23][emoji23]
Hapo ndio tofauti ilipo,
Ndio maana mada hii inalenga kujitunza
Hata mwanamke naye libido inapungua bhana, tena sana[emoji23] hii ni kwa wote. Me anapungua nguvu ila ke libido inakuwa ndogo mno, ngoma draw
 
Kwema Wakuu!

Hatufuatiliani wala hatupangiani maisha. Ila tunakumbushana huku nami nikijikumbusha pia Kwa Nia nzuri tuu. Ili baadaye tusijekujikuta katika Huzuni kuu.

Vijana tunapoambiwa tule na tunywe Kwa nidhamu sio Kwa sababu tunaonewa wivu au kuna mtu anataka kuwa juu yetu Kwa kutupa amri. HASHA! Bali ni Kwa faida yetu.

Kisukari na Presha sio magonjwa mazuri Kwa ustawi wa Ndoa zetu. Ukisikia pigo Baya basi ni kukosa nguvu za kiume. Tena Kwa miaka 40 Kwa mwanaume bado ni kijana. Na Kwa bahati nzuri miaka hiyo wengi neema ndio zinazidi kufunguka na wamesha-settle. Sasa ume-settle halafu unajikuta huna nguvu za kiume. Asikuambie mtu inahuzunisha Sana..

Presha na kisukari yatakufanya ukose Raha ya maisha sio tuu kwenye ndoa Bali hata katika ulaji wako. Utapangiwa nini ule na kipi usile. Vyakula vizuri utabaki kuvitazama tuu, utakula chukuchuku na michemsho mpaka Ulie.

Ni akheri ujipangie sasa hivi Kula Milo mizuri Kwa kufuata kanuni za Afya ya Mwili. Na ni akheri magonjwa hayo yakupate too late yaani huko miaka ya 80+ lakini sio 40+.

Ni hatari na utateseka Sana. Miaka 80+ huna ulichobakiza, hata wewe mwenyewe utakiri kuwa umekula chumvi nyingi vyakutosha. Lakini sio miaka 40-60. Hiyo ni miaka michache Sana.

Ukiona Taikon anaelezea jambo fulani basi kaa nalo macho, lizingatie Sana. Kwa sababu Taikon nipo kwaajili ya kujenga na wala sio kubomoa.

1. Kula na kunywa vizuri,
i. Kula Mbomboga Kwa wingi, kula Protein Kama nyama nyeupe, maziwa, mayai, Kwa wingi,
Kula wanga kidogo Sana. Mfano unapika maharage mengi halafu unakula na wali kidunchu, au ugali kidogo na Samaki au nyama au maharage mengi.

ii. Matunda, pendelea Kula matunda,
Kama umeoa, pendelea Ndizi zilizoiva angalau kila siku moja hasa usiku, hii itafanya uume wako kuwa na nguvu kutokana na madini ya Potassium.

Mkeo aweke Kachumburi yenye Nyanya, vitunguu, limao na pilipili hizi zinaongeza Libido.
Safisha figo Kwa Matikiti, matango, usisahau mapapai na maembe, pia machungwa huku utapata vitamini

Weka chumvi kiasi yenye ladha ya Kwa mbali. Usiweke chumvi nyingi. Kuweka chumvi nyingi kuna sababisha hatari ya kupata Presha "Hypertension" ambayo sio nzuri Kwa Afya yako.

Kula Milo miwili ukiwa age ya 25-50 iwe balanced.

iii. Kunywa maji mengi, angalau Lita mbili na nusu mpaka tatu na nusu Kwa siku.
Pombe kunywa kiasi Kwa STAREHE sio kujiumiza. Angalau kwa wiki mara moja na hakikisha usinywe mpaka ukazima.

Maji mengi ni dawa kwani yanafanya seli za mwili wako kufanya kazi Kwa ufanisi zaidi. Maji hupunguza pia sumu mwilini na kuufanya mwili wako kuwa na Nuru.

Yaani mtu anayezingatia kunywa maji ngozi yake hung'aa

Pia maji mengi husababisha mtu kutokuzeeka Kwa haraka. Na hii ni kutokana na Uzalishwaji wa seli za mwili kufanyika Kwa ufanisi

2. Fanya mazoezi,
Mazoezi hujenga mwili na kuufanya kuwa na Afya, kwani hufanya mzunguko WA damu kufanya kazi vizuri. Kumbuka Damu ndio hubeba virutubisho na kuvisafitisha mwilini. Kumbuka pia ndani ya damu ndio kuna Seli nyeupe zinazolinda mwili dhidi ya magonjwa, Seli nyekundu ambazo husafirisha hewa ya Oksijeni kuzipa Seli, tishu na ogani Uhai. Hasahasa Ubongo.

Hii ni kusema mazoezi yanaimarisha ufanyaji kazi WA viungo vya Mwili Kama vile Ubongo. Hii inafanya akili kuwa active.

Aina ya mazoezi
i. . Mazoezi ya Mwili
Haya yanalenga zaidi viungo na organ za mwili. Kukimbia, Push-up n.k.

ii. Mazoezi ya Akili/Ufahamu.
Haya yanalenga zaidi tafakuri, uchanganuzi, uchambuzi, n.k. haya ni Kwa kusoma Nyaraka na vitabu, michezo na Bangua bongo, Game zinazoshughulisha akili n.k.
Pia mazoezi ya ubongo hufanyika Kwa kujaribu kufanya vitu vipya ili kutafuta changamoto mpya. Kama ni biashara, au kazi au miradi unaanzisha ili akili ipate changamoto mpya.

iii. Mazoezi ya Kiroho na Nafsi.
Haya hulenga zaidi roho na Nafsi yako.
Kudhibiti Nafsi yako na matamanio yake, mfano Kufunga Kula na kunywa,
Kama unapenda kunywa pombe kujizuia kutokunywa Kwa muda wa siku kadhaa. Kama unapenda Kulala na wanawake, kujizuia hata Kwa miezi sita bila kuchepuka, hayo ni mazoezi ya kiroho na nafsi.

Pia kutoa Zaka au Sadaka Ile inayouma. Ni zoezi la Nafsi au kiroho.

Hii itakusaidia kujidhibiti, pia kuzuia Nyege mshindo au ukosefu wa maamuzi.

3. Mapumziko na Burudani/STAREHE.
Angalau Kwa siku ulale masaa yasiyopungua Nane.
Starehe au burudani angalau Kwa wiki au Kwa mwezi mara moja. Hii itakufanya usiyachoke maisha na kuyaona hayana maana.

Usingizi utakusaidia kutunza Ubongo wako na hii itakusaidia nyakati za uzeeni kwani utakuwa haupotezi kumbukumbu kijinga jinga.

Kabla watu hawajaona uzee wako wewe mwenyewe utaanza kuuona Kwanza Kwa kujikuta unasahau sahau mambo, na hiyo huanza kutokea miaka 30+ kama hutokuwa mtu wa kuzingatia mapumziko.

Kijana wa sasa unapaswa ujidhibiti mwenyewe ili isijekula kwako ufikishapo miaka 40.
Hakuna kitu kibaya Kama kufikisha umri huo yaani 40+ halafu ujikute hauna pesa, halafu magonjwa Kama kisukari na Presha vikupige. Ni hatari Sana.

Kupigiwa nje nje! Yaani mwanamke wako wala hatakuwa na Woga, nawe utakuwa unajua na chakumfanya hauna.

Wale mnaolalamika andiko refu nimewasikia. Nipumzike sasa!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Ushauri bora sana mkuu,asante!
 
Kwa kiasi kikubwa Sukari na presha ni matokeo ya mitindo mibaya ya maisha, Kula na kunywa.
Wachache huwa nayo ya kurithi.
Ukiwa na "mitindo mibaya ya maisha, kula na kunywa," mwili unasusa kuzalisha insulin ?????

Answer that.
 
Back
Top Bottom