Uchaguzi 2020 Kijana mbaroni kwa kuchana picha za Magufuli

Kwamujibu wa sheria zauchaguzi hairuhusiwi kuchana mabango ya wagombea kama wahusika wakiona na kutoa taarifa na ukajulikana na kukawa na ushahidi unaingia matatani.
Tuwaache mbuzi wachane ila sisi wanadamu tuache huo upuuzi. Siasa nikuvumiliana

Sent from my Infinix X603 using JamiiForums mobile app
Swali ni je, kwanini za upande mwingine tumeshuhudia hadi bendera kushushwa ila sheria haichukui mkondo wake?
 
Sisi picha huwa tunazichania mioyoni mwetu hizo za ukutani tumewaachia Mbuzi wapenda Mabadiliko
 
🤣🤣🤣 wajitokeze wenzake kutoka humu Jf wakamtoe maana ni kijana wa humuhumu. Nadhani akiwa huko ndo atajua Sasa kuwa ile support ya nyuma ya keyboard, haina uhalisia wowote uraiani.

Kama unamchukia Rais na hutaki aendelee kukaa madarakani, kwanini usihamasishe Vijana wenzio mkapige kura kwa wingi? Kwahiyo kuchana hizo picha kungebadilisha Nini Sasa🤔.
 
POLISI mkoani Morogoro wamemkamata mtu aliyetambuliwa kwa jina la Isihaka Exavery (20) mkazi wa Mkundi, manispaa ya Morogoro kwa tuhuma za kuchana picha za mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Magufuli.

Kijana huyo pia anatuhumiwa kuchana picha za mgombea udiwani kata ya Mkundi kupitia CCM .

Kamanda wa Polisi wa mkoa huo Wilbroad Mutafungwa, alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea Oktoba 15 mwaka huu saa tano asubuhi katika mtaa wa Mlimani, kata ya Mkundi, Manispaa ya Morogoro.

Kamanda Mutafungwa alisema kijana huyo alichana picha za Magufuli na za ombea Seif Zahoro Chomoka, akakimbia.

Alisema, Polisi baada ya kupata taarifa hizo walifika eneo la tukio na kuanza msako na kwa kushirikiana na wananchi walioshuhudia tukio hilo walimkamata mtuhumiwa huyo na picha alizochana.

Kamanda Mutafungwa alisema Polisi wanaendelea kumhoji kijana huyo na kwamba upepelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani.
Upuuzi mtupu Polisi kushupalia hili.
 
Huku kwetu, mabango na picha za wagombea zimekuwa zikichanwa .
hii sio tabia nzuri ,bora huyo aliekamatwa atakuwa mfano kwa wengine.
 
POLISI mkoani Morogoro wamemkamata mtu aliyetambuliwa kwa jina la Isihaka Exavery (20) mkazi wa Mkundi, manispaa ya Morogoro kwa tuhuma za kuchana picha za mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Magufuli.

Kijana huyo pia anatuhumiwa kuchana picha za mgombea udiwani kata ya Mkundi kupitia CCM .

Kamanda wa Polisi wa mkoa huo Wilbroad Mutafungwa, alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea Oktoba 15 mwaka huu saa tano asubuhi katika mtaa wa Mlimani, kata ya Mkundi, Manispaa ya Morogoro.

Kamanda Mutafungwa alisema kijana huyo alichana picha za Magufuli na za ombea Seif Zahoro Chomoka, akakimbia.

Alisema, Polisi baada ya kupata taarifa hizo walifika eneo la tukio na kuanza msako na kwa kushirikiana na wananchi walioshuhudia tukio hilo walimkamata mtuhumiwa huyo na picha alizochana.

Kamanda Mutafungwa alisema Polisi wanaendelea kumhoji kijana huyo na kwamba upepelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani.
 
Huyo RPC amekosa kazi ya kufanya, kule Songwe vijana wahuni wa ccm walishusha bendera ya Chadema mbona hatukusikia polisi wamesema lolote, huu Utawala double standards.
Usipoelewa siasa,bora usijihusishe na siasa ila fanya kutekeleza yale sheria inasema juu ya maamuzi yanayotokokana na siasa
La sivyo mihemko yenye asila kali itakugharimu wewe pamoja na familia yako,
Hapo atasomewa vifungu mpaka basi
 
Kule Daresalama tuliona youtube clip ikimuonesha mbuzi akiwa anachana bango la Gwajima, hapo Mambosasa atamshtaki nani ??.
 
Mbuzi wa Dar utadhani hawana mwenyewe, wana akili kuliko wakazi wengi tu.
Mbuzi kuchana mabango si kwamba wanaelewa nini wanafanya ila ni ile halufu iliyopo kwenye karatasi huwavutia nakuhisi ni kitu cha kutafunika
Kwa nini ccm?
Ukiangalia kiasi cha mabango yanayopatikana kwa wingi na kwa wepesi zaidi ni ccm kuliko chama kingine chochote kile,mfano huku niliko hakuna bango la chama kingine tofauti na CCM
 
POLISI mkoani Morogoro wamemkamata mtu aliyetambuliwa kwa jina la Isihaka Exavery (20) mkazi wa Mkundi, manispaa ya Morogoro kwa tuhuma za kuchana picha za mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Magufuli.

Kijana huyo pia anatuhumiwa kuchana picha za mgombea udiwani kata ya Mkundi kupitia CCM .

Kamanda wa Polisi wa mkoa huo Wilbroad Mutafungwa, alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea Oktoba 15 mwaka huu saa tano asubuhi katika mtaa wa Mlimani, kata ya Mkundi, Manispaa ya Morogoro.

Kamanda Mutafungwa alisema kijana huyo alichana picha za Magufuli na za ombea Seif Zahoro Chomoka, akakimbia.

Alisema, Polisi baada ya kupata taarifa hizo walifika eneo la tukio na kuanza msako na kwa kushirikiana na wananchi walioshuhudia tukio hilo walimkamata mtuhumiwa huyo na picha alizochana.

Kamanda Mutafungwa alisema Polisi wanaendelea kumhoji kijana huyo na kwamba upepelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani.
Hiyo kazi angeyaachia mabeberu ya Kawe tu yaliyohamia Moro hivi karibuni.... Pole yake!
 
Mbuzi kuchana mabango si kwamba wanaelewa nini wanafanya ila ni ile halufu iliyopo kwenye karatasi huwavutia nakuhisi ni kitu cha kutafunika
Kwa nini ccm?
Ukiangalia kiasi cha mabango yanayopatikana kwa wingi na kwa wepesi zaidi ni ccm kuliko chama kingine chochote kile,mfano huku niliko hakuna bango la chama kingine tofauti na CCM
Wewe uko wapi hapo Mkuu ??.
 
Back
Top Bottom