Uchaguzi 2020 Kijana mbaroni kwa kuchana picha za Magufuli

Uchaguzi 2020 Kijana mbaroni kwa kuchana picha za Magufuli

Vipi zinapochanwa za upinzani eg chadema?
Kwanza ukienda hata kutoa taarifa polisi watakuweka ndani wewe unaetoa taarifa na ukabambikiwa kesi ya kubaka!
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] wajitokeze wenzake kutoka humu Jf wakamtoe maana ni kijana wa humuhumu. Nadhani akiwa huko ndo atajua Sasa kuwa ile support ya nyuma ya keyboard, haina uhalisia wowote uraiani.

Kama unamchukia Rais na hutaki aendelee kukaa madarakani, kwanini usihamasishe Vijana wenzio mkapige kura kwa wingi? Kwahiyo kuchana hizo picha kungebadilisha Nini Sasa[emoji848].
Unatekenywa beki
 
Hivi Lissu yupo wapi Leo kwa kampeni? Eti makamanda

093ffc51-1138-4d86-8f8d-698a84dcf16b.jpg
 
Kwanza kuweka hayo mabango ni ufujaji wa fedha na ubadhilifu mkubwa
 
Mvua imenyesha last week na kuharibu hayo mabango na picha zao hatukuona wanasema kitu wala kuonekana kusikitika.

Wamuachie kijana wa watu. Mungu anawaona.
 
Nchi imekuwa ya ovyo hii, mbona mbuzi wakizitafuna hawawakamati??
 
POLISI mkoani Morogoro wamemkamata mtu aliyetambuliwa kwa jina la Isihaka Exavery (20) mkazi wa Mkundi, manispaa ya Morogoro kwa tuhuma za kuchana picha za mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Magufuli.

Kijana huyo pia anatuhumiwa kuchana picha za mgombea udiwani kata ya Mkundi kupitia CCM .

Kamanda wa Polisi wa mkoa huo Wilbroad Mutafungwa, alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea Oktoba 15 mwaka huu saa tano asubuhi katika mtaa wa Mlimani, kata ya Mkundi, Manispaa ya Morogoro.

Kamanda Mutafungwa alisema kijana huyo alichana picha za Magufuli na za ombea Seif Zahoro Chomoka, akakimbia.

Alisema, Polisi baada ya kupata taarifa hizo walifika eneo la tukio na kuanza msako na kwa kushirikiana na wananchi walioshuhudia tukio hilo walimkamata mtuhumiwa huyo na picha alizochana.

Kamanda Mutafungwa alisema Polisi wanaendelea kumhoji kijana huyo na kwamba upepelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani.
Hivi wale waliochana picha za chadema na kushusha bendera walikamatwa?
 
"Takwimu zao zinaonyesha hakuna dalili yoyote kwa Mgombea wa Chama cha Meko full kupata hata asilimia 40 ya kura. Chama cha Meko full wameshakata tamaa na ushindi. Kwa msingi huo wamepangwa kumtangaza Mgombea wa Chama Cha Meko full usiku wa manane.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom