sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
Ilikuwa ni mida ya saa 11 na robo hivi nikiwa nimetoka kazini nimeenda kiwanja flani kufanya mazoezi. nilifika nikaona kuna majabizano ya kelele kati ya watu wawili.. wa kwanza tumwite papai ni mrefu kiasi ila hana mwili wa mazoezi, wapili tumuite nazi huyu ni mfupi kuzidi X lakini ana mwili wa mazoezi.
Nazi alikuwa anauza simu yake kwa laki 3 japa mtaani lakini alikosa mteja, sasa akaenda kwa papai amsaidie kutafuta mteja, mzembe akapata mteja ambae yupo tayari kutoa laki 5 kwajili ya simu, mteja alifika uwanjani akampa nazi laki 5 sasa nazi akampa elf 50 papai, ndio hapo sasa papai akawa anataka laki 2 yake.
Papai akawa anafanya juhudi kumsimamisha nazi anaomba waongee basi ampe hata laki 1 na nusu iwe fair lakini Nazi akawa analeta ubabe hataki, Nazi kuonyesha ubabe si akamrushia ngumi Papai akawa anamwambia njoo uchukue kama unaweza huku kazipanga ngumi.
Papai alichofanya ni kama alimvamia hivi na uzito wake pale sakafuni akaanza kumpiga nazi makofi ya nguvu, hapo watu hatuamini tunachokiona aisee, leo Nazi vipi tena na alivyokuwa fiti vile! Nazi anabloku lakini wapi, Papai anazama kwenye mifuko Nazi akileta ubishi anaongeza makofi, Papai akazama mfukoni akachukua chake akawa anamkanya shoti aache dhulma.
Nazi akainuka kwa hasira anamkimbilia papai, watu wanamkamata aache lakini ni mbishi akaachiwa, Papai akamkwida akamuongezea makofi mawili tena akawa anamsisitiza aache, Papai alondoka uwanjani kuzuia fujo zaidi huku katuacha midomo wazi.
Quote Reply
Report Edit